Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,175
- 2,294
@ ZAWADI NGODA ,Na ndiyo maana hili eneo limekuwepo kufumbuwa watu macho ambao hawaoni kama wewe,Hemu niambie tangu 2005 mpaka sasa niambie mafanikio ambayo yapo unayaona zaidi ya kujulikana kama waombaji wakubwa wa misaada na wakati tumekalia utajiri ambao unaliwa kijanja janja na wenye uwezo. Halafu watu wanapo ongelea safari wanalinganisha gharama na hali halisi ya mazingira ya nchi kiuchumi .. Wake up tutakwisha
Mimi nilitarajia nyie mlioanzisha hii THREAD mtafakari faida na hasara za safari za Rais nje ya nchi, leo unanipa kazi hiyo mimi! Unajua, unapoandika thread ni lazima uwe na target (goal), na ndio maana nilipojibu nilijaribu kuwafumbua macho na kuweka target ya thread. Hii ilibidi iwekwe wazi na muanzilishi wa thread, ili thread yake ieleweke.
Kama lengo lilikuwa ni kuhesabu namba za safari (quantity) alizofanya Rais, naweza kusema kuwa thread haijafanikiwa. Lakini kama lengo lilikuwa kutathimini ubora (quality) au mafanikio ya safari hizo, thread ingekuwa na maana zaidi na yenye TIJA kwa watanzania. Leo Thread imekaa kisiasa zaidi kuliko kimaendeleo.