Sala ya Iddi kitoka Msikiti Mkuu wa Bakwata, Kinondoni DSM: Mgeni Rasmi Baraza la Iddi ni Rais Samia, JK, Salma, Mchengerwa Ndani!. Eid Mubarak!

Sala ya Iddi kitoka Msikiti Mkuu wa Bakwata, Kinondoni DSM: Mgeni Rasmi Baraza la Iddi ni Rais Samia, JK, Salma, Mchengerwa Ndani!. Eid Mubarak!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi

Nafuatilia live ya Swala ya Idd El Fitri kupitia TBC live!, kutokea kwenye Msikiti Mkuu wa Bakwata, Msikiti wa Mfalme Mohammed wa 6 wa Morocco, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Karibuni

View: https://www.youtube.com/live/c2Ad4IXVKUU?si=OMJZtMBCkCXGDagu

Nimemuona Rais Samia amehudhuria ibada hii kama muumini wa kawaida.

Kwenye Uislamu na kwenye Swala za Kiislamu Msikitini, hakunaga mgeni rasmi isipokuwa Allah!, na mwanamke haruhusiwagi hata kuzungumza!, hivyo Rais Samia hakuzungumza lolote hapo Msikitini hata kusalimia tuu.

Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Aboubakar Zubeir Bin Alii, amewanasihi Waislamu kutotenda dhambi siku ya leo, wasije wakaharibu funga yao yote!. “kufanya dhambi leo, ni kama kufanya dhambi siku ya kiama mbele ya Allah Subhana wa Taala”.

Pia Mufti Mkuu, ametukaribisha kwenye Baraza la Iddi, litafanyika ukumbi wa JNICC , mgeni rasmi ni Rais Samia. ambapo huko sasa ndio Rais Samia atazungumza!.

Karibuni.

Paskali
 
Hivi kwenye swala za misikiti mingine kama:
Masjid al-Nabawi
Masjid al-Haram
Imam Reza
Nao wanafanya kama tunachokifanya Tanzania?! