Sakata la Zumaridi na namna alivyokamatwa na polisi ni kichefuchefu, sheria haikuzingatiwa

Sakata la Zumaridi na namna alivyokamatwa na polisi ni kichefuchefu, sheria haikuzingatiwa

Kwani kufanya maigizo ya kijinga ni kinyume cha sheria au Katiba ya nchi?
Mbona Masanja huwa anafanya maigizo ya kijinga na hakamatwi?
Mwambie!kwanza Hadi makanisa mama yana maigizo kwa nini huwa wa naongea kama wanaimba?hebu refer '' Bwana awe nanyi. ''
 
Huwezi kumpenda Yesu usiyemjua wala kumuona ukamchukia Zumaridi uliyemuona kwa macho na kumsikia.
Basi tuseme Mungu na hafai kwasababu hatumuoni Wala kumjua..

Ikae hivyo ki-atheist zaid, Au na Hilo unapiga mkuu?
 
Mtoa mada na ww ni kati ya yale mazombie ya zumaridi???🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
1.Je!Biblia ilieleza style ya kudance unapomtukuza Mungu?kiungo chochote unachokiona kwenye mwili wa binadamu kimeumbwa kwa mfano wa Mungu,hata akikata mauno ni kiungo cha Mungu sema binadamu mmetunga sheria zenu,sijaona kwenye amri kumi za Mungu sehemu iliyokataza kucheza kwa kutumia style Fulani na viungo fulani tu. Kuhusu mavazi hakuna sehemu imesema haya ni mavazi ya kikiristo au haya ni kipagani....

2.Yehova kampa kila binadamu utashi wa kuchagua mema na mabaya. na kila mtu atalipwa ujira wake sawasawa na matendo yake... Wale watu kwa hiari Yao wameamua kumuamini nyie wana dunia mnaanza kuwahukumu,je? hiyo ni kazi yenu kuhukumu au kazi ya Yehova?Jamani tusiwe kama mafarisayo

1.Biblia imeeleza watu wavae mavazi ya kujistiri mwili, kupitia mavazi uamsha tamaa ya uasherati.mavazi ya kumtukuza shetani mfano taiti, kaptula, bikini, suruari, vimini lengo kuu ni kuchochea tamaa ya uzinzi.Maandiko yameeleza kila kitu Mkristo aweje kuanzia Vyakula, mavazi,
 
Kulingana na sheria ya Tanzania hukumu mtu anayemdhiaki Mungu ni kifungo cha muda gani? Au ni faini kiasi gani?
Kosa la kudhihaki Mungu,kutumikisha wanaume ki....no ,na kusafirisha binadamu kinyume cha taratbu
 
Kabisa, cha ajabu mtu anatangwa IMAGE INACHAFULIWA halafu baadaei anaachiwa kwa kukosa ushahidi! Brand za watu zilindwe, kama kuna makosa, sheria zifuatwe huo ndiyo ubinadam!
SIUNGI MKONO UCHAFU WOWOTE! LAKINI IPO HAKI YA MTUHUMIWA
Binafsi yangu Mimi nashindwa kumpinga kwa kuwa police hawana cha maana wanachoeleza kuhusu mtuhumiwa,wanadai kashtakiwa kwa ajili ya Human trafficking ya watu 149 mbona hawasemi kawa traffic kutoka wapi,kwenda wapi,kwa lengo gani?UBABAIFU!Niamini,kuna sehemu kuna mtu ana maslahi na hii case. Hawa mapolice washapoozwa
 
Mkuu DP,Kama kuna taratibu za kufuata mbona ile siku ya kwanza police Hawa kufuata taratibu za kumkamata,walienda bila search warrant wakaingia kikomandoo.kwa nini rule ukuta wa mtu na geti lipo?,siku ya pili ndio wakaenda kiutaratibu Je hiyo imekaaje?
Baadae ya polisi kuruka ukuta, nyie mlichukua hatua gani?

Hivi unajua issue ya kwenda kumkamata mtu kahifadhi wahamiaj haramu Ni Kama vile unavokwenda kumkamata mtuhumiwa wa ugaidi au madawa.

Hawa watu wa human trafficking Mara nyingi huwa wako na silaha za moto kujilinda, na wako tayar kufanya chochote ilimrad wasitiwe Kwny mikono ya sheria.
(Fuatilia wanavyokamtwa waethipia wanaozamia tanzania Mara nyingi)

Na ukisema ufuate utaratibu,
utafeli kuwakamata maana wengi wao huwa wako connected na viongozi corrupt wa mitaa na police.
Ukinifanya unatoa taarifa, ukienda ukuti mtu.

Nadhan police walitaka kuwakamata ready handled, caught on surprise.

WALICHOKIFANYS POLISI SIO KITU KIGENI KABISA KWNY MASUALA YA UKAMATAJI WA WATU WA HUMAN TRAFFICKING.
 
Nyie chekeni tu lakini akija kamatwa kiongozi wa kisiasa kwa style ileile mtakuja kunielewa!

Hatukatai makosa! Lakini sheria zinafuatwa? Makosa wanayotuhumiwa na makosa ya Jinai kweli au ya kupikwa?

AIBU TUNAIPATA MAHAKAMANI
Wacha kila kitu kuwahi kwenye siasa.

Wewe huenda ni mmoja wa mazombie yale tuliyoyaona pale.

Ebu tembelea youtube na uangalie kipande cha video clip ya hao wanaojifanya mazombi wa zumaridi jinsi walivyomnyanyasa yule askari aliekwenda pale.

Tena Polisi walifanya ustaarabu kwa kuondoka baada ya kufanyiwa fujo na mazombie wa Zumaridi,kabla ya kurudi siku ya pili.
Ambapo Zumaridi na mazombie wake walijihami kwa kufunga gate ili askari wale wasiingie.

Pia polisi walikwenda pale kwa kutimiza amri ya mahakama ya mkuyuni,ambapo kuna mtu alikuwa amefungua kesi ya mke wake pamoja na mtoto aliyestahili kuwa shule na badala yake amekwenda kuishi kwa Zumaridi.
Hivyo mahakama ndiyo ikatoa amri kwamba mama yule akamatwe pamoja na mtoto yule ili aweze kuendelea na masomo.
Kilichofuatia ni Zumaridi kuwatuma Zombie wake kuwazuia askari wale kutimiza wajibu wao.

Watanzania tusikimbilie kujificha kwenye siasa kwa kila jambo,hata yale ambayo ni wazi kwamba yako kinyume na sheria.

Zumaridi anatuhumiwa kusafirisha watu,wakiwemo watoto waliostahili kuwa shuleni.
kutoka sehemu mbalimbali za nchi na kukaa nao mle huku akiwaaminisha yeye ni Mungu.

Kanisa lake pia lilikwisha fungiwa kwa kufanya shughuli zake bila kibali.

Eneo alilokamatiwa ni eneo la makazi ya watu na hivyo amekuwa kero kwa wakazi wa eneo lile kwa kelele zisizokoma kutokana na ibada za kishetani za Zumaridi.
 
Sheria gani inasema ukileta mgeni kwako, ukiwa na kipaimara au msiba unatakiwa kuripoti serikali ya mtaa?

Tuwekee hiyo sheria na hukumu yake kwa wasioifuata.
Wacha kutetea ujinga.wale mazombie yalikuwa kwenye kipaimara wakati yakifanyia askari uzombie ule?
 
1.Biblia imeeleza watu wavae mavazi ya kujistiri mwili, kupitia mavazi uamsha tamaa ya uasherati.mavazi ya kumtukuza shetani mfano taiti, kaptula, bikini, suruari, vimini lengo kuu ni kuchochea tamaa ya uzinzi.Maandiko yameeleza kila kitu Mkristo aweje kuanzia Vyakula, mavazi,
Swali la kwanza hujanijibu..

2. Wakristo wote Tanzania sijaona wanajisitiri naongea kwa Experiences kila siku naenda kanisani,kujisitiri wanajisitiri waislamu tu...haya Zumaridi kavaa nini cha ajabu pale?nimepita you tube mbona hakuna la ajabu pale,kama ana mapaja manene sio yeye wa kilaumiwa.... msikuze mambo jamani.... Acheni kutoka vibanzi wenzenu wakati nyie mna maboriti
 
Hata mimi sioni sababu.
Halafu Tanzania uwa inafurahisha. Akikamatwa mtu wanayempenda bila kufuata sheria, raia inalalamika, akikamatwa mtu wasiyempenda bila kufuata sheria, raia inasema hata kama ache akamatwe.
Hili ni tatizo kubwa hata kwa vijana kadhaa wa upinzani na wanaharakati wanaolalamika vyombo vya dola vinawaonea.
 
