Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Kuna shida mahali kwenye mindsets za mtu mweusi!!!
Hao waliotuletea hii elimu wanasoma kwa ku relax sana na bado hadi leo hii ni wagunduzi hodari
Sisi tulio ipokea elimu , tunasoma kwa kujitesa sana na hatuvumbui chochote
Daah umeongea madini sana nilisoma tuu bila kuangalia Id yako ikabidi nishushe aisee watoto wanasoma kwa tabu sana kuanzia hizo gari wanazopanda na Serikali hata haifikirii kuwatolea kodi waagize bus nzuri watoto wetu wasione Elimu ni adhabu..
 
Siku ya kikao cha wazazi nikamuuliza MD akasema eti watoto wenyewe ndio wanapenda. Wazazi tuliikataa tukamtaka wafuate ratiba mtoto abebe kulingana na ratiba
 
Daah umeongea madini sana nilisoma tuu bila kuangalia Id yako ikabidi nishushe aisee watoto wanasoma kwa tabu sana kuanzia hizo gari wanazopanda na Serikali hata haifikirii kuwatolea kodi waagize bus nzuri watoto wetu wasione Elimu ni adhabu..
Inakera sana broo, mtoto anahangaika na elimu anakuja kupata degree, baadaye anahangaika na bahasha ya khaki kutafuta kazi kwa kina bakhresa.
 
Kuna shida mahali kwenye mindsets za mtu mweusi!

Hao waliotuletea hii elimu wanasoma kwa ku relax sana na bado hadi leo hii ni wagunduzi hodari.

Sisi tulio ipokea elimu , tunasoma kwa kujitesa sana na hatuvumbui chochote
Kwani huyo mtoto hiyo saa 10 ndo anaingia darasani?

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Mm natamani Ile sera mpya ya elimu ianze kutumika, yaani mashindano ya mitihani yaondolewe, kuwe na pass and fail tu, hii itaondoa mkimbizano wa kutafuta shule kuongoza Ili kuvutia watu
Kuna jamaa mmoja anadai kuwa hii itaZiua shule binafsi. Mana tayari imeanza kwa std4,f2 and f4. Yaani labda shule 200 zinapata ufaulu wa A,shule 600 zinawekwa group B and so on.


Kiukweli watu ambao hawajasoma na wakapata hela huwa wanawanyanyasa watt wao mno na wanatembea kifua mbele kuwa mie mwanangu nalipa 3M naseri anadhani kuwa more money more education quality. Na ulimbukeni fulani wa ego inawasumbua. Pia wakiwa wanasumbuka ama kusumbuliwa na wasomi so wanaumia mno wanaapa kuwa lazima wasomeshe watt wao kufa na kupona ili wwsinyanyasike Tena.unakumbuka ramadhani ntuzwe alivyosumbuliwa na watu wa TRA na sijui Kama wamemfilisi na hawajamlipa nadhani Mungu wangu.


Yaani Hawa jamaa wa private schools shule zimefungwa wanataka watt wabakie shuleni eti wasisome twisheni za mitaani wanaziita.
Madarasa yenye mitihani ndio usiseme kabisa wanalipa zaidi kuwa wanafundisha jioni. Yaani tabu tupu kwa wtt Hakuna kupumua ama hata kucheza. No extra curricular
 
Dar saa 11 asubuhi unapishana na school bus ina wanafunzi jiulize waliamka saa ngapi mpaka wamejiandaa. Tunawatesa sana watoto anafika shule amechoka.

Unakuta mtoto amazungushwa kwenye school bus zaidi ya masaa 2 au 3 hadi anaenda kuanza vipindi.
 
Jana wangu wa miaka mi 3 naambiwa gari lake la sa moja lime change route kwahiyo natakiwa nimuandae sa kumi na moja na nusu awe tayari...halafu kurudi sa kumi na mbili na nusu jioni........ Dereva nimemwambia haiwezekani,mwenye shule nimemwambia kama itashindikana aende shule nyingine.
 
Kuna dosari kubwa mno katika mtaala mzima wa elimu ya kibongo.

Mfano watoto wa darasa la saba kuambiwa waende shule mpaka jumapili. Siku za kawaida wanawatoa saa 2 usiku. Kuna kipi cha mno wanachosomeshwa sasa hivi ambacho sisi miaka ya 90 hatukukisoma??

Hapo hapo mtoto anabebeshwa rundo la mitabu kama vile anasomea masters ya udaktari.
Watoto shule mpaka j2 😆
 
Ni ujinga na ulimbukeni wa elimu na asilimia kubwa ya wazazi wanaofanya hivyo ni wale ambao hawajaenda shule ila Mungu kawabariki kipato aisee hili kundi linatesa watoto mtoto darasa la pili apumziki kama hivyo kamamka sasa tisa anaenda shule kurudi nyumbani sasa tatu usiku maana.. akitoka shule anaenda tution yaani elimu inakuwa kama utumwa.
Wazaz ambao hawakusoma afu wakatoboa ndio wanatesa watoto....

Ila sie ambao tulipiga kayumba darasa la kwanza had form 6 game tulijua hatuna presha..
 
Watu wa Dar mnalalamika mno. Watoto wenyewe hao wanabeba begi kutoka mlango wa nyumba mpaka getini anakutana na school bus akifika shule analibebea mpaka darasani kwake. Mnawalea watoto ki mayai mno
 
Mbona kawaida sanaaa
Mfano watokao Tegeta/Mbagala/Mbezi ya Kimara kwenda Shule ya Diamond - Pale Upanga DSM
Apa umegusa kwenyewe .watotot wa shule hii wanatoka mbali mno. Lakin ada ni affordable na inatumia lugha ya kingereza. Wazaz wanaona kuliko kuwapeleka kayumba bora wabak huko
 
Mtoto anasoma Posta anakaa Chanika kisa English medium ya serikali,Kuna SIKU Niko kwenue gari saa nne usiku katoto ka std tuko nako kamesimama kanasinzia
 
Kuna shida mahali kwenye mindsets za mtu mweusi!

Hao waliotuletea hii elimu wanasoma kwa ku relax sana na bado hadi leo hii ni wagunduzi hodari.

Sisi tulio ipokea elimu , tunasoma kwa kujitesa sana na hatuvumbui chochote
Kwa kweli yaan, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Inakera sana broo, mtoto anahangaika na elimu anakuja kupata degree, baadaye anahangaika na bahasha ya khaki kutafuta kazi kwa kina bakhresa.
Bado swala la mikopo utasikia hawa wamepata hawa bado wanaojadili hayo walisoma bure kabisa sema mimi niliwahi kufikiri kuwa huu ni mpango maalumu wa kuzorotesha Elimu na watu wengi waishi maisha magumu ili watawaliwe kirahisi haiwezekani Mtanzania kwa rasilimali tulizonazo tunahangaika kutafuta fursa Nje ya Nchi huku wageni wakila hiyo keki na Watawala...
 
Mimi wa kwangu ndo natoka kuwapeleka saa hivi.

Vipindi wanaanza saa mbili.

Gari ya shule inapita saa 12, mda huo wanakuwa wamelala maana wanaamka saa 12 na robo.

Safi kabisa.

Kusoma si adhabu.
Boraaa wee aunt uko sahihi.
 
Back
Top Bottom