Sabaya Senior (Loy Sabaya) apata Ushindi wa Kishindo Uenyekiti CCM Arusha
Alafu nimegundua Tanzania kiongozi anayepambana na mafisadi na wakwepa kodi anaititwa katili mfano Hayati Magufuli..huo ndio ukweli
Mkuu fasadi alikuwa yeye JPM mwenyewe maana kwa mujibu wa CAG, Musa Asad.

Tirilioni 1.5 JPM alishindwa kuzitolea maelezo zilipoenda! Akaona isiwe taabu akamtimua kwa nguvu! Bila kufuata utaratibu wala sheria!

Mkuu kama ulifahamu zilipoenda utufahamishe maana ni hela zetu wananchi walipakodi, kila mmoja wetu alilipa kodi tena kwa lazima ya kupata risiti juu!

Mkuu usisahau kusemea na elfu ishirini (20,000/=) ya vitambulisho vya majinga zilipoenda!

Je, kwa tafsiri yako huo haukuwa ufisadi? Je, mhusika hakuwa fisadi?

Tuanzie hapo ili tuielewe hoja yako vizuri!!!
 
Habari mbaya sana kwa majizi yote na Chadema
Mkuu chadema wamekuibia nini? Walikuibia lini? Uliwa ripoti Kituo gani cha polisi? Walihukumiwa lini?

Mkuu wewe ni muungwana sana na una uelewa mkubwa wa mambo, kwanini unajishusha namna hii?

Ukisema huwapendi hamna neno, ila kusema ni wezi ilhali hawajakubia kitu sio uungwana mkuu!
 
Ni roho za watu walioachika, kumbuka Geku hana ndoa, alikuwa anapiga mume mbaya kabisa.
Mtu anakaribia menopasue hana mume, vijana wanapita na kupotea lazma awe na hasira.
Wanawake wakipata vyeo kwa kujiuza wanakuwa walipa visasi wazuri sana!
 
CCM kisiki cha mpingo. Wanapeana tu madaraka, huku sisi tukipewa kofia, tisheti na chumvi.
 
Usiyempenda kaja.
---
Mkutano Mkuu maalum wa kumchagua Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha, umemchagua Loy Thomas Sabaya, kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoani humo.

Sabaya ambaye ni Baba mzazi wa aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 473, akifuatiwa na Ndg Daniel Mrisho Pallangyo aliyepata kura 374, Solomon Ole Sendeka Kivuyo kura 59 na Edna Israel Kivuyo aliyepata kura 10.

Sabaya anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen aliyefariki hivi karibuni.

My Take
Kama wewe ni mtoto wa mkulima shika jembe ukalime maana siasa ni connection ya wenye majina.
Tanzania ukiwa na jina maarufu hata kwa kuuwa au ushoga utapita vizuri kwenye uchaguzi wa viongozi!
 
Aliwahi kutoa amri wa kuchoma moto makazi ya wanakijiji kule Serengeti akiwa mkuu wa Wilaya. Kweli uwezi kuwa kiongozi CCM kama mikono yako hainuki damu...hongera sana Familia ya kigaidi kwa kushinda m/k CCM Arusha.
Ni mchapa kazi ..watu walipaswa kuhama wakagoma akawanyoosha..endelea kusema ugaidi
 
Loy Ole Sabaya, baba wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, ameshinda nafasi ya Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha kwa kupata kura 473, kati ya kura 907

Hata hivyo, kabla ya ushindi huo alikumbwa na swali zito kutoka kwa Mjumbe mmoja, swali ambalo lilikatishwa na kuzuiwa kabisa kujibiwa.

Mjumbe huyo alimhusisha Sabaya na utwaaji wa ardhi za Wananchi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara na kugeuza ardhi hizo kuwa Mapori Tengefu jambo ambalo linadidimiza Haki za wananchi hasa wafugaji.

Swali hilo lilizua zogo baadhi ya wapiga kura wakitaka lijibiwe sambamba na muulizaji kukatishwa huku Mwenyekiti wa uchaguzi huo akizuia lisijibiwe.



Pia soma; Sabaya Senior (Loy Sabaya) apata Ushindi wa Kishindo Uenyekiti CCM Arusha
 
Loy Ole Sabaya, baba wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, ameshinda nafasi ya Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha kwa kupata kura 463, kati ya kura 907

Hata hivyo, kabla ya ushindi huo alikumbwa na swali zito kutoka kwa Mjumbe mmoja, swali ambalo lilikatishwa na kuzuiwa kabisa kujibiwa.

Mjumbe huyo alimhusisha Sabaya na utwaaji wa ardhi za Wananchi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara na kugeuza ardhi hizo kuwa Mapori Tengefu jambo ambalo linadidimiza Haki za wananchi hasa wafugaji.

Swali hilo lilizua zogo baadhi ya wapiga kura wakitaka lijibiwe sambamba na muulizaji kukatishwa huku Mwenyekiti wa uchaguzi huo akizuia lisijibiwe.

View attachment 2833465

Pia soma; Sabaya Senior (Loy Sabaya) apata Ushindi wa Kishindo Uenyekiti CCM Arusha
Ndiyo, alikuwa ameandaliwa kwenye hicho cheo. Sasa unasemaje?
 
Ilikuwa sahihi kulizuia
Ardhi hutwaliwa na serikali na kugeuzwa matumizi sio mkuu wa wilaya
 
Akiwa mkuu wa wilaya ya songea mauaji ya raia yalishamiri kwelikweli

Mpaka wananchi wakaandamana kwa mkuu wa mkoa
Tutegemee mengi sana kwa wapinzani, roho za mauaji zinarudishwa taratibu, 2024 uchaguzi wa Madiwani na wenyeviti tutegemee hayo au labda hata yale ya kina Alphons Mawazo, na watch-8.
 
Back
Top Bottom