"Na sema: Sifa zote njema za ukamilifu ni za Allah ambaye hakujifanyia mwana, wala hana mshirika katika ufalme, wala hana kipenzi wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu wake, na mtukuze kumtukuza kulikokuwa kukubwa".
Qu'ran 17:111
"Na walisema: Allah amejifanyia mtoto, ninamtakasa kumtakasa! {na hilo}, bali ni vyake yeye vilivyomo mbinguni na ardhini, vyote vinamnyenyekea yeye."
Qu'ran 2:116
"Na wao husema kuwa mwingi wa rahma ana mtoto, kwa hakika mmeleta jambo kubwa mno! zinakaribia mbingu kupukutika kwa hilo, na kupasuka pasuka ardhi, na milima kuanguka vipande vipande, kwa wao kudai kuwa mwingi wa rahma ana mtoto, wala halingani mwingi wa rahma kuwa na mtoto, hapana yeyote aliyemo mbinguni na ardhini isipokuwa atafika kwa mwingi wa rahma hali ya kuwa ni mja wake, hakika yeye amewadhibiti na amewahesabu kuwahesabu, na kila mmoja katika wao atamjia yeye siku ya qiyamah hali ya kuwa yu peke yake."
Qu'ran 19:88-95