SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

....kuna wakati natamani kuishi mwezini, kumbe Tanzania wote ni malofa na mafala!!!!!
 
Penye udhia penyeza rupia una mabilioni chungu nzima ya mkataba feki ambao ulikingiwa kifua na wanene kuliko wanene wote Tanzania ili uupate halafu eti watu wanataka kukuchezea. Nchi hii ufisadi hautakwisha kamwe mpaka pale chama cha mafisadi kitakapopoteza madaraka nchini na hili sijui litatokea mwaka gani maana washajua kifo chao kitasababishwa na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi na kamwe hawatakuwa tayari kufanya makosa ya kuruhusu katiba mpya kwa kutumia rasimu ya John Sinde Warioba. Kigumu chama cha wenye majipu! KIGUMU CCM Oyee! CCM Oyee!
 
We kashfa hyo moja anaingia kitwanga, mwema, lugumi, zitto, riz one, cjui katibu wa nini khaaa!! Ndo maana wameamua wakwepeshe tuu, vita ya ufisad ni ngum kwli
 
Mimi naamini maneno ya Aeshi (?) M/kiti wa PAC niliyemsikia kwa masikio yangu na niliyemuona kwa macho yangu akiongea ITV.

Kamwe sitaamini hili tamko lindana la ofisi ya Bunge. Halafu nani alisema Magu anaweza kutumbua kila jipu? !
Aliyesema Magu anaweza kutumbua kila jipu ni anayewalipa mawaziri mishahara ya uwaziri na ubunge na kuwapa gari la uwaziri na jingine la ubunge huku akizuwia watumishi hewa na wale wanaopokea mshahara zaidi ya mmoja.
 

Mkuu samahani nnaomba utusaidie hapa ,kama hali ndio hii wananchi wanayo nafasi gani kisheria katika hili ukizingatia walio ibiwa ni wao!?
 
HII NCHI BWANA.......! Hivi mababu zetu kina MKWAWA, MACHIEF 40 walionyongwa, wangejua haya yote wangejitoa kweli kuipigania hii nchi hadi kupoteza uhai? Bora Chief Magungo tu, nahisi alionyeshwa na Mungu mapema.
 
Reactions: 911
Kumbe siku hizi runinga zinasema na kuonyesha uongo jamani! Yule nilie muona na kumsikiliza si makati mwenyekiti jamani
 
Hii nchi bora kuwa mwizi tu. Maana wezi na wabadhirifu wa mali ya Umma ndio mashujaa na watanuaji mijini. Jifanye mwema, utazikwa na sanda moja huku umeacha nyumba yako mahame.
 
Mkuu samahani nnaomba utusaidie hapa ,kama hali ndio hii wananchi wanayo nafasi gani kisheria katika hili ukizingatia walio ibiwa ni wao!?
Mkuu hapa kuna hoja mbili. Kwanza, lazima wananchi wawezeshwe kupata ukweli wa tukio zima ili kupitia wanasheria waweze kubaini kama kuna tatizo
Pili, wananchi wana haki ya kuishtaki serikali mahakamani

Yapo matatizo ya aina mbili
Moja, hali iliyopo ni kutaka kufunika ukweli kwa kutumia vyombo na mamlaka zinazohusika.
Dana dana inayoendelea inaeleza ugumu wa kupata ukweli. Utakwendaje mahakamani ukiwa huna ukweli mkononi? Ukiamua kwenda kutafuta haki ya kupata ukweli, la pili litajitokeza

Pili, zitatumika mbinu za kuhakikisha mahakama haikupi uwezo wa kupata ukweli. Hapa ieleweke mahakama haina tatizo, bali mbinu za kiufundi zitakazo ilazimu mahakama kusimamia sharia kama zilizvyo. Nikupe mfano

Yupo mwanasiasa aliyedhuriwa na watu kwasababu za kisiasa. Alipotaka kutaja wahusika , walikamatwa watu wawili watatu na suala likawa mahakamani. Hadi leo hatujui ukweli na uchhunguzi unaendelea

Suala hili limechukuliwa na bunge, hivyo hoja ya kuingilia mihimili inaweza kutumika
Na katika bunge kamati ya ulinzi, usalama na mambo ya nje imekiri kushiriki

Mwisho, unamkymba Katabalo ?
 
Reactions: BAK
Mungu was mbinguni shuka uwasaidie watanzania. Tumeweka mijambazi yenye nguvu na akili madaraka. Halafu yanaigiza na kututaka tuyashangilie eti majipu!! Majipu?!!!stupid baada ya kumtorosha agent was wizi yanatuzuga kijingaaaaa!!!!! Chama cha majambazi awamu ya tank no hatari ya karne.
 
kutegemea bunge hili linaloongozwa na watuhumiwa wa rushwa kubwa kupambana na ufisadi ni maigizo makubwa sana. bunge hili huko mbele litatumika sana kuficha maovu ya serikali na watawala. binafsi sina imani na mtemi chenge kama mmojawapo ya kiongozi wa bunge. huo ni mtazamo wangu.
 
Hakuna Cha Kasim Majaliwa wala Pombe Magufuli
Majipu mengine hayatumbuliki na hili jipu limeshawashinda tayari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…