Sababu za kiroho kwanini lazima ufunge Ramadhani hata kama sio muislamu

Kwahiyo mkuu shetani ni muislam?
 
KAMA KUBADILISHA RATIBA YA KULA NDIO KUFUNGA.

BASI MIMI NAWEZA NIKAFUNGA MIAKA 10.

NAKULA USIKU KAMA WAISILAMU ALAFU NAJIDANGANYA NIMEFUNGA.

HII DINI YA HOVYO SANA

Usiku na asubuhi Chief

Saa 2 usiku na Saa 10 asubuhi ya siku nyingine

Sasa Mtu ule daku Msosi wa nguvu saa 10 asubuhi utashindwa nini kuvumilia mpaka jioni saa 12?

Hakuna kufunga hapo
 
Hakuna mtu mwenye uwezo wa kula kucha mpaka alfajiri. Atashindwa tu maana tumbo la kiasi chake cha kuuweka chakula na maji. Mnajua fika mnapoongea hivi mnaongea kwa dhihaka tu.

Usiku ni wakati wa kulala so nani atakesha usiku kucha anakula tu. (na ukiona kuna wanaofanya hayo basi hao Sio waumini wa kweli ni wafuata mkumbo tu) hawajajua maana ya Ramadhan

Ukifunga kwa ladha ya imaani basi hata chakula unakiona kawaida tu kama siku nyenginezo.

Halafu kusema unaweza kuishi kwa kufunga mchana bila kula wala kunywa mchana kwa lifetime yako Sio rahisi. Usiku Sio mchana. Mchana unaambatana na kutafuta rizk. Kuna watu wanaofanya kazi za sulubu Sio maskhara wakifunga wanafunga kwa imaani hasa. Kuna baadhi ya nchi baadhi ya miongo mchana wao (day) ni zaidi ya masaa 18 au 20 yaani wanapata masaa manne tu ya kula na kufanya ibada zao za usiku.

Sio rahisi bazee. Ni imaani
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ila Kiranga[emoji119]
 
Zamani tulipokuwa wadogo wakati ndio tunaanza kujifunza kufunga. Wakati wa mchana kila unachokiona unakitamani, lkn kwa vile umefunga unasema wacha niweke nitakila maghrib wakati wa kuftari.
Nazi ikipasuliwa unapeleka kikombe uwekewe maji ya nazi mpk maghrib utakunywa, ndizi mbivu ikikatwa ikitolewa moyo unasema uwekewe utakuja kula maghrib. Ukiona wtt waliokuwa hawajafunga labda wanagaiwa biscuits na wewe unachkua ya kwako unaweka kuja kula maghrib. Lkn wallah ikifika maghrib kuisha kunywa gilasi lako moja la maji na chakula kdg tu basi tayari unajiskia kuvimbiwa. Hata vile ulivoviweka vyote unakuwa Huna habari navyo tena.

Haifai kwa muumin kufakamia mavyakula ukavimbiwa mpk hata pumzi ya kufanya ibada inakuwa haipo.

Kufunga katika dini ni pamoja na kuongeza imaani yako muumin. Kupata feelings za how it feels kukaa bila ya kula for hours, kwani kuna baadhi ya watu ni maskini hawana chakula cha kutosha cha kila siku. (kujishusha hata kama chakula unacho unakaa na njaa kwa ajili ya Allah)
 
KAMA KUBADILISHA RATIBA YA KULA NDIO KUFUNGA.

BASI MIMI NAWEZA NIKAFUNGA MIAKA 10.

NAKULA USIKU KAMA WAISILAMU ALAFU NAJIDANGANYA NIMEFUNGA.

HII DINI YA HOVYO SANA
Kama huna imaani ya juu lichoamrishwa Sio rahisi.
Hebu practice kukaa bila ya kula na kunywa kwa mchana mitatu. Wakati wa mihangaiko yako ya kutwa. Utembee tembee juani kdg. Ujiskie kiu ila huwezi kunywa maji. Ukutane na moshi wa mishkaki na harufu za nyama choma na soda zinatoka jasho kwa baridi ila inakubidi kujizuia kula hata kama pesa unayo mfukoni. Kama unafanya kazi huduma kwa wateja kutwa asubuhi mpk jioni unaongea bila hata kunywa maji na uwezo unao ila inabidi kujizuia.

