Saa ya Rais Samia yadaiwa kuwa na thamani ya Tsh. Milioni 111,601,22/=

Saa ya Rais Samia yadaiwa kuwa na thamani ya Tsh. Milioni 111,601,22/=

Tujue mshahara wake na marupurupu.

Pia tukubali kuwa kila mtu ana vipaumbele vyake. Wakati wewe unapambania ugali, yupo mwingine anapambania kumalizia appartments zake.

Tunatofautiana. Hatuwezi kumvika kipngozi magunia hata hali iwe ngumu vipi. Ni bora kutomchagua kuliko kugusa ubinadamu wake
Acha kupotosha maana halisi ya kinachozungumzwa..acha Rais, wewe unaweza kuvaa magunia hata km huna hela kununua nguo za kawaida..! hakuna anayemvika kiongozi hata km pesa inayotumika kununua ni ya anaowaongoza, yeye mwenyewe anajivika lakini tunamshangaa kutumia pesa tunayomchangia kufanya anasa! akiwa kwenye nafasi hiyo hatutarajii awaze anasa!
 
Rais ni zaidi ya wananchi wote na vyeo vyote katika nchi.Rais ni mtu mwingine na wa pekee katika nchi zetu.Mshahara wake na marupuru yake, hiyo saa ni kitu kidogo sana. Jitahidi urekebishe paa la kibanda chako ikibidi utoke mabondeni, masika inakuja.
Mjinga wewe, Rais ni kiongozi sio boss, anawaongoza watu masikini wa Tanzania, nchi masikini alafu anavaa saa ya milioni 100?? Kiongozi lazima aonyeshe unyenyekevu na aishi maisha ya wale anaowaongoza
 
Mimi ni kiongozi? Unapokuwa kiongozi lazima uonyeahe uchungu na nia ya dhati na maumivu ya wale unaowaongoza, unadhani Nyerere angeamua kuwa tajiri Angeshindwa? Lakini kwakuwa alikuwa kiongozi na sio boss ndiyo maana leo una uhuru ulionao sasa! Acha kutetea upumbavu
 
Ko asinunue saa kwa mshahara ambao ni halali yake, kisa uchungu kwenu masikini?
Wew hapo hauli nyama roast kisa umasikin wa wajomba zako kule kijijini ?
Mimi ni kiongozi? Unapokuwa kiongozi lazima uonyeahe uchungu na nia ya dhati na maumivu ya wale unaowaongoza, unadhani Nyerere angeamua kuwa tajiri Angeshindwa? Lakini kwakuwa alikuwa kiongozi na sio boss ndiyo maana leo una uhuru ulionao sasa! Acha kutetea upumbavu
 
Kuna uhakika gani kama ndio yenyewe jamani? Labda mama is faking till she makes it je?

Ila mimi sijui hizo saa watu huwa wanazipendea nini? Niache kuvaa apple smart nivae mshale dunia hii ya sasa? Na uwezo upo?
Kwa hiyo unadhani hakuna saa za Mshale nzuri wapo wenye hizo Apple na pia wana mshale ni uwezo tu..
 
Mtoa mada ni mtu mpumbavu sana na hana akili, siku zote tunam judge mtu na kile alichonacho kwa nguvu ya mshahara wake!, wangapi mitaani wanatembelea amarok, au volkwagen za milioni 150, kila kitu judge kwa kupimia na mshahara wa muhusika, sasa ujinga ni kila kitu alichonacho kiongozi unaki translate kwenye madawati, shule, inamaana ipo siku utafikia kusema kiatu chake kinatosha kujengea choo cha shule! 😁😁😁
Cdm sijui wanatumiaga akili gani.
Kati ya watu wapumbavu na wewe ni mmojawapo. Hao wanaomiliki hivyo vitu ni viongozi? Unaelewa maana ya kuwa kiongozi? Watu unaowaongoza hawana uhakika wa milo mitatu alafu wewe unavaa saa ya milioni 100? Una akili timamu? Baba wa familia masikini watoto hawana chakula wewe unaenda kununua gari? Unatumia makalio kufikiria au?
 
Asipo vaa yeye avae nani?.
Kwanza sio lazima awe amenunua yeye, anaweza kabisa kuwa ni amezawadiwa tuu!.

Pili hata ukinunua kuna ubaya gani?.

Kwangu tatizo sio bei bali rais wetu kuvaa saa yenye kichwa cha serpenti!, atakuwa hakujua yeye anaona tuu kaletewa expensive gift ya saa ya bvlgari serpenti watch kumbe ni amemvaa serpent bila kujijua!.

Siku moja natafuta miwani, nikapita duka fulani nikaipenda miwani fulani ya Cartier. Nilipotaka kuinunua nikaambiwa hiyo ni order ya JK, wameleta only 2 pieces custom made from factory!. Piece moja JK ndio ameichukua, hiyo piece iliyobakia ni sample ya dukani ili watu wafanye order, amini usiamini nilioder, na baada ya kunichukua vipimo, wakanipa hiyo piece, ili order yangu ikifika ndio itakaa sample!, hivyo nikavaa Cartier ya JK!. Naomba nisitaje bei humu nikaonekana na brags!. View attachment 2911766
View attachment 2911767 hiyo frame ni Cartier pure 22 carat gold, ina grams za kutosha, unauziwa na kupewa certified certificate of authenticity, kwa bank za wenzetu unaitumia kama dhamana!.

Anavaa watch ya Patek Philippe, anatumia peni ya Montblanc Meisterstuck, simu yake ni Iphone 6 Pink Diamond na anapiga suti za Saville!. Wazungu wanatudharau sana na kutuona sisi Watanzania ni masikini sana, walipomuona JK kapiga suti ya Saville wakajua kwa umasikini wetu rais wetu hawezi kununua!, wakasema lazima atakuwa ni amehongwa suti!. Ikaripotiwa JK kahongwa suti!, nilipandisha uzi huu humu JF
Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi! walituomba radhi!.

We deserve the best that money can buy!.
Tena watu wanapigia kelele ma VX, mimi nimeshauri viongozi wetu wakuu wakiwemo waheshimiwa wabunge wetu watumie armoured vehicles!. Afrika tuna shida sana, Kiongozi gari ya milion 600?
P
Kuna tofauti ya kuwa kiongozi na kuwa boss. Hususan kiongozi wa nchi masikini kama Tanzania! Kiongozi unatakiwa uyaishi maisha ya wale waliokuchagua! Hauwezi kuwa baba wa familia inayolala njaa alafu ukaenda kununua gari la thamani huku watoto wako wanateseka! Ni AIBU! vinginevyo haustahili au haukupaswa kupewa hiyo nafasi. Leader must be humble! Unadhani Nyerere angeamua kuwa boss na si kiongozi leo tungekuwa na uhuru? Pili unasema amezawadiwa, unazielewa sheria za utumishi wa umma? Haruhusiwi kupokea zawadi! Akipokea ni mali ya Tanzania si mali yake.
 
Kumbuka,
Ni Rais unaemzungumzia 🐒

hata hivyo hata PhD yake pia ulinung'unika, kualikwa kwake Rome na Pope, ulinung'unika, kusafiri kwake ng'ambo mara kwa mara manung'uniko, kuchangia mamilioni kwenye club zinazoshiriki mashindano ya kimataifa kuwatia hamasa manung'uniko, kusafiri na wasanii kwenda india manung'uniko, kuingilia katika kwake matibabu ya viongozi na wananchi manung'uniko, akisifiwa manung'uniko, na kwahiyo nung'uniko hili nalo litapita 🐒
Litapita lakini watanzania watabaki bila umeme, bila huduma bora za afya, bila elimu bora n.k
 
Acha kupotosha maana halisi ya kinachozungumzwa..acha Rais, wewe unaweza kuvaa magunia hata km huna hela kununua nguo za kawaida..! hakuna anayemvika kiongozi hata km pesa inayotumika kununua ni ya anaowaongoza, yeye mwenyewe anajivika lakini tunamshangaa kutumia pesa tunayomchangia kufanya anasa! akiwa kwenye nafasi hiyo hatutarajii awaze anasa!
Kachota Hazina si ndiyo?
Tupe usuli tubebe bango
 
Back
Top Bottom