Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Nimeumia sana moyoni!
Shule nyingi zinaendeshwa kwa Mihemiko na ushindani wa ajabu ajabu. Hawana ratiba za masomo kwa siku zinazojulikana kwa watoto.Shule zinawabebesha watoto mavitabu mengi hata ambayo siku hiyo hawatayatumia.sijui kwa nini hawatoagi ratiba ya vipindi ili mtoto aende na madaftari na vitabu vitakavyotumika siku hiyo.

Wanawakalisha sana watoto.watoto wanaishi kwa hofu ya mtihani siyo kujifunza na kuelewa.
 
Jana wangu wa miaka mi 3 naambiwa gari lake la sa moja lime change route kwahiyo natakiwa nimuandae sa kumi na moja na nusu awe tayari...halafu kurudi sa kumi na mbili na nusu jioni........ Dereva nimemwambia haiwezekani,mwenye shule nimemwambia kama itashindikana aende shule nyingine.
Mtoto wa miaka 3 anaenda shulee? Seriously??
[emoji102] uwiiiiiih
 
Ni ujinga na ulimbukeni wa elimu na asilimia kubwa ya wazazi wanaofanya hivyo ni wale ambao hawajaenda shule ila Mungu kawabariki kipato aisee hili kundi linatesa watoto mtoto darasa la pili apumziki kama hivyo kamamka sasa tisa anaenda shule kurudi nyumbani sasa tatu usiku maana.. akitoka shule anaenda tution yaani elimu inakuwa kama utumwa.
Sasa nikuambie wazazi wasomi Ndo mabingwa wa huo upupu,na hv wako busy na kazi Ndo kabisaa
 
Ukitaka kuelewa ni jinsi gani hii SYNDROME ya kufaulisha kwa MAUMIVU YOYOTE YAWAYO kwa mtoto ilivyobebwa na wazazi vs walimu.

1: Jaribu kulieleza hilo siku ya kikao cha wazazi na walimu.

2: Eleza kwenye grupu la usafiri la watoto wa shule

Utaonekana wewe ni mpinga elimu na ufaulu wa watoto.
Ni ulemavu tumeshatwishwa wazazi na wizara iko kimya.

Pia, watoto wanatembea na mabegi utafikiri wanajifunza kuwa makuli. Mwishowe ni kesi za kutibu migongo ya vijana wadogo kuongezeka.

Vijana wanafikia kuona shule kama adhabu na hatujui ni kwa kiadi gani tunawaumiza ubongo na kutengeneza magonjwa ya afya ya akili vs mengine physical.
Mbaya zaidi wanayosomea Wala hayasaidii kwenye maisha ya kawaida
 
Ratiba yatakiwa izingatiwe.

Hapo ni mzazi kuandika kwenye diary kuwa ratiba ifuatwe, muwekee mtoto madaftari husika tu. Akichapwa nenda kapambane nao huko shuleni, wakimfukuza wakurudishie ADA
Unapohitaji ustawi wa jamii hapo si njiai mwafaka, ila unapotafufa utatuzi binafsi hapo utafanikiwa.
 
Watu wa Dar mnalalamika mno. Watoto wenyewe hao wanabeba begi kutoka mlango wa nyumba mpaka getini anakutana na school bus akifika shule analibebea mpaka darasani kwake. Mnawalea watoto ki mayai mno
Wakati mwingine ni muhimu kujichunguza binafsi kabla ya kusema ni nini unakiona kwenye kioo unachokitizama.
 
Sio makubaliano mkuu. Naongelea kwa experience. Walipojulisha wazazi haikuwa na mjadala, ilikuwa ni taarifa.
Unaambiwa si moja kwa moja ila kwa kuashiria kuwa ukitaka mlete mwanao hutaki acha.
Sifa zao zinaathiri watoto kwa kiasi kikubwa.
Inafikia wakati mzazi na mtoto hamuonani kabisa. Ukiuliza elimu ya darasa la 7.
Mzazi ndo mwenye kosa.
Ukiaona dalili za ajabu mhamishe mtoto mpeleke shule ya kawaida ila mkazanie kusoma.

Kwa ujeuri wangu siwezi mpeleka.

Mtoto atasoma siku 5 pekee
 
Shule za serikali zinafuata mfumo huo darasa la kwanza na la pili muda wao wa kutoka ndio huo, kimbembe ni kwa hizi ingilishi midiamu
Ila sababu ni serikali kutoingilia kati.
Yatakiwa iwekwe sheria

Siku za kusoma ni 5 pekee

Muda wa kusoma mwisho saa 8

Ratiba ifuatwe
 
Mimi wa kwangu ndo natoka kuwapeleka saa hivi.

Vipindi wanaanza saa mbili.

Gari ya shule inapita saa 12, mda huo wanakuwa wamelala maana wanaamka saa 12 na robo.

Safi kabisa.

Kusoma si adhabu.
Tatizo ni wazazi wengi hawataki fanya majukumu yao. Wengine wanaachia boda boda wapeleke watoto shule.

Bora mtoto asome shule ya jirani
 
Pia, watoto wanatembea na mabegi utafikiri wanajifunza kuwa makuli. Mwishowe ni kesi za kutibu migongo ya vijana wadogo kuongezeka.

Watoto wanaopanda School Bus kwa kufuatwa mpaka getini nyumbani na kurudishwa,hayo mabegi wanatembea nayo muda gani? Au hapa unaongelea watoto wanaosoma Shule za Serikali wasiokuwa na usafiri?
 
Daah umeongea madini sana nilisoma tuu bila kuangalia Id yako ikabidi nishushe aisee watoto wanasoma kwa tabu sana kuanzia hizo gari wanazopanda na Serikali hata haifikirii kuwatolea kodi waagize bus nzuri watoto wetu wasione Elimu ni adhabu..
Tatizo kodi ikiondolewa gari litakuja ila matumizi yake yanakuwa tofauti
 
Siku ya kikao cha wazazi nikamuuliza MD akasema eti watoto wenyewe ndio wanapenda. Wazazi tuliikataa tukamtaka wafuate ratiba mtoto abebe kulingana na ratiba
Ila mtoto ni wako,wewe ndo watakiwa mwambia afuate ratiba kama inavyoelekeza
 
Leo nimshuka kutoka basi la mkoani mida ya around saa 9 usiku hapa stand ya magu.
Kupanda daladala ya gomz mida hiyo nashangaa kuna katoto kashule moyoni nikajiuliza shule mida hii nani atamfungulia.
Hilo ni moja ya gap watu wenye nia mbaya wanaweza kutumia.
#EeBabaMunguTulindieWatotoWetu

Noma sana
 
Back
Top Bottom