Anastahili kula kuku Jakaya kawafanyia watanganyika mambo makubwa hakuna rais yeyote aliyafikia haya kuwaletea identity yenu tena "Tanganyika" ama kweli historia inajirudia, uhuru wa Tanganyika kwa kiasi kikubwa ulikuwa na msukumo wa watu wa pwani, na leo mtoto wa watu wa pwani amerudisha tena uhuru wenu Tanganyika, Kikwete anastahili kupongezwa na ni Baba wa mabadiliko Tanzania, mwache ale kuku mpaka amalize muda wake, baada ya kukaa kumlaumu Jakaya jipangeni 2015 haiko mbali hamna hata draft ya katiba ya Tangayika shughulikieni mambo ya msingi ikifika 2015 muweze kusimama sio tena kuitegemea Zanzibar ambayo ina katiba yake, raisi wake, baraza la wawakilishi na mahakama yake, Tanganyika haina kitu zero ya sufuri.
Wazanzibari sasa wanajiandaa kuchagua watu watakaoingia katika commission ya mgawanyo wa mali zilizokuwa za jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hasa zilizorithiwa kutoka East African Community, Watanganyika mna kazi kubwa mbele yenu, kwanza ni kuamua Lowasa awe Raisi wa Tanganyika au shirikisho, lakini mjue kwa kuanzia Rais wa kwanza wa shirikisho atatoka Zanzibar then ndio Tangayika maana hamjatulia, Mtwara inawashinda kuidhibiti mtaiweza Tanzania mpya, so ni Mzanzibari ndio Rais wa kwanza wa shirikisho, ili mpate muda Tangayika kushughulikia matatizo yenu ya ndani, Mtwara, Arusha, Iringa na kwengineko.