Saa ya Rais Samia yadaiwa kuwa na thamani ya Tsh. Milioni 111,601,22/=

Saa ya Rais Samia yadaiwa kuwa na thamani ya Tsh. Milioni 111,601,22/=

Ni ujinga kiongozi wa nchi masikini tena anayelipwa mshahara kwa kodi za masikini kuvaa saa ya milioni 111 wakati wale unaowaongoza hawana uhakika wa milo motatu kwa siku! Kuna tofauti ya kiongozi na 'boss' Rais anapaswa kuwa kiongozi na sio boss.
Tujue mshahara wake na marupurupu.

Pia tukubali kuwa kila mtu ana vipaumbele vyake. Wakati wewe unapambania ugali, yupo mwingine anapambania kumalizia appartments zake.

Tunatofautiana. Hatuwezi kumvika kipngozi magunia hata hali iwe ngumu vipi. Ni bora kutomchagua kuliko kugusa ubinadamu wake
 
Binafsi hayo hayatuhusu nadhani, je anasimamia nchi vizuri? Umeme, maji, elimu, afya, bidhaa anasimamia vizuri? Kama hawezi bora akae pembeni tuweke wapambanaji nchi ipige hatua.
 
Una uhakika gari la waziri mkuu wa Tanzania ni la kifahari kuliko la waziri mkuu wa UK au Japan,?
Mara nyingi tu viongozi wa nchi wafadhili wa Tanzania wanatumia magari madogo sana na wengine wanatumia hata public transport ikiwa ni pamoja na aliyekuwa chancellor wa Ujerumani na wengine. Mnapenda kuona misafara ya magari 100 mnafikiri hizo gharama zinatoka wapi? Ni kodi yako na gharama hizo zinakula kwako in terms of maendeleo hafifu, umeme, sukari, miundombinu mibovu n.k. Muwe mnajielewa watanzania!
 
Analipwa shilingi ngapi kwa mwezi?
Umasikini ni zaidi ya uchawi!! Ndio maana kwenye umaskini mkubwa ndipo kwenye uchawi sana!! Sasa hiyo saa na kipato chake mbona ni ardhi na mbingu, hiyo si perdiem yake ya siku kadhaa tu
 
Lakini serikali hiyo hiyo ya Nyerere enzi hizo ilikuwa inaweza kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi maskini ikiwemo elimu, matibabu, maji nk.

Fikiria maelfu ya wanafunzi ndoto zao za kielimu zimekufa kwa kunyimwa ufadhili wa serikali, halafu eti nikanunue saa ya milioni mia.....hiiii bhagosha!​
Elimu ipi bora ilitoa? Kanda nzima kuwa na shule 1 ya sekondari ndio elimu bora?
Au kupora shule za Mission kisha kutojenga shule za serikali ?
Hio Afya gani aliitoa? Alijenga hospital ngapi? Hakuanzisha hata chuo kipya tu cha wauguzi/ Madaktar, kisha unasema alileta huduma gani?
Yan ushindwe kuwapa watu sukari uweze kuwapa elimu bora na Afya ? Unaona inawezekana ?
Huyo Nyerere wako miundombinu tu hakuifanyia kazi, watu wanatoka dar wanaenda kenya ndio waende Mwanza, yeye yupo tu,

Nambie Nyerere alifanikisha lipi ukiachana na masuala yake ya ukombozi ? Huduma gani kwa wananchi alifanikiwa kuwapa ?
 
Mshahara anaolipwa kwa kodi za watu masikini? Huyo sio kiongozi ni boss. Kiongozi lazima aonyeshe uchungu na aishi maisha ya wale anaowaongoza
Ko asinunue saa kwa mshahara ambao ni halali yake, kisa uchungu kwenu masikini?
Wew hapo hauli nyama roast kisa umasikin wa wajomba zako kule kijijini ?
 
Mshahara wake ni sh ngapi? kiasi kwamba ashindwe kununua hio saa
Ujinga, unapokuwa kiongozi unapaswa kuishi katika namna jamii ikuone kama kiongozi aio boss. Haiwezekani wale unaowaongoza hawana uhakika wa milo mitatu alafu wewe unavaa saa ya milioni mia
 
Back
Top Bottom