Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Mh.Dr Jakaya M. Kikwete tangu alivyochaguliwa Oct,2005 hadi sasa April,2013 amesafiri safari za nje ya nchi mara 357...Kikubwa ni kwamba Safari moja inagharimu Mill.300

Tutafakari tokea alivyoanza kusafiri taifa limefaidika na nini ukilinganisha na gharama za kodi za walalahoi.

Nawasilisha....
 
kama safari ziko hivyo hapa TZ huwa anakaa muda gani kuweka mipango ya kuendelea nchi yake, ndio maana kila sehemu ya nchi hii wananchi wanalia na viongozi wanaotakiwa kutatua matatizo ya wananchi nao wanalia kiukweli ni muhimu mshikaji anatakiwa kuingizwa kwenye Kitabu cha guiness dooooo hadi kero.
 
Wasiwasi wangu asije akawa ameandika wosia kama wa Wakili Mawala; wa kuwa azikwe mahali alipofia.
Maana tusije kuwa nchi ya kwanza kuzika Rais nchi aliyofia.
 
Tangu zitolewe sababu zinazosababisha kiti cha rais wetu kisikalike kuwa ni kuitangaza Tanzania katika mataifa yaliyoendelea kana kwamba ni nchi mpya kama Sudan ya kusini ambayo inahitaji kukimbizana katika ulimwengu huu wa maendeleo, nimejiuliza mengi sana,

1. 1. Je, ni safari ngapi amefikisha hadi hivi sasa?

2. 2. Je, amewazidi nini akina Kagame, Kibaki, Mseven na Nkurunziza ambao safari zao zinahesabika?

3. 3. Je, safari hizo zimesaidia kukuza uchumi wetu na kuzipiku nchi jirani ambazo marais wake hawasafiri kama yeye?

4. 4. endeleza na wewe …………………………………………………………………

Sina wivu ila ni haki yangu kujua matumizi ya kodi yangu.
 
Mh.Dr Jakaya M. Kikwete tangu alivyochaguliwa Oct,2005 hadi sasa April,2013 amesafiri safari za nje ya nchi mara 357...Kikubwa ni kwamba Safari moja inagharimu Mill.300

Tutafakari tokea alivyoanza kusafiri taifa limefaidika na nini ukilinganisha na gharama za kodi za walalahoi.

Nawasilisha....

Unataka kutuambia Jamaa walivyopiga 3.7 Bilion zilikuwa ni hela za safari 10 ? Na huwa anachukua Overdraft alafu?
 
jaman duuh this is too much, 345 for 8yrs!
tunaweza kupata details za wa kenye na uganda?
 
Ukisikia na bajeti ya vitafunio magogoni utashangaa,,utajiuliza vitanio vyote hivyo hata Refugees camp hawamalizi. Hii nchi kichefuchefu hadi basi
 
alafu by the way, hizo trip 345..tuseme anatumia siku tatu kwenye misafara yake( hii average tu) kwahiyo huyu rais katumia 1035 days nje ya nchi yake.. kuweka 1035 days into years ni ametumia average miaka miwili nje ya nchi so far!

That is unacceptable!
 
Anamaliza mwaka mmoja akishinda Airport,,ni zaid ya Vasco Da Gama

mkuu, ukifanya calculations amemaliza miaka miwili nje kwa estimates kama nilivyofanya kwenye post yangu juu,kamaliza miaka miwili nje..anaenda mwaka wa tatu
 
mkuu, ukifanya calculations amemaliza miaka miwili nje kwa estimates kama nilivyofanya kwenye post yangu juu,kamaliza miaka miwili nje..anaenda mwaka wa tatu

Ki ukweli inabidi tupiganie Mh.kuingia kwenye kumbukumbu za Guinness..
 
Mpaka hapo safari zake zinatia mashaka nchi. Zimezidi kuwa nyingi na kugeuka mzigo kwa taifa.
 
Back
Top Bottom