Kosa la kudhihaki Mungu,kutumikisha wanaume ki....no ,na kusafirisha binadamu kinyume cha taratbu
Kuna mwanaume aliyelalamika kutumikishwa kingono? Acheni ujambazi wenu ninyi.
 
Baadae ya polisi kuruka ukuta, nyie mlichukua hatua gani?

Hivi unajua issue ya kwenda kumkamata mtu kahifadhi wahamiaj haramu Ni Kama vile unavokwenda kumkamata mtuhumiwa wa ugaidi au madawa.

Hawa watu wa human trafficking Mara nyingi huwa wako na silaha za moto kujilinda, na wako tayar kufanya chochote ilimrad wasitiwe Kwny mikono ya sheria.
(Fuatilia wanavyokamtwa waethipia wanaozamia tanzania Mara nyingi)

Na ukisema ufuate utaratibu,
utafeli kuwakamata maana wengi wao huwa wako connected na viongozi corrupt wa mitaa na police.
Ukinifanya unatoa taarifa, ukienda ukuti mtu.

Nadhan police walitaka kuwakamata ready handled, caught on surprise.

WALICHOKIFANYS POLISI SIO KITU KIGENI KABISA KWNY MASUALA YA UKAMATAJI WA WATU WA HUMAN TRAFFICKING.
Wewe hayo ya wahamiaji haramu umeyatoa wapi bro?Wale ni wa Tanzania kamili na vitambulisho vya NIDA wanavyo... Ndio maana tuna sema report ya policcm Ina UKAKASI.
 
Nakubaliana na wewe hapo kwenye kumkamata zumaridi hata Mimi niliona Sheria ilipindishwa Sana lakini hii huwa inatokea Mara nyingi hasa kwa jeshi la polisi hapa Tanzania askari anakuja tu anamkamata raia bila kufuata taratibu maalum.
Hapo kwenye mashtaka ya mtuhumiwa kuhusu kusafirisha watu nadhani wamemaanisha human trafficking? ambayo tafsiri yake kisheria inaweza kua Pana sana, wataalam washeria watatusaidia.
Kuhusu ibada ni kweli kuabudu sio kosa kisheria lakini umefuata taratibu? Kumbuka zumaridi alikua na kanisa na likafungiwa kwa sababu zilizowekwa wazi kisheria na zilizokua na mashiko kabisa na alitii amri, so kitendo Cha yeye kuanza kufanya ibada nyumbani kwake maana yake kahamishia kanisa pale ambapo kwanza sio eneo la kanisa ni eneo la makazi na pia bado vigezo vilivyofanya afungiwe Mara ya kwanza hajavitimiza lakini analazimisha kuendelea na kanisa lake.
Kama anataka kuabudu bila kusumbuliwa afuate Sheria asajili kanisa lake na afuate taratibu zote za kisheria hakuna atakayemsumbua hata wakitaka kulala humo kanisani hakuna atakayewafuatilia.
Sababu gani za kisheria zilizosababisha kanisa lake kufungiwa?
 
Tatizo tunakimbilia kulaumu bila kufatilia kwa kina, nahili limekuwa Tatizo kwa vijana wengi.

Kamanda wa polisi ameeleze vyema kabisa, kwamba wao walienda kumfata mtoto kwa kibali cha mahakama nahuyu mtoto inasemekana alitoroshwa hali iliyopelekea asiendelee na masomo.

Walipofika kwa huyo mama hawakupewa ushirikiano, wakaongeza kikosi wakaingia kwa nguvu na kukuta mengine yanayoendelea humo ndani ni kinyume cha sheria.

Naweza kuwa nimeongeza au kupunuza maneno ila tafuta maelekezo ya kamanda wa polisi yatakusaidia
Mtoa mada anamihemko
 
Back
Top Bottom