Sakata la Zumaridi na namna alivyokamatwa na polisi ni kichefuchefu, sheria haikuzingatiwa

Pole sana muumini wa Zumaridi. Kikubwa huyo Zumaridi ana mapungufu makubwa sana ktk utendaji wake. Kwanza Polisi walipoingia mara ya kwanza hakupaswa wale watu wake wa mapepo wawatishie polisi, wewe nadhani uliona hao watu wake wenye majini walivyokuwa wanaruka kama vile wana weza kupambana na serikali. Pia kingine ujue mwanza kuna watu wanakuwa na biashara za viungo vya binaadamu kwenye mambo ya madini na uvuvi, jua kabisa polisi na vyombo vya usalama wana information za kutosha juu ya Zumaridi, kaa utulie mkuu wangu. Mimi simhukumu kwa sababu sina information ila kwa kitendo cha wafuasi wake wenye majini kuwatishia askari tena mmoja yule bonge alitoa bastola kidogo aanze kuitumia lakini akairudisha mfukoni. Asipoangalia Zumaridi atapotea kabisa ktk ulimwengu huu, maana onyo la kwanza alipewa kwa kufungiwa, alipaswa aufate utaratibu wa kibali na kuendesha ibaada zake kwa mujibu wa vibali.
 
Kwahiyo polisi utaratibu walioufanya uko sawa?
Kwanini wamvamie?
Hao mabaunsa wa zumaridi wapole Sana walitakiwa wawatandike Askari wajifunze utaratibu.
Wameenda kizembe Sana eboo
 
Nakubaliana nawe kwa maana ya ukiukwaji wa sheria ila mfalme wako anakashfu imani za watu wengine kitu ambacho kinaweza sababisha uvunjifu wa amani
Kwani huyo mfalme ni dini gani?
Yaani anatumia kitabu gani kuendesha ibada?
 
Hivi kanisa lake limesajiliwa?Katiba yake umeiona?
Au mpaka yatokee kama ya "kibwetere" kuteketeza waumini ndani ndo muanze kulalama tena.. eti serikali ilikuwa wapi!

WAACHE WAFANYE KAZI YAO!
 

Kadanganya nini?
Watoto kawakusanya au wameenda na wazazi wao Kama wanavyooenda kwenye nyumba zingine za ibada?
Kuhubiri kipumbavu ndio kupoje tofauti na wahubiri wengine wote?
Kuna mtu ameporwa au waumini hupeleka sadaka na matoleo Yao Kama ilivyo kwa madehebu mengine?
Mungu yupi unamjua anaejifananisha nae maana miungu ni wengi wajuaje nae ni mungu kwa Imani yake? Kwani lazima mungu wake awe ndio yule wako na wenu? Tangu lini watu wapangiwe Aina ya mungu wa kumuabudu?
Kwahiyo kosa lake hajasoma katiba? Watanzania wangapi hawajaisoma?
Kila mmoja apaswa kusoma vitabu vitakatifu? Ni vipi haswa? Kwanini viwe vitakatifu kwa kila mmoja wakati Imani sio moja?
Ikiwa zumaridi Hana vibali vya kuendesha ibada hiyo yaweza kuwa kosa kisheria za nchi, lakini mengine ni wivu wenu tu hamna tofauti nae.
Masuala ya Imani hayawezi fanana kwa watu wote kwani Safari ya Imani haiko uniform kwa watu wote.
 
Kosa labda ni hao watoto kutokwenda shule kwa sababu wazazi wao wamewapeleka hapo lakini mengine yote ni wivu wenu tu.
Kwani utaratibu wa ibada lazima mfanane?
Muelimisheni azingatie sheria za nchi kwa watoto kwisha habari
 
Kwani Kuna tofauti gani Kati ya cult na hiyo unaita kanisa?
Huko kanisani hamkusanyiki na kufanya mambo yenu ya Imani?
Acheni wivu
 
Mkuuu nawewe ni mfuasi wa huyu mtu?? Au ni Miongoni mwa wale Zombies wa juzi waliorekodiwa?

Tuweke utani pembeni sisi watu Weusi tumepoteza dira kwenye masuala mazima ya kuabudu kwa sasa tunfanya mazingaombwe tu.
Hujawaona wazungu wanaombea silaha za urusi zisiwadhuru Ukraine?
 
Walifuatwa majumbani kwao?
Wanaenda sababu ya shida zao, ingefaa Sana Kama mngewatatulia shida zao ili wasiende huko mnakosema kubaya
 
Kwahiyo polisi utaratibu walioufanya uko sawa?
Kwanini wamvamie?
Hao mabaunsa wa zumaridi wapole Sana walitakiwa wawatandike Askari wajifunze utaratibu.
Wameenda kizembe Sana eboo
Je wewe una uhakika hawakuwa na kibali? Msipende kuteta vitu usivyovifahamu. Kwa ufupi hayo mapepo yake nadhani yalishaanza kutoka maana keshapata kichapo cha kutosha na wigi hana tena. Unajua wakichapwa waislamu huwa wakristo mnashangilia, rejea mwebe yanga, sasa kwa huyu kushushiwa tu kichapo kidogo inakuwa nongwa.
 
Mwenye picha za mfalme zumarid aweke maana mleta uzi kashindwa kabisa kuweka
 
Mkuu take time google Sheria ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu afu uje fasta ufute Uzi wako...!
Mimi kosa ninalo liona ni kuwa Polisi walikwenda kizembe ...Yale Mamisukule yangeweza hata kuwaua!
 
mbona Mungu mwenyewe amepoa tu jamani?

Hiki unachoeleza hapa kina utofauti gani na wale wanaomtetea Mungu wao kwa Mapanga na Mitutu?
 
Kuna michango ya watu humu inatia Kichefuchefu.

Watu wanataka tufanane mawazo. Hata kama mawazo yao ni ya kipumbavu.
 
Umetaja watu wawili

1.Zumaridi
2.Zumalidi.

Yupi ni yupi na yupi si yupi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…