Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Nikiuonaga huu uzi tu hapa jf najua bwana mkubwa yuko kwenye pipa anaelekea kubembea au kuvutwa na vitoroli vya farasi.
 
Alipochaguliwa urais 2005 alikwenda kwenye kikao cha AU Ethiopia na akahutubia kwa mara ya kwanza kwa kiswahili. baada ya pale aliporudi akaanza kufunga safari za kujitambulisha kwenye nchi mbali mbali za kiafrika(acha Marekani) Mimi mpaka leo sijaelewa ilikuwaje watu aliowahutubia tayari kama rais wa nchi aanze tena kuwafuata kwao kuwambia "mimi ndiye rais mpya wa Tanzania" Uchaguzi ukishafanyika na dunia ikatangaziwa kuwa rais aliyechaguliwa ni fulani (Kwa kesi ya JK kumbuka alikuwa waziri wa mambo ya nje hivyo hakuwa mgeni kwa viongozi wengi duniani na hasa wa kiafrika akiwa amezunguka sana kwa nafasi yake) si inatosha? Mbona hatuwaoni akina Obama na wengine wakija kujitambulisha kwake?
 
SASA HII KURUGENZI INAPOTOA MAELZO YA SAFARI ZA RAis haioni inamuombua kiongozi wa nchi. je yeye kwanini anaweka pamba masikioni kwa kuendelea kukandamiza fedha za wavuja jasho wa hapa bongo?
 
Akifika muda wa kumaliza urais wake atazunguka nchi zoote akaage kote!hapo sizaidi nchi 45...Kibaki sidhani kama alikuwa anazurula kama huyu fastjet
 
Nadhani mtoa mada alitaka kusema Kiwete kasafiri Km 2770 na sio kutembea!!! Kutembea ni neno tata kidogo na most of the time inamaanisha kutembea kwa miguu!!! (Profesa Safari tusaidie Kiswahili hapa)

Ok Now kama ni kusafiri Km hizo kwa 9 days ukigawanya kwa siku ni Km 307.77 Hizi Km kwa siku Compare na Trip moja ya Mje anagalia tofauti yake kwa benefit kwa Watz halafu ndipo utampongeza au la! Ila binafsi sioni la Kupongeza hapa.

Kama una wasiwasi hapo kwenye Red Umeandika kitu Gani? au na wewe unamaanisha raisi kikwete ni kiwete?

Kutembea kuna siku hizi kuna maanisha kuna leta maana nyingi Kutemea kwa miguu,Kutembea na mkeo,kutembea na Gari yaani ukichukulia mtoa maneno anazungumzia kitu gani na wakati gani Jason bourne Yupo Sawia na ni wewe pekee ambaye hujaelewa kiswahili hiki rahisi kabisa karibu wachangiaji wote wameelewa na ndio kiswahili haswa kinachotakiwa kitumike au ulikuwa unataka kuvuruga sredi tu watu waache kuyaona anayofanya raisi katika kutumbua kodi za Watanzania
 
Last edited by a moderator:
ina maana katika miaka karibu 8 ya rais kuwa madarakani,zaidi ya mwaka 1 ame-spend outside tz,au nimesahau math
 
mbona safari za mwaka huuu 2013 sizioni au alieanzisha huu uzi amechoka kufuatilia?
 
Inamana 2013 rais wetu mheshimiwa dk wa ukweli jakaya kikwete hajasafiri popote duniani?
 
Urais miaka hii 10 Tz ni kama kikosi flani cha muziki ambacho kiongozi wa band anaamka na kuuliza leo show wapi? Kisha wadau wanakwea pipa.
 
Kelele za mlango hizo,kwa nini mnakuwa na wivu Rais wetu mpendwa akisafiri nje kwenda kuhemea?
 
ndugu habari zenu...
mimi nina maswali najiuliza ...
katika kipindi chake kwanza uongozi yaani 2005-2010 mh rais alikuwa ana ziara nyingi za kustukiza katika wizara na taasisi mbalimbali za serikali
je hizi ziara zilikuwa na tija..?
na mbona zimesitishwa..?
pia na baadhi ya mawaziri walikuwa wanatumia hii approach je na wao walikuwa nifuata upepo..?
ama waliona hazina tija?
 
sasa hivi anafanya ziara za kushitukiza za kimataifa
 
Ha ha ha Ninaweza.. Wamechoka.. Maana wamehesabu mpaka pumzi imekata.. Mzee wa "nafuuu" bado anakata mawimbi..

mkuu wasichoke ili tutunze kumbukumbu zetu sawa kwa ajili ya vizazi vijavyo. Huenda akavunja hata rekodi zilizo wahi kuwekwa tutajuaje bila kumbukumbu?
 
mkuu wasichoke ili tutunze kumbukumbu zetu sawa kwa ajili ya vizazi vijavyo. Huenda akavunja hata rekodi zilizo wahi kuwekwa tutajuaje bila kumbukumbu?

rekodi alishavunja alipofikia safari ya 200 Ninaweza.. na hakuna mwingine ambae atakaeweza kufika alikofika yeye.. Vizazi vijavyo waambiwe tu raisi ambae alivunja rekodi ya kusafiri sana ni Mr "nafuuu" ambaye aliweza kusafiri mara 300+s (isomeke pluses)
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom