Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

...320 angalau ukizidisha mara siku 3 anazokaa huko, karibu miaka 3 "raisi" yuko uhamishoni ndani ya miaka 6 ya "utawala" wake!
 
By:
JichoD

Jamani hacheni kumpigia JK kelele. Mzee kaenda kuomba ili tupate hela za dagaa watoto wale. Hao wanaogoma, ni viherehere vyao. Hamjui Matonya kazeeka na Jk ndo kapewa urithi wake? Tanzania tumebarikiwa na kiongozi omba omba dunia yote inamjua, hiyo ni moja ya historia aliyotuachia ambayo lazima tujivunie nyie mnapiga kelele zenu wana Magwanda Kha, hamna dogo kweli.

Mwacheni atabasamu huko , Cameroon na Bill gates wako huko pengine anaweza kurudi na hela tununulie dagaa ! Nyie ndo mlimtuma apeleke bakuli sasa kelele za nini? Tayari tunarekodi ya kuwa namba nane kwa uchafu na namba tatu kwa kuomba omba kwa karibuni tutakuwa namba kwa uwoga... kwa hiyo tulieni kaka zangu
 
Pilot jakaya at work
 
Jamaa ni nouma....yaani kwa miaka 6 mwaka mmoja kacheza nje ya nchi lol!!
 
Msimlaumu raisi wetu mpendwa jamani. He is a Vasco Da Gama wa tanzania yuko katika harakati za uvumbuzi wa new economy.
 
320 hizi ni aina tofauti za Safari tu bado muda/siku anazo kaa huko

kazi ipo wakuu
 
UPDATES:

SAFARI ya 321 ya Mh Rais Jakaya M. Kikwete, sasa leo anatua katika nchi ya Afrika kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia atakapowasili leo Jumamosi, Januari 28, 2012
 
Atajirusha sana na mwisho anaanguka
Wapenda starehe hawa wanalijuaga hilo!!!akiendelea hivi wala hafiki 2015....ataanguka tu....tena kwa vilio hivi vya watanzania!!!...ataanguka tu kwa natural causes...mark my word....
 
Wapenda starehe hawa wanalijuaga hilo!!!akiendelea hivi wala hafiki 2015....ataanguka tu....tena kwa vilio hivi vya watanzania!!!...ataanguka tu kwa natural causes...mark my word....

Nimekupata vema sana, dhana hiyo huwa haipingani na binadamu muovu kabisa, mwamuzi ni mungu tu!
 
Wapenda starehe hawa wanalijuaga hilo!!!akiendelea hivi wala hafiki 2015....ataanguka tu....tena kwa vilio hivi vya watanzania!!!...ataanguka tu kwa natural causes...mark my word....
Watz tuache lawama, kila kitu lawama kwa rais sasa mlitaka ashinde ikulu? Alishasema asiposafiri mtakufa na njaaa!
 
UPDATES:

SAFARI ya 321 ya Mh Rais Jakaya M. Kikwete, sasa leo anatua katika nchi ya Afrika kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia atakapowasili leo Jumamosi, Januari 28, 2012
Kwanini ziara nyingine asingetuma mwakilishi? Huu ni uroho wa kusafiri na kupiga picha na masuperstar, Davos na Ethiopia kote yeye??
 
Msimlaumu raisi wetu mpendwa jamani. He is a Vasco Da Gama wa tanzania yuko katika harakati za uvumbuzi wa new economy.
Elimu yake ameshindwa kuitumia kuinua uchumi wetu, halafu akavumbue uchumi mwingine huko inawezekana??
 
akitoka huko anaumiza kichwa na kusafu kwenye internet kucheki mkutano mwingine ata kama ni wa nyanya..anaenda
utasikia RAHISI anakwenda kuhudhuri mkutano wa environmental disaster toronto canada,mwisho wa siku wanakopi na kupest walichokisikia bila kujua tunafotautiana kimazingira,mwishowe yanakuja yaleyale ya kuimiza upandaji wa miti mipya kumbe miti hiyo haifai kwa mazingira ya tanzania,mwishowe inanyonya maji yote inasababisha ukame inakua disaster nyingine kwenye mazingira.
Mwalimu wangu wa mazingira pale chuoni alinambia viongozi wa nchi hii hawana focus nzuri,wanaanzisha policy ambazo haziko relevant,hata zile weak wanashindwa kuziimplement au wanashindwa kabisa kuanzisha policy.
Huyu jk ni janga la kitaifa,tutajutia sana.na bado.
 
Kula bata jk mpaka watie akili!!ukitoka huko andaa safri nyingine EUSTONIA kujadli changamoto za uchumi wa bara la Asia!
 
Kwa mujibu wa kunganisha taarifa za kwenye vyombo vya habari nimepiga hesabu na kugundua safari za mkuu wa nchi mapka sasa ametumia Ka EPA kamoja cha billion 80.5 fedha hizi ukilinganisha na alichokipata utakuta kwamba safari hizi zimetia hasara kubwa kwenye nchi hii.

Hesabu hizi ni kwa kadirio la million 250 kwa safari ikiwa wadau wengine wanasema inafika mpaka million 300, ewe Allah mwingi wa rehema ongea na baba yetu. Amina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…