Sakata mafuta ya kula: Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza bandarini na kukagua matanki ya mafuta

Ziara ya ghafla na TBC wapo ! Humdanganyi mtu yeyote ! Halafu badala ya kukagua hivyo viwanda zaidi ya elfu 3 ambamo bila shaka vya mafuta ya kula vimo kwanini anaenda bandarini ?
Kuna breaking news bila waandishi?
 
Kajichanganya kwenye crude, semi refined na double...Nakumbuka pale ikulu alismea semi refined na double "Piga kodi ya kuereweka iri waache kuturisha uchafu"

Sasa kwenye crude unatozaje ghali? Halafu mafuta yakipanda bei unakuja hapa tena kupiga porojo. Huyu mzee michosho kweli!
 
Mlicheza na Sheria ili mtupige...sasa mmeshtukiwa mnahaha
 
Anakera! Wa kulaumiwa ni Kiwete na Mkapa! Mateso yote y Watanzania mtayabeba hata kaburini huko mtakako kuwa!
 
Kwenye crude piga kodi ya maana ili viwanda vyetu vikue
 
i muda mfupi baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandari ya Dar es Salaam
 
Unless huelewi tatizo hili limesababishwa na nini.

Yeye ndiye aliyesema kwamba anashangaa kwa nini tunaendelea kuleta mafuta toka nje. Akasema kuwa hao wanaoleta mafuta toka nje wapandishiwe kodi. TRA wakatekeleza agizo lake. Wakaenda mbali zaidi, wakawataka waagizaji wa mafuta ghafi walipie kodi kama vile wameingiza mafuta yaliyokamilika na siyo mafuta ghafi.

Waagizaji wakakataa. Mafuta yakadoda bandarini. Ndiyo hayo aliyoenda juyaona.

Hivi unajua kuwa hayo mafuta ghafi hata kama waagizaji wakikubali kulipa kodi kama mafuta yaliyokamilika, ni wewe na mimi ndio tutakaoumia maana wafanyabiashara ni lazima wataongeza bei? Sasa hapo ndiyo utasema huyu bwana ana huruma na watu wa chini?

Jambo la muhimu la kutambua ni kuwa hii nchi haianzi leo, imekuwepo, serikali imekuwepo miaka yote. Yeye anafanya kama vile nchi imeanza leo na kama vile kabla yake hakukuwepo na serikali. Badala ya kujifunza, aelewe kila jambo kwa nini lipo kama lilivyo, na inapobidi arekebishe, yeye anavuruga kila kitu. Na hiyo ndiyo sababu kila anachofanya hakileti matokeo chanya kwa maisha ya wananchi.
 
Serikali kama inadhani biashara au uwekezaji ni rahisi, itangaze kuwa itafanya yenyewe kwa kupitia TRA. Mambo yetu yamekaa kijinga kijinga hivi. Vifu ambavyo hatustahili kufanya ndivyo tunavyofanya.
 
Hahaha sasa watu washashtuka mkuu anatembea na kibunda ndomana lazima atafatwa kuombwa mpunga.....

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…