Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

ni rahisi kwako kuongea ikiwa huna mtoto ama hujakutwa na kadhia kama hiyo.

Mtoto keshasoma shule hiyo hiyo miaka saba, unakutana na usumbufu huo ikiwa keshaingia darasa la saba. Unaanzaje kumuhamisha mtoto wa darasa la saba? Process na usumbufu wake unaujua?

Si kila anaetaabika anapenda tabu hiyo, kuna kipindi mambo mengine yapo nje ya uwezo wa mtu.
Mtoto anahama vizuri likizo ya mwisho
 
Baadhi ya Shule hapa Dar pia wanafanya hivyo hivyo.Daftari zote Mzazi utapewa wakati unakwenda kuchukua report ya mtoto pale ndiyo utapitia Daftari zote kwa pamoja kuona.Lakini siku zote mtoto anarudi nyumbani na Daftari moja tu na kitabu kwa ajili ya H/work.Mzazi huna hata haja ya kununua Bag kubwa la Shule sababu halina kazi.
Hizo shule ni bora, ungeziorodhesha ili watu waone wafikirie
 
Mi mwenyewe kama shule iko karibu mtoto atatembea tu.
Labda iwe kuanzia KM 5, tofauti na hapo anatrot tu
Chini ya 5KM kwa mtoto siyo tatizo kutembea.Tatizo wazazi wengi hatupendi 'kuwatesa' watoto wetu.
 
Sijui wanamuwahisha afanye nini. Mtoto anatakiwa aanze shule na miaka 5, la 1 aanze na miaka 7
nyumban akae akifanya nn
Kujifunza ujinga wa mtaan ??bora aende shule
Miaka 7 std 1 ??katakuwa kazee kadarasa
 
Hizi shule siku hizi watoto wetu wanateseka Sana.
Ni mateso ambayo yanawafanya hata ukuaji wa kiakili uwe mbovu.
Tunatengeneza kizazi hatari sana kwenye jamii.
Hapa kwangu huwa naamshwa na honi ya gari inayokuja kufuata wanafunzi.
Saa 11 kamili asubuhi.
Anazungushwa mji mzima mpaka saa 2 ndio masomo yañaanza.
Upumbafu tu
 
Hata wale wanaowasindikiza watoto stend asubuhi wana kazi sana, unakuta wamekaa mpaka wanasinzia huku kampakata mtoto kashalala kitambo, mwisho wa siku mtoto anapata A ila anashindwa kusolve simple real world problem.
Mimi sioni faida za A kukariri. Rudia huohuo mtihani baada ya miezi 2 uona watakavyofeli. Watanzania tunashindwa kutofautisha kusomea mitihani na kusoma ili kupata maarifa.
 
Rwanda wanabadili muda wa watoto kwenda shule ili wapata angalau muda wa kunywa japo chai na wazazi wao hiyo taabu inamkuta mwanangu anatoka nyumbani 11:30 kigambon mpaka mikocheni aliko pangiwa shule jana kafika shule saa 1:30 mwalimu mkuu kamchapa mpaka kamtegua mkono na anajua changamoto aliyo kua nayo mtoto aliambiwa anakaa mbali
 
Back
Top Bottom