Nyie chekeni tu lakini akija kamatwa kiongozi wa kisiasa kwa style ileile mtakuja kunielewa!
Hatukatai makosa! Lakini sheria zinafuatwa? Makosa wanayotuhumiwa na makosa ya Jinai kweli au ya kupikwa?
AIBU TUNAIPATA MAHAKAMANI
Wacha kila kitu kuwahi kwenye siasa.
Wewe huenda ni mmoja wa mazombie yale tuliyoyaona pale.
Ebu tembelea youtube na uangalie kipande cha video clip ya hao wanaojifanya mazombi wa zumaridi jinsi walivyomnyanyasa yule askari aliekwenda pale.
Tena Polisi walifanya ustaarabu kwa kuondoka baada ya kufanyiwa fujo na mazombie wa Zumaridi,kabla ya kurudi siku ya pili.
Ambapo Zumaridi na mazombie wake walijihami kwa kufunga gate ili askari wale wasiingie.
Pia polisi walikwenda pale kwa kutimiza amri ya mahakama ya mkuyuni,ambapo kuna mtu alikuwa amefungua kesi ya mke wake pamoja na mtoto aliyestahili kuwa shule na badala yake amekwenda kuishi kwa Zumaridi.
Hivyo mahakama ndiyo ikatoa amri kwamba mama yule akamatwe pamoja na mtoto yule ili aweze kuendelea na masomo.
Kilichofuatia ni Zumaridi kuwatuma Zombie wake kuwazuia askari wale kutimiza wajibu wao.
Watanzania tusikimbilie kujificha kwenye siasa kwa kila jambo,hata yale ambayo ni wazi kwamba yako kinyume na sheria.
Zumaridi anatuhumiwa kusafirisha watu,wakiwemo watoto waliostahili kuwa shuleni.
kutoka sehemu mbalimbali za nchi na kukaa nao mle huku akiwaaminisha yeye ni Mungu.
Kanisa lake pia lilikwisha fungiwa kwa kufanya shughuli zake bila kibali.
Eneo alilokamatiwa ni eneo la makazi ya watu na hivyo amekuwa kero kwa wakazi wa eneo lile kwa kelele zisizokoma kutokana na ibada za kishetani za Zumaridi.