Sababu za kiroho kwanini lazima ufunge Ramadhani hata kama sio muislamu

vizuri umekubali tujadiliane kwenye msingi wa logic (mantiki).

Maana nje ya mantiki, hakuna kujadiliana, ni kelele tu.

Kwa sababu misingi ya kujadiliana inatumia mantiki.
Naanzia hapa. Msingi mama wa logic ni akili,yaani huwa mnasema wenyewe ya kuwa elimu ya Mantiki ni elimu kwayo humuepusha mtu kukosea katika kujenga hoja. Hii ndiyo maana ya Mantiki yaani kwa ufupi haishughuliki na dhati ya ukweli. Msingi huu mama unao zalishwa na mawazo na kulinganisha mambo kisha kuhitimisha,kutokana na akili ambayo haijakamilika.Mantiki ambayo husema "Wanyama wana miguu minee,mbwa ana miguu minne,basi mbwa ni mnyama". Hapa huwa mmemalza wenyewe. Sasa nitakuuliza kipi hutangulia ? Sifa au kitu husika ?

Si kweli kwamba nje ya mantiki ni kelele,bila shaka utakuwa huijui Mantiki. Ndani ya mantiki kumejaa ubishi na ushabiki mtu anashikilia nadharia za kina Aristoto na kuishi nazo,yaani yeye alikosea na nyinyi mnakosea.

Siyo kweli kwamba misingi ya kujadiliana inategemea mantiki,hii ni kwa mujibu wenu,sababu mijadala ilikuwepo hata kabla ya waasisi wa logic walikuwa hawatajiki. Elimu ambayo haina hata uwezo wa kuniambia ya kuwa nikifa naenda wapi huu ni wasi wasi wa Shetani.
Ukisema Mungu ni mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye upendo wote, kwa kufuata mantiki, hana tabia wala hana sababu ya kuumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya kufanyika.
Hapa unadhihirisha udhaifu wa elimu ya mantiki.

Swali msingi gani wa mantiki umekupa hitimisho hili ? Lakini swali la msingi umejuaje hilo wakati halina kinyume chake ? Haya ni matumizi mabaya ya akili,kuna muda huwa najiuliza hivi huwa unaelewa unachokiandika au huwa unakitafakari kabla ya kukiandika ?

Naendelea....
 
Ulimwengu huu unaruhusu mabaya kufanyika.
Siyo ulimwengu,bali Mola mwenyewe ndiyo anaruhusu haya yatokee,sababu yeye ni mjuzi wa yote mkamilifu.
Hivyo, kimantiki, ulimwengu huu haujaumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.
Hili tunaliita wazo,wazo au dai,dai ambalo linahitaji uthibitisho. Sasa swali umepitia mchakato gani mpaka kupata wazo hili na kulihitimisha hivi ?

Sasa thibitisha hili na utuambie imekuwaje hali ipo hivi ilivyo ?

Sasa hili najua huwezi kulithibitisha ila naonyesha watu kwamba haya ni mawazo tu mnayatoa na hamna ushahidi. Maana yake sababu akili ndiyo msingi mkuu wa Mantiki,huwezi kwenda mbele zaidi ya wazo.

Mantiki niliidharau sana...

Na zaidi, Mungu huyo hayupo.
Swali liko pale pale umejuaje kwamba Mola hayupo ?
Kwa sababu, Mungu huyo kuwepo na kuruhusu ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kuwepo ni contradiction.
Ajabu huwa naiona hapa,hujajua kwamba Mola hayupo na huwezi kuthibitisha halafu hapo hapo unampangia afanye kwa mujibu wa mawazo yako. Hiki kituko kingine.

Nionyeshe Contradiction ilipo,wakati kila jambo liko wazi na linathibitishwa.

Hayo mabaya ameyaruhusu yeye yawepo ndiyo maana akawa muweza wa yote yaani yote anayaweza. Laiti kama ungekuwa unafikiri kwa umakini hii kauli ingekutosha.

Naendelea ..
 
Wewe sema tu huna jibu, hayo mengine ni blah blah tu za kukwepa swali.

Sent from my TECNO BC1 using JamiiForums mobile app
Hata nikiwa sina jibu, hilo nalo linaonesha Mungu hayupo.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo angewapa watu majibu yote na maswali ambayo hawana majibu yake wasingeyajua.

Hujathibitisha Mungu yupo, thibitisha Mungu yupo.
 
Longo longo nyingi + porojo


Mwisho wa yote unakimbia ukipata kiboko yako[emoji16]
 
Hizi ndo hadithi kama zile za juma na uledi..


Yaani utume askari 10000 kuvamia seemu yenye majeshi, alafu wasiue mtu hata mmoja..

Hao labda hawakua na jeshi kabisa, walivamia raia tuu
Tatizo hamtaki kusoma halafu mnabisha kila kitu, ndo maana mnatawalika kirahisi na mnadanyika kirahisi. Dunia ya leo si ya kubisha , nenda tu kagoogle The Conquest of Mecca
 
Ni sawa na kusema mama yake mzazi babu mwenye miaka sabini ni binti mdogo mwenye miaka mitano.
Naendelea...

Huu mfano hauingii hapa sababu hili liko wazi,na kama logic yenu inatoa mifano mfu namna hii,lazima uone Mola hayupo. Kuweka wazi jambo ambalo liko wazi ni matumizi mabaya ya akili.

Onyesha huo mfano unakaa wapi katika kadhia hii.
Hapa ni kama mimi nimekuambia hakuna binti wa miaka mitano ambaye ana mtoto wa kumzaa wa miaka sabini, kwa sababu hiyo nincontradiction ya kimantiki.
Sada hili nataka ulionyeshe kwa Mola wetu. Usilinganishe vitu visivyo fanana.

Sasa jikite katika mada,tumia mantiki yako kuthibitisha ya kuwa Mola hayupo. Ukiweza naacha kujadili hii mada.
Halafu wewe unaniuliza, wewe ymejuaje huyo binti hayupo? Kama hayupo umejuaje kuwa hayupo?
Hili liko wazi ni tofauti na hili ninalo kutaka uthibitishe.

Hii ni selft evident truth,yaani ukiona kitu fulani kinakupa jibu la uwepo wa vingine.
Naona unazunguka tu kwa kutoa mfano usiojibu swali langu.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote naye ni wazo la kufikirika tu, kiuhalisia hayupo.
Safi kabisa sasa thibitisha,yaani usitumie Strawman Argument kijana,jibu hoja kulingana na swali husika. Unachofanya wewe ni kama "Umekutana na bondia (mimi) hatari badala uingie kwenye ring upigane umekaa nje unaonyesha mikwara" . Nacheka sana.


Bado nakudai kijana.
Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.
Huku rahisi sana. Nataka ukiri ya kuwa umeshindwa kuthibitisha ya kuwa Mola hayupo,haya yanabaki kuwa ni madai,mpaka pale utakapo tupa ushahidi.

Uthibitisho wa uwepo wa Mola unathibitishwa kwa njia nyingi sana. Hizi ni miongoni mwazo.

1. Self evident truth
2. Contingent facts
3. Akili
4. Mazingira
5. Ufunuo

Hizi ni baadhi ya dondoo. Sasa nadubiri ukiri kwamba umeshindwa kuthibitisha ya kuwa Mola hayupo kisha nije kumaliza kazi yangu.

Nipo ....
 
Hadithi nyingine zinachekesha. Nani ashinde njaa kana kwamba vyakula vimekwisha? Ukifa utafunga taka usitake.
 
Mwenyezi Mungu hawezi kamwe kutenda na kufikiri Kama unavyofikiri wewe. Akili zake si kama za binadamu.
Bado hujathibitisha kuwa MM hayupo!
 
Mwenyezi Mungu hawezi kamwe kutenda na kufikiri Kama unavyofikiri wewe. Akili zake si kama za binadamu.
Bado hujathibitisha kuwa MM hayupo!
Sawa.

Tufanye hivi. Nakupa nafasi kwamba labda uko sawa na mimi nimekosea, tujadiliane kwa kumpa nafasi mtu wa upande wa pili kwamba inawezekana yeye akawa sawa na wewe ukawa umekosea.

Mimi naondoa kauli zangu zote za kukataa uwepo wake huyo unayemuita Mwenyezi Mungu.

Kwa sababu deep down mimi napenda kujua ukweli zaidi ya kushinda ligi tu.

Nafungua ukurasa mpya wa kutaka kumjua. Kama yupo kweli hata mimi nitafurahi kwa sababu nyingi tu.

Nakuuliza swali.

Unajuaje kwamba huyo unayemuita Mwenyezi Mungu yupo kweli na si hadithi tu?

Unajuaje hata hiyo habari ya "Mwenyezi Mungu hawezi kamwe kutenda na kufikiri kama unavyofikiri wewe...." si hadithi tu iliyotungwa na watu ikakubalika bila ya kuwa kweli?
 
Well said bro. U know Kiranga is a type of a guy who thinks that things must make sense with him before they happen.. Kiranga ukiweza kuutambua ukweli huu kwamba when things want to happen they just happen and they don't need to make sense with you before they happen basi utakuwa umepiga hatua kubwa Sana ya ufahamu kwa kuwa sababu kubwa inayo kufanya usiamini kuhusu uwepo wa Mungu ni hiyo "ignorance" kwamba " when things want to happen they must first make sense with you before they happen ".

U think too much bro
 
Unapata wapi sababu ya kusema kwamba things must make sense with me before they happen?

Hivi mimi ninaposoma watu waliokana uwepo wa Mungu walioishi miaka maelfu kabla yangu, hao walikana kivyao au walikana na mimi?

Ninaposema Mungu wa Biblia na Quran hayupo, kwa sababu habari zilizoandikwa kuhusu huyo Mungu zina contradictions, vitabu vinavyomuelezea huyo Mungu vinajipinga vyenyewe, Quran inajipinga yenyewe, Biblia inajipinga yenyewe, hapo nakana uwepo wa Mungu kwa sababu hai make sense kwangu au kwa sababu hata vitabu vyenyewe vinajipinga kabla ya mimi kuvipinga na watu wengi tu tofauti na mimi wanaona hayo?
 
Kabla sijaenda mbali.

Una criticize logic kwa kuandika illogical nonsense, wewe hata hujui logic ni nini na illogical nonsense ni nini.

Umeandika hivi katika ku criticize logic:-

"Wanyama wana miguu minee,mbwa ana miguu minne,basi mbwa ni mnyama"

Hii ni fallacy na logical non sequitur (kuunganisha kimatiki mambo ambayo hayana uunganiko). Hii si logic.

Hii ndiyo logical non sequitur ile ile wanayoitumia waamini "kuthibitisha" kwamba Mungu yupo kwa kusema

1. Ulimwengu upo. Umeumbwa
2. Hatujui kiumbe aliyeumba ulimwengu, hakuna kiumbe aliyeumba ulimwengu.
3. Basi lazima Mungu yupo na kaumba ulimwengu.

Nimemuuliza mtu athibitishe kuwepo kwa Mungu jana hapa akatumia hii logical non sequitur.

Sasa unasema je hii ni mantiki wakati hii ni kukosa mantiki?

Mpaka hapo umeboogie step.

Logical non sequitur is lack of logic, not logic.

Inaonekana huwezi kufikiri katika a very basic level.
 
Unapinga kwa sababu haimake sense with you.

Lazima ukubali kwamba watu wanao amini kuhusu uwepo wa Mungu wanakuzidi kitu kimoja. They all appreciate the fact that when things need to happen they just happen..They don't need to make sense with them before they happen
Una question kuhusu contradiction kwenye Bible na Qur'aan kwa sababu hiyo hiyo kwamba unataka hoja zi make sense with you before they happen.

Mawazo kwamba when things need to happen they have to first make sense with everyone before they happen yalikuwa valid enzi za kina Aristotle.
 
Wewe mwenyewe ukishasema watu wanao amini uwepo wa Mungu wameshakubali kwamba when things happen they happen, they don't need things to make sense to them, hapo hapo umeshakubali kitu kinacho make sense to you.

Yani things happenning without making sense makes sense to you.

Sasa hapo mbona na wewe unakubali jambo linalo make sense kwako la kitu ku happen bila ku make sense kwako?

Unanilaumu kuwa nafanya kitu kile kile ambacho wewe unafanya!

Unaelewa hata point yako ni nini na kwamba point yako inakufanya wewe na mimi tuwe sawa?
 
Mdogo mdogo utaanza kuelewa. Now ur talking. Kwa hiyo umekubali kwamba hoja zako kuhusu uwepo wa Mungu ni invalid?
 
Mdogo mdogo utaanza kuelewa. Now ur talking. Kwa hiyo umekubali kwamba hoja zako kuhusu uwepo wa Mungu ni invalid?
Nitaelewa lini? Nitajie tarehe turudi kuhakiki hapa. Vinginevyo acha uzushi.

Hoja zangu ni invalid kwa sababu gani? Unajua kusoma kwa ufahamu? Au unahitaji mazoezi ya vitabu vya kiada?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…