Mungu Ana hikma alivotuamrisha kufunga masaa ya mchana. Ndio masaa hasa yenye uhitaji wa kula na kunywa kuliko usiku

Hivi kweli utafunga usiku wakati ambao umepoa hamna joto kali, hamna mihangaiko kama ilivo mchana ya kutafuta rizk and on top of that ndio time ya kulala. Nafkiri hata watt wa miaka mitatu wangeweza kufunga. Lkn laa. Tunatakiwa kufunga mchana ili tuwe tested juu ya imani zetu kwa namna tulivyoamrishwa jee tutaweza.

Unajua kuna baadhi ya nchi wanafunga mpk masaa 18 ndio jua linazama! Yaani baada ya hapo una masaa manne tu kabla kuanza tena kufunga. Halafu kirahisi tu bila imaani useme Unaweza. Jaribu
 
Hapa ndipo mnapofeli, huwezi kutafsiri Quran kwa kuchukua mstari mmoja mmoja kama hivo.

Hakuna some gumu kama tafsiri ya Quran, inabidi kwanza uwe mtaalamu wa lugha ya kiarabu, yaani ujue syntax na semantics ya lugha ya kiarabu.

Halafu kila aya ya Quran lazima ujue imeshuka kwa sababu gani. Halafu lazima ujue aya nyuma na ya mbele yake. Huwezi kutafsiri sisisi kama hivo ndugu.

Nikupe mfano mdogo tu, Waislamu waliteswa sana walivokua Makka ikabidi waamrishwe wahame, kwanza Mtume Muhammad aliwaambia waende Ethiopia, kipindi hicho iko chini ya Mfalme mkristo akiitwa Najjash. Muhammad aliwaambia waende huko kwa sababu huyo mfalme alikua muadilifu na kweli walivofika walipewa ulinzi. Hii itoshe kukujuulisha kua Uislamu hauna shida na ukristo.

Mfano wa pili ni kuwa baada ya kupigana vita mara mbili na makafiri wa Makka , Muhammad aliingia nao mkataba wa Amani, kuwa miaka 10 pasiwe na vita. Lakini hawa makafiri wa Makka wakavunja mkataba wakawaua Waislamu. Muhammad akakusanya jeshi la watu elfu 10 akaivamia Makka. Kilichowastaajabisha Makafiri wa Makka ni kua wakati Makka inatekwa hakuuliwa hata mtu mmoja na Makafiri wote walipewa msamaha mbali ya madhila yote walowafanyia Waislamu. Na wote wakasilimu kwa hiari yao.

Sasa unaposema Uislamu ni dini ya vita sijui unatumia vigezo gani.

Halafu jambo la msingi ambalo nyinyi hamlijui ni kua shida ya uislamu sio ukristo bali ni Umagharibi.
 
Kubadilisha muda wa kula ndio mfungo?kweli MUNGU mnamchukulia kama mjomba enu,kuna sehemu katika biblia panasema " nazichukia sikukuu zenu za mwandamo wa mwezi" lakini wanajifanya hawapaoni!
 
Eti makafiri hii ni shida ya utumwa wa kitamaduni mwenyewe hilo neno unaona ziito ukilisema kwa kiarabu,baada ya miaka 600 ndio ukaja uislam sasa hapo nani kafiri/mpingaji?
 
Labda nikuwekee kwanza za majini mnayofuga
Kafiri hauna hoja. Kazi kuropoka. Sema ufahamishwe kama vitu hauvielewi. Mi sijaja kuleta ubishi we mfuasi wa Brian Deacon.
Nenda ukaombewe mashetani ya kutoke kwanza. Hii dini itaendelea kusimama hata makafiri mkichukia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…