Safari ya kununua hisa za NMB inaanzia hapa. Ml 87 stake, liwalo na liwe!

Nimeona inashambuliwa. Ina liquidity ndogo DSE ila ni kubwa NSE...

Bei ya sasa ya DSE ni kubwa kuliko hisa hiyo hiyo ukinunua NSE....

Mimi nimeamua kuisoma kwanza hii wave ipite. Nitanunua ikifika 1400-1600
Hapo vzr me nasubiri uchaguzi ukikaribia inashuka sana kutoka na political climate ya Kenya.
 
Hivi mnaonunua hisa za haya makumpuni mnafuatilia financial statements zao kweli au ndio ninyi mnacheza na trending za bei ya vipande?
 
Hivi mnaonunua hisa za haya makumpuni mnafuatilia financial statements zao kweli au ndio ninyi mnacheza na trending za bei ya vipande?
Mkuu kama huna taaluma ya kiuhasibu utafuatilia saa ngapi hayo mambo?

Mengine ni unafuata trend tu. Yani NICOL, NSSF, AFRIPRISE, I TRUST, VERTEX, UGANDA SOCIAL FUND n.k waweke NMB halafu mimi ngumbaru nijifanye nachambua report nitafute nini? Tia hela. Au nachambua CRDB ili iwaje?

Mimi huwa naangalia bei ya sokoni kama inahimilika na kama haijapanda sana then nanunua...

Kuna kampuni nilinunua kwa kuweka trust tu kuwa new management itafanya mabadiliko....

Nyingine nilinunua ikiwa IPO kwa kujua itapanda tu like I trust...

So kuna sababu nyingi zinafanya mtu anunue... Sio financial statement pekee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…