Safari ya kununua hisa za NMB inaanzia hapa. Ml 87 stake, liwalo na liwe!

Uliyoandika yote ni point isipokuwa tu hapo uliposema kwamba NMB haiji kufilisika.Labda ni kusaidia kufahamu kwamba NMB inaweza kufilisika.Ispofilisika kwa sababu ya Mabadiliko ya soko itafilisika kwa sababu ya uzembe(complacency),Ama la basi itafilisika kupita Natural Process.

Kwa nini nasema hivi?Ni kwa sababu Kanuni za uchumi zinaongoza uendeshaji wa Benki na kwa kawaida Law of Diminishing return ikianza kufanya kazi utaona namna Benki inavyofilisika.So cha muhimu angalia Vital Metrics ili ufahamu iwapo thamni ya hisa za NMB inaendana na Actual Assets za NMB,Angali ROI ya NMB kama inaendana na kasi ya ukuaji wa BEI ya HISa za NMB.Unaweza angalia Yield yake tua utaona ninachotaka kukwambia.

Usichanganye HYPE ya SOKO na UIMARA WA BIASHARA.

Mwisho,KUCHUKUA MKOPO WA BENKI NA KUUTUMIA KUNUNULIA HISA ni moja kati ya maamuzi ambayo sio ya Kiuwekezaji ambayo mtu anaweza kufanya.Anyway nimesema niweke neno kidogo na nikutakie kila la heri
 
1.Nipe list 3 wa Brokers wauhakika
2.Nimuda gani sahihi wa kununua hisa? Binafsi nina account ya DSE ila sina elimu ya kutosha ya kuanza kununua hisa. Nasubiri zishuke ninune au nifanyaje?
3.Kipi nianze kati ya kununua Hisa, Hati fungani au UTT?
Ingia Youtube ndugu kuna elimu za kutosha..Pia kuna mwamba anaitwa Mwalimu Emilian Busara,mtafute huko pitia elimu zake au kununua kitabu.

Kwenye mitandao ya kijamii pia wamejaa Financial educators wengi.
 
Sijasema nimechukua mkopo bank. Bali nimepewa mkopo wenye riba ya 2% na taasisi ninayofanyia kazi. Ambapo ni almost free loan
 
NMB ni miongoni mwa Systematic Important Banks ( SIBs) Too Big to fail. Hivi kwa akili zako serikali na Bank kuu itaziacha NMB na CRDB zifilisikeπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ unadhani uchumi wa Tz utakuwa kwenye hali gani kwenye hiyo scenario. Hizi banks mbili tu zina market share ya more than 60% Just imagineπŸ€” Kuhusu ROI hii bank imekuwa ikifanya vizuri miaka nenda rudi……. Hilo la Market price ni issue ya Demand and supply sokoni. Kifupi usipo wekeza NMB na CRDB kwenye Banks then uwekeze wapi? Hizo ni kama maji usipoyaoga utayanywa!
 
Mkuu mbona umejitosa kwa kiasi kikubwa hivi
 
Ingia Youtube ndugu kuna elimu za kutosha..Pia kuna mwamba anaitwa Mwalimu Emilian Busara,mtafute huko pitia elimu zake au kununua kitabu.

Kwenye mitandao ya kijamii pia wamejaa Financial educators wengi.
Asante sanaa mkuu
 
Mnaendelea kuwekeza au mnaogopa wadau? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Usiogope calculated risks kwani hakuna pesa rahisi duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…