Sababu 3 muhimu kwanini mwanaume mwenye hela humvutia mwanamke kirahisi

Sababu 3 muhimu kwanini mwanaume mwenye hela humvutia mwanamke kirahisi

Nilivyokuwa binti nilikuwa nikitongozwa na mwanaume mwenye pesa natoka mbio, yaani hata kumsikiliza nilikuwa staki...
Now natamani nitongozwe na mwenye pesa ndo hawanitongozi kama sio gundu hili ni nini
😂😂Ila demi
 
😂😂 sio gundu hiyo inaitwa karma. Kwahiyo unatongozwa na akina sie
 
Nilivyokuwa binti nilikuwa nikitongozwa na mwanaume mwenye pesa natoka mbio, yaani hata kumsikiliza nilikuwa staki...
Now natamani nitongozwe na mwenye pesa ndo hawanitongozi kama sio gundu hili ni nini
Mwanaume tukiwa na pesa hupenda mwanamke mzur wa sura na umbo
 
Men searching for leadership and authority while women looking for security and support lets stand as it is

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
Kuvutiwa na mtu inatokea naturally tu, ukishaweka kigezo cha material yoyote hapo kwa kiasi kikubwa kinachoangaliwa ni masilahi sio mvuto tena yaani hicho kigezo cha pesa kikiondolewa maana yake mwanamke hana tena sababu ya kuvutiwa na uyo jamaa huo sio mvuto tena ni masilahi yanaangaliwa hapo. Ungesema sababu ambazo zinawafanya wanawake wavutiwe na pesa ungeeleweka zaidi maana hapo kinachoangaliwa ni pesa sio mwanaume kama mwanaume. Mkandamizaji pesa anayo ila alichapiwa na katibu wake
Kweli mvuto ni asilia, mwanamke anapenda kufanyiwa vitu.
Je, masilahi/ material yoyote sio muhimu katika mapenzi?
Unaposema kinachoangaliwa ni pesa, je mwanamke akiwa na pesa atahitaji mwanaume?
 
Kweli mvuto ni asilia, mwanamke anapenda kufanyiwa vitu.
Je, masilahi/ material yoyote sio muhimu katika mapenzi?
Pesa ni muhimu. Hata kama mapenzi sio pesa ila jitahidi iyo pesa isikosekane kabisa. Mwanamke kuvutiwa au kumpenda mwanaume mwenye pesa sio kosa ila kama pesa ikiwa ndio determining factor pekee hapo hakuna mvuto tena
Unaposema kinachoangaliwa ni pesa, je mwanamke akiwa na pesa atahitaji mwanaume?
Kiuhalisia mwanamke na mwanaume kila mmoja anamhitaji mwenzake. Kiuhalisia mwanamke anakuzwa kwa mtazamo kwamba akishavunja ungo ataolewa na kuhudumiwa na mwanaume na yeye mwanamke atapaswa kuwa mtiifu na mnyenyekevu kwa mwanaume wake kama malipo ya matunzo anayoyapata sasa mwanamke akifanikiwa anakua anaona hakuna nafasi ya mwanaume kwenye maisha yake(mafanikio yake yanamdanganya). Kwann ajishushe mbele ya mwanaume wakati na yeye mwenyewe anaweza kujitunza. Fatilia kesi za talaka utakuta zaidi ya 90% ni ndoa za wanawake wasomi au wenye pesa
 
Mwanamke yeyote anahitaji usalama kutoka kwa mwanaume wake, ndicho kitu cha kwanza wanakiangalia kabla ya kuwa kwenye mahusiano, japo huwa halisemwi waziwazi.

Usalama wanaotaka ni usalama wa kiakili, kiroho na kimwili ilii aweze kujiachia kwa mwanaume. Usalama wa kimwili mwanamke huupata pale anapojua mahitaji yake ya kimwili yanaweza kutimizwa, na mahitaji ya mtoto wake yataweza kutimizwa.

Hela inatimiza mahitaji makuu ma 3 ya kimwili. Mwanamke anakua na uhakika anaweza kuvaa, kula na kulala sehemu nzuri na salama, ukiwa na pesa hivyo vitu vinakua rahisi kwako kutimiza. Sehemu pakiwa na uhakika wa kula basi mtu hujisikia salama kuishi, haijalishi ni mwanamke au mwanaume.

Pia hela inaepusha migogoro midogo midogo, Mfano, unakuta mwanaume anamlalamikia mwanamke anamaliza sabuni ya kuogea, huyo mwanamke atajisikia usalama kuishi na mwanaume anayemuacha ajisafishe kwa amani bila kulalamikiwa kuhusu sabuni.

Hela inawezesha kusafiri na kufurahia sehemu tofauti. Ukiwa na pesa ni rahisi kumtoa mwanamke wako kwenda kutembea (ni jambo muhimu).

Wanawake wanapenda kuweka kumbukumbu tofauti tofauti pamoja na watu wawapendao. Usije ukakaa na mwanamke sehemu moja tu siku zote 365, utachokwa. Panga siku za kutoka. Haijalishi una hela kiasi gani, ila hakikisha mnabadili mazingira angalau mara moja kwa wiki.

Hela inasaidia kupata huduma za kiafya kirahisi. Atajiona yupo salama kwako unapokua na hela ya kumhudumia anapoumwa. Wanawake ni rahisi kukubali kuwa ni wagonjwa (sisi wanaume tunaona kuumwa ni udhaifu) ndo mana mara kwa mara atakuambia anaumwa, sio jambo baya sababu inabidi wawe na afya nzuri ili waweze kuleta uhai mpya wenye afya hapa duniani.

Mahitaji mengine kama vocha, vipodozi na manukato unaweza msaidia kadri uonavyo sawa, hakikisha mwanamke unayetaka kujenga naye maisha anayaweza hayo mahitaji madogo, pia unaweza mfundisha jinsi ya kupangilia matumizi ili asikuelemee kwenye hivyo vitu vidogo.

Ila usije ukadhani ni hela pekee ndio itakuwezesha kumtunza mwanamke wako. Wapo wanaowatimizia wanawake mahitaji ya kifedha na wamewashindwa wanawake, sababu wameshindwa kutimiza mahitaji mengine.

Bali uwezo wako wa kumridhisha kimwili, kiakili na kiroho, na kuwa kiongozi wake mzuri unakuwezesha kumtunza mwanamke unayetaka kujenga naye maisha, ndio maana katika kundi la infinite kiumeni utajifunza kila siku jinsi ya kumvutia na kumtunza mwanamke unayetaka kujenga naye maisha.
Money is power
 
mwanamke akifanikiwa anakua anaona hakuna nafasi ya mwanaume kwenye maisha yake(mafanikio yake yanamdanganya)
Umesema vizuri. Lakini,
Kwa nje inaonekana hivyo, lakini kiukweli ni kwamba wanaume wanaogopa wanawake wenye mafanikio, au wanakua na chuki nao bila sababu kwa kulinda imani kuwa mwanamke hawezi kumzidi kipato.
.
Wengi hawataki/ wanaogopa changamoto ya kuwa viongozi wa wanawake waliowazidi kipato na kuishia kulalamika wanawake wenye pesa wanajiona. Kwa mwanaume kuwa kiongozi wa mahusiano hakuji tu, lazima ufanyie kazi na ujifunze. Watu wanadhani mtu unakuwa kiongozi tu bila kuhangaikia lakini ki ukweli uongozi una mitihani mingi na kadri unavyozidi kupanda ndivyo mitihani inakua migumu na kuongezeka. Wanawake wenye pesa ni changamoto tu ya wewe kama mwanaume kujifunza na kuishi naye.
.
Mwanaume anayejifunza hana muda wa kulalamika, na mwanaume anayelalamika hana muda wa kujifunza.
 
Nakuombea mkeo/mpenzi wako awe tajiri ili ujionee uhalisia. Haya mambo ni rahisi sana kuwaona wenzako mabwege kama wewe hayajakukuta
 
Back
Top Bottom