Mimi ni mfanyabiashara niliyeridhika na shughuli zangu. Ninamsapoti mama kwa sababu hana roho mbaya wala chuki na wafanyabiashara tofauti na mtangulizi wake. Pia kuhusu hizo connection za kisiasa ningezitaka ningezipata kitambo tu.
Familia ya kina Sabaya ni ya kawaida sana. Siyo zile familia za kusema wana ushawishi ndani ya chama na ndani ya serikali au mojawapo ya hizi 2. Ni self made politicians. Kuwa DCs ni ukada ndani ya CCM ambayo hata mtu mwingine maskini anaweza na wengi wameweza. Hakuna string dynasties nchi hii.
Nchi hii huwezi kukosa nafasi ya kisiasa kisa hutokei familia ya wanasiasa au ukoo wa walioshika nchi. Mifano ipo mingi.
Lakini pia hatulingani ushawishi ila madhara yake sio makubwa hapa nchini.