Sakata la Escrow: AG Werema amvaa Kafulila, Amwita tumbili asiyeweza amua mambo ya msituni

Uelewa mdogo wa viongozi wa bunge ndio chanzo, hawaoni kama kuna kitu ndani ya hoja ya Kafulila na wenzake. Hakili ndogo kuongoza kubwa ndo madhara yake.
 
Viongozi wa ccm kwa matusi hawajambo, ukiona hivo ujue hawana hoja
 
Mzee Werema nafikiri ni mtu makini sana na anastahili kugombea Urais 2015. WEREMA FOR PRESIDENT 2015.
 
Kafulia VS Werema

Mwanasheria Mkuu wa serikali Werema amemtukana Mbunge Kigoma Kusini David Kafulila kuwa ni "TUMBILI" alipoombwa na mbunge huyo kutoa ufafanuzi kuhusu pesa zilizokuwa katika account ya Escrow iliyokuwa bank kuu ya Tanzania.

Kauli kama hiyo si ya kiongozi mwenye nafasi ya juu serikalini tena Mwanasheria Mkuu wa serikali. nakumbuka mara kadhaa amekuwa an mazoea ya kauli za matusi bungeni.

Source: Habari Leo
 
Hili nalo neno, haiwezekani mtu na akili zake timamu tena mwanasheria mkuu wa serikali awe anatukana watu hovyo, tena ni aibu kumtukana mtu mzima kama werema kumtukana kafulila ambaye ni mdogo sana kiumri kwake, ni kweli yawezekana kazi imeshamshosha basi tu afanyeje


Werema amechoka kazi, analazimishwa tu kuendelea...
 

Sikubaliani na wewe, Kiongozi wa ngazi ya juu kama AG, amongst qualities za mtu kama huyu, ambaye alishakuwa Jaji, ni muhimu kuwa na hekima za hali ya juu sana ( charisma) ya kujizuia na kutoa busara zaidi pale anapokuwa provoked. Sio muendelezo wa uhuni tunaouona kwa watu wanaotakiwa kuwa role models.

Inasikitisha na kukatisha tamaa, hivi kizazi hiki hakina mtu atakaye simama kama kioo kwa watoto wetu, hasa hawa watu waliopewa heshima na Rais ya kusimamia na kuamua mambo mengi ya Nchi kwa niaba ya Watanzania?

AG amepoteza haiba ya kuwa Kiongozi, makosa mengi anayoyafanya Bungeni alistahili kujipima, atoke kabla ya kutolewa!
 
Sio lugha nzuri kwa binadamu mwenzako. Usishabikie

huyu jamaa sijawahi kuona ame comment kitu cha maana! ushabiki wa namna hii hata kwenye mambo yasiyofaa ni upungufu wa akili.
 
Tiba Pekee ni Kuandaa Pambano la ndondi Kati ya wale Wabunge wapinzani wa jadi angalau Serikali iingize Pesa kuliko malumbano kuishia hewani pasipo faida yeyote.

YAANI..Judge na Mtafsiri wa Sheria Mkuu wa Serikali anachukua sheria mkononi, kwanza kutoa matusi mazito, ya kihuni na ya kidhalilishaji, pili anaamua akiwa na akili timamu kuacha kiti chake ili akamtwange Kafulila, tatu akijua wadhifa wake na mahali alipo kuwa ni muhimili mkubwa wa kisheria na kimaadili ameshindwa kujizuia na Nne akiwa na taarifa na ufahamu kamili kwamba procession zote za bunge zinarushwa live na runinga, kwa hiyo watoto na watu wazima wanaona moja kwa moja bila ukakasi anachokifanya....

Nashangaa....Inakuwaje vigumu kwake kuona hii kitu imepitiliza haistahili hata kupoteza muda wetu mwingi kumjadili...Nashangaa....inakuwaje uongozi uliomteua haukerwi na tabia hizi?
 
Wadhamani wapo wengi wanangojea Pambano la Ndondi Spika aandaa mapambano watu wajue nani zaidi kwenye nguvu za mikono na ni nani zaidi kwenye nguvu ya Mdomo kuchonga.
Si wametengeneza gym pale bungeni? Hayo ndo matokeo ya kunyanyua chuma,.. Kujiamini. Mbona wanashiriki mpira wa miguu,dansi,mpira wa pete,.. Tuone na ngumi za waheshimiwa,tukianza na hawa wanaotukanana,ifuate ya Lissu Vs Ndugai,Pinda Vs Mbowe, Lema Vs Nchemba, Komba Vs Mbatia...
 


Tatzo sio Musoma; sisi ni wastaarabu. Tunaweza kuwa na misimamo na kupigana lakini si udhalilishaji na matusi. Matusi ni CCM si Musoma; kwani Lusinde, Masaburi, Yule wa ---- (kigoma), juzi hapa Profeseri Tibaijuka, yule mama mzanzibar vs Jusa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…