Mkuu jioni njema; Hapa mie nasikitika hawa wandugu sijui vipi, hivo mafunzo na elimu waliyo gharamikiwa na kunyanyuliwa
kiwango chao, la ajabu hawatumii akili kufikiri..kweli ni hasara iliyojee kweli hawa wataweza kujenga nchi au kuwajibika na kulipa fadhila ya kimaendeleo, Ni hasara mtupu kuwa na raia wa namna hii yani " matsusi na maneno machafu juu ya jamii ndiyo shahada ya usomi wao, chuki na fitina ndo imani zao, Uharibifu na mparaganyo ipo ndani ya nyoyo na itikadi zao.
Nashangaa sijui tutaishi na wajamaa na maswahiba hawa vipi. Mkuu hebu soma hoja zao na tazama mfululizo wa matamko yao ya kukatiza morali za wananchi na kuwapotezea mwelikeo. Wapo wapo Full nondo kulaumu na kupakiziya.
Kila la heri nchi itajengwa na wachapa kazi na tuzo lao ni development na maisha bora. haijalishi nani awe Rais tupo pamoja.