Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Hata mtoto wa chekechea naye eti wanampeleka tuition.

Tatizo ni kutaka sifa ambazo hazina msingi...

Wakifika chuo ni msiba
Kweli halafu ujue Kuna katoto la std 1 kanasoma tuition [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kuna jamaa mmoja anadai kuwa hii itaZiua shule binafsi. Mana tayari imeanza kwa std4,f2 and f4. Yaani labda shule 200 zinapata ufaulu wa A,shule 600 zinawekwa group B and so on.


Kiukweli watu ambao hawajasoma na wakapata hela huwa wanawanyanyasa watt wao mno na wanatembea kifua mbele kuwa mie mwanangu nalipa 3M naseri anadhani kuwa more money more education quality. Na ulimbukeni fulani wa ego inawasumbua. Pia wakiwa wanasumbuka ama kusumbuliwa na wasomi so wanaumia mno wanaapa kuwa lazima wasomeshe watt wao kufa na kupona ili wwsinyanyasike Tena.unakumbuka ramadhani ntuzwe alivyosumbuliwa na watu wa TRA na sijui Kama wamemfilisi na hawajamlipa nadhani Mungu wangu.


Yaani Hawa jamaa wa private schools shule zimefungwa wanataka watt wabakie shuleni eti wasisome twisheni za mitaani wanaziita.
Madarasa yenye mitihani ndio usiseme kabisa wanalipa zaidi kuwa wanafundisha jioni. Yaani tabu tupu kwa wtt Hakuna kupumua ama hata kucheza. No extra curricular
Mi nikishaona hizo dalili mbona mtoto atarudi Serikali amalizie la 7
Hakuna atachopoteza kwa mwaka 1
 
Jana wangu wa miaka mi 3 naambiwa gari lake la sa moja lime change route kwahiyo natakiwa nimuandae sa kumi na moja na nusu awe tayari...halafu kurudi sa kumi na mbili na nusu jioni........ Dereva nimemwambia haiwezekani,mwenye shule nimemwambia kama itashindikana aende shule nyingine.
Kwanini usitafute mtu wa kumpeleka?
Mbona Wahindi hununua gari kwa ajili ya kupeleka mtoto shule?
 
Hata za cambridge ukikagua hutakuta vitabu vya hivyo. Vitabu vya shule huwa na mihuri, kama ni vitabu vya ziada lazima wazazi walihusika katika ununuzi maana yake tungeona tu
Afadhari wewe umehoji.Shule anayosoma mtoto wangu,unakwenda Shule unalipia Vitabu vya mtoto wako na unapewa vyote unavikagua na kuandika Jina la mtoto wako.Sijawahi kuona kitabu cha namna hiyo.
 
Ratiba yatakiwa izingatiwe.

Hapo ni mzazi kuandika kwenye diary kuwa ratiba ifuatwe, muwekee mtoto madaftari husika tu. Akichapwa nenda kapambane nao huko shuleni, wakimfukuza wakurudishie ADA
Na baadhi ya Shule daftari na vitabu vyote vinabaki Shuleni anawekewa kwenye locker yake,mtoto anakuja nyumbani na daftari la H/ work tu na kitabu atakachotumia kujibu H/ work.Hakuna cha kubebeshwa Begi kubwa la madaftari.
 
Mtoto anasoma Posta anakaa Chanika kisa English medium ya serikali,Kuna SIKU Niko kwenue gari saa nne usiku katoto ka std tuko nako kamesimama kanasinzia
Manispaa zatakiwa anzisha English Medium sehemu mbali mbali ili kuzuia watoto kujazana Maktaba, Olympio na Diamond
 
Mzazi ndo mwenye kosa.
Ukiaona dalili za ajabu mhamishe mtoto mpeleke shule ya kawaida ila mkazanie kusoma.

Kwa ujeuri wangu siwezi mpeleka.

Mtoto atasoma siku 5 pekee
ni rahisi kwako kuongea ikiwa huna mtoto ama hujakutwa na kadhia kama hiyo.

Mtoto keshasoma shule hiyo hiyo miaka saba, unakutana na usumbufu huo ikiwa keshaingia darasa la saba. Unaanzaje kumuhamisha mtoto wa darasa la saba? Process na usumbufu wake unaujua?

Si kila anaetaabika anapenda tabu hiyo, kuna kipindi mambo mengine yapo nje ya uwezo wa mtu.
 
Wazungu hawana huu ujinga, madaftari na vitabu vingi hubaki shuleni kwenye lockers,
Sisi mzazi anaona sifa mtoto kubebeshwa begi kubwa.

Baadhi ya Shule hapa Dar pia wanafanya hivyo hivyo.Daftari zote Mzazi utapewa wakati unakwenda kuchukua report ya mtoto pale ndiyo utapitia Daftari zote kwa pamoja kuona.Lakini siku zote mtoto anarudi nyumbani na Daftari moja tu na kitabu kwa ajili ya H/work.Mzazi huna hata haja ya kununua Bag kubwa la Shule sababu halina kazi.
 
Watoto wanaopanda School Bus kwa kufuatwa mpaka getini nyumbani na kurudishwa,hayo mabegi wanatembea nayo muda gani? Au hapa unaongelea watoto wanaosoma Shule za Serikali wasiokuwa na usafiri?
Umekariri sio shule zote binafsi watoto hupanda school buses.
 
Dunia ya sasa ni very competetive ,acha wajifunze mapema waje ku-enjoy baadae..Sema wazazi likizo muwaacheni watoto wenu wale maisha msiwapige matuisheni tena
 
Afadhari wewe umehoji.Shule anayosoma mtoto wangu,unakwenda Shule unalipia Vitabu vya mtoto wako na unapewa vyote unavikagua na kuandika Jina la mtoto wako.Sijawahi kuona kitabu cha namna hiyo.
Ni kuleta taharuki tu na hizo shule haziwezi jiharibia maana watafungiwa.

Ukiomba uthibitisho hutaupata
 
Back
Top Bottom