Sakata la Escrow: AG Werema amvaa Kafulila, Amwita tumbili asiyeweza amua mambo ya msituni

Sakata la Escrow: AG Werema amvaa Kafulila, Amwita tumbili asiyeweza amua mambo ya msituni

Uelewa mdogo wa viongozi wa bunge ndio chanzo, hawaoni kama kuna kitu ndani ya hoja ya Kafulila na wenzake. Hakili ndogo kuongoza kubwa ndo madhara yake.
 
Viongozi wa ccm kwa matusi hawajambo, ukiona hivo ujue hawana hoja
 
Mzee Werema nafikiri ni mtu makini sana na anastahili kugombea Urais 2015. WEREMA FOR PRESIDENT 2015.
 
David-Kafulila.jpg
Kafulia VS Werema
werema-jaji_238_280.jpg

Mwanasheria Mkuu wa serikali Werema amemtukana Mbunge Kigoma Kusini David Kafulila kuwa ni "TUMBILI" alipoombwa na mbunge huyo kutoa ufafanuzi kuhusu pesa zilizokuwa katika account ya Escrow iliyokuwa bank kuu ya Tanzania.

Kauli kama hiyo si ya kiongozi mwenye nafasi ya juu serikalini tena Mwanasheria Mkuu wa serikali. nakumbuka mara kadhaa amekuwa an mazoea ya kauli za matusi bungeni.

Source: Habari Leo
 
Hili nalo neno, haiwezekani mtu na akili zake timamu tena mwanasheria mkuu wa serikali awe anatukana watu hovyo, tena ni aibu kumtukana mtu mzima kama werema kumtukana kafulila ambaye ni mdogo sana kiumri kwake, ni kweli yawezekana kazi imeshamshosha basi tu afanyeje


Werema amechoka kazi, analazimishwa tu kuendelea...
 
Ni kweli wakati Wao wanaongea Werema hakuomba mwongozo wa M/kiti wala hakuwaingilia ingilia alikaa kiimya hadi wakamaliza kuongea,tatizo lilianzia pale walipoanza kumwingilia ingilia ndipo akapoteza umakini kabsa ikawa Kama ilivyokuwa kwa Juma nkamia na Pia Peter Serukamba inapaswa Wabunge wawe wanavumilia kwanza Mtu amalize kuzungumza kisha wajibu kwa kufuata Kanuni, kinyume na hapo tutashuhudia Vioja zaidi ya hivi.

Sikubaliani na wewe, Kiongozi wa ngazi ya juu kama AG, amongst qualities za mtu kama huyu, ambaye alishakuwa Jaji, ni muhimu kuwa na hekima za hali ya juu sana ( charisma) ya kujizuia na kutoa busara zaidi pale anapokuwa provoked. Sio muendelezo wa uhuni tunaouona kwa watu wanaotakiwa kuwa role models.

Inasikitisha na kukatisha tamaa, hivi kizazi hiki hakina mtu atakaye simama kama kioo kwa watoto wetu, hasa hawa watu waliopewa heshima na Rais ya kusimamia na kuamua mambo mengi ya Nchi kwa niaba ya Watanzania?

AG amepoteza haiba ya kuwa Kiongozi, makosa mengi anayoyafanya Bungeni alistahili kujipima, atoke kabla ya kutolewa!
 
Tiba Pekee ni Kuandaa Pambano la ndondi Kati ya wale Wabunge wapinzani wa jadi angalau Serikali iingize Pesa kuliko malumbano kuishia hewani pasipo faida yeyote.

YAANI..Judge na Mtafsiri wa Sheria Mkuu wa Serikali anachukua sheria mkononi, kwanza kutoa matusi mazito, ya kihuni na ya kidhalilishaji, pili anaamua akiwa na akili timamu kuacha kiti chake ili akamtwange Kafulila, tatu akijua wadhifa wake na mahali alipo kuwa ni muhimili mkubwa wa kisheria na kimaadili ameshindwa kujizuia na Nne akiwa na taarifa na ufahamu kamili kwamba procession zote za bunge zinarushwa live na runinga, kwa hiyo watoto na watu wazima wanaona moja kwa moja bila ukakasi anachokifanya....

Nashangaa....Inakuwaje vigumu kwake kuona hii kitu imepitiliza haistahili hata kupoteza muda wetu mwingi kumjadili...Nashangaa....inakuwaje uongozi uliomteua haukerwi na tabia hizi?
 
Wadhamani wapo wengi wanangojea Pambano la Ndondi Spika aandaa mapambano watu wajue nani zaidi kwenye nguvu za mikono na ni nani zaidi kwenye nguvu ya Mdomo kuchonga.
Si wametengeneza gym pale bungeni? Hayo ndo matokeo ya kunyanyua chuma,.. Kujiamini. Mbona wanashiriki mpira wa miguu,dansi,mpira wa pete,.. Tuone na ngumi za waheshimiwa,tukianza na hawa wanaotukanana,ifuate ya Lissu Vs Ndugai,Pinda Vs Mbowe, Lema Vs Nchemba, Komba Vs Mbatia...
 
Hatuwezi moja kwa moja kuita kitendo cha Werema ni kupandwa na hasira. Ni ujinga tu na kukosa busara. Yeye amekuwa akitukana wabunge, hasa wa upinzani kila siku, wapo kimyaa, wanamvumilia. Jana alianza yeye kumtukana Kafulila kwamba ni tumbili, ujinga, ujinga mtupu. Lakini kuna jambo, hawa wenzetu wa mkoa wa Mara balaa. Tujikumbushe....

WASSIRA: Mbali na kuwa na matusi huyu alibatizwa jina la Tyson mchana kweupe katika ofisi za MAELEZO, Dar alipomuwinda kama swala na hatimaye kumpiga Mhariri wa gazeti la DIRA ati kwa kuandika Wassira ni swahiba wa Mrema. Neno "swahiba" kwa Wassira akasema ni tusi na kuanza kumsaka na hatimaye kumpiga! MUSOMA hiyo!

MUHONGO: Huyu anaamini watu waliosoma hapa nchini ni wale waliosomea elimu ya miamba, mawe. Hutukana karibu kila anaposimama bungeni. MUSOMA hiyo!

WEREMA: Huyu ndo kiboko maana yeye huwa hata anafikia kujisifu "sisi watu wa Musoma". Matusi mtindo mmoja na kwa kutokemewa huko nyuma jana alifikia hatua ya kutaka kupigana bungeni. MUSOMA hiyo!

Jamii gani hii ya watu wa kufikia cheo cha Waziri ama Mwanasheria Mkuu ndimi zao zinatema matusi na kutaka kupigana? Wanadai ati huko kwao Musoma kupigana ama kutukana ni SIFA. SIFA???????? Kubwa jinga!


Tatzo sio Musoma; sisi ni wastaarabu. Tunaweza kuwa na misimamo na kupigana lakini si udhalilishaji na matusi. Matusi ni CCM si Musoma; kwani Lusinde, Masaburi, Yule wa ---- (kigoma), juzi hapa Profeseri Tibaijuka, yule mama mzanzibar vs Jusa
 
Back
Top Bottom