Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Nimeumia sana moyoni!
Shule nyingi zinaendeshwa kwa Mihemiko na ushindani wa ajabu ajabu. Hawana ratiba za masomo kwa siku zinazojulikana kwa watoto.Shule zinawabebesha watoto mavitabu mengi hata ambayo siku hiyo hawatayatumia.sijui kwa nini hawatoagi ratiba ya vipindi ili mtoto aende na madaftari na vitabu vitakavyotumika siku hiyo.

Wanawakalisha sana watoto.watoto wanaishi kwa hofu ya mtihani siyo kujifunza na kuelewa.
 
Mtoto wa miaka 3 anaenda shulee? Seriously??
[emoji102] uwiiiiiih
 
Sasa nikuambie wazazi wasomi Ndo mabingwa wa huo upupu,na hv wako busy na kazi Ndo kabisaa
 
Mbaya zaidi wanayosomea Wala hayasaidii kwenye maisha ya kawaida
 
Ratiba yatakiwa izingatiwe.

Hapo ni mzazi kuandika kwenye diary kuwa ratiba ifuatwe, muwekee mtoto madaftari husika tu. Akichapwa nenda kapambane nao huko shuleni, wakimfukuza wakurudishie ADA
Unapohitaji ustawi wa jamii hapo si njiai mwafaka, ila unapotafufa utatuzi binafsi hapo utafanikiwa.
 
Watu wa Dar mnalalamika mno. Watoto wenyewe hao wanabeba begi kutoka mlango wa nyumba mpaka getini anakutana na school bus akifika shule analibebea mpaka darasani kwake. Mnawalea watoto ki mayai mno
Wakati mwingine ni muhimu kujichunguza binafsi kabla ya kusema ni nini unakiona kwenye kioo unachokitizama.
 
Mzazi ndo mwenye kosa.
Ukiaona dalili za ajabu mhamishe mtoto mpeleke shule ya kawaida ila mkazanie kusoma.

Kwa ujeuri wangu siwezi mpeleka.

Mtoto atasoma siku 5 pekee
 
Shule za serikali zinafuata mfumo huo darasa la kwanza na la pili muda wao wa kutoka ndio huo, kimbembe ni kwa hizi ingilishi midiamu
Ila sababu ni serikali kutoingilia kati.
Yatakiwa iwekwe sheria

Siku za kusoma ni 5 pekee

Muda wa kusoma mwisho saa 8

Ratiba ifuatwe
 
Mimi wa kwangu ndo natoka kuwapeleka saa hivi.

Vipindi wanaanza saa mbili.

Gari ya shule inapita saa 12, mda huo wanakuwa wamelala maana wanaamka saa 12 na robo.

Safi kabisa.

Kusoma si adhabu.
Tatizo ni wazazi wengi hawataki fanya majukumu yao. Wengine wanaachia boda boda wapeleke watoto shule.

Bora mtoto asome shule ya jirani
 
Pia, watoto wanatembea na mabegi utafikiri wanajifunza kuwa makuli. Mwishowe ni kesi za kutibu migongo ya vijana wadogo kuongezeka.

Watoto wanaopanda School Bus kwa kufuatwa mpaka getini nyumbani na kurudishwa,hayo mabegi wanatembea nayo muda gani? Au hapa unaongelea watoto wanaosoma Shule za Serikali wasiokuwa na usafiri?
 
Daah umeongea madini sana nilisoma tuu bila kuangalia Id yako ikabidi nishushe aisee watoto wanasoma kwa tabu sana kuanzia hizo gari wanazopanda na Serikali hata haifikirii kuwatolea kodi waagize bus nzuri watoto wetu wasione Elimu ni adhabu..
Tatizo kodi ikiondolewa gari litakuja ila matumizi yake yanakuwa tofauti
 
Siku ya kikao cha wazazi nikamuuliza MD akasema eti watoto wenyewe ndio wanapenda. Wazazi tuliikataa tukamtaka wafuate ratiba mtoto abebe kulingana na ratiba
Ila mtoto ni wako,wewe ndo watakiwa mwambia afuate ratiba kama inavyoelekeza
 

Noma sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…