Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Siku zote wajinga ndiyo waliwao. Mjanja kama mimi siwezi kujimaliza kwa huyo Mwamposa, hata kwa shilingi ya Mkoloni!Juzi Bi. mkubwa wangu kanitembelea nyumbani, sasa yeye ni mmoja wa waumini wa kwa Mwamposa.
Baada ya salamu za hapa na pale akaomba awekewe channel ya Mwamposa aangalie ibada.
Wakati tukiangalia kulikuwa ni kipindi cha sadaka, kilichonishanga ni hii sadaka ya kujimaliza yaani toa chote ulichonacho ili ubarikiwe zaidi.
Nikamuuliza Bi mkubwa na wewe huwa unajimaliza? Akanijibu ndio kuna siku nilijimaliza nikakosa mpaka nauli nikachoka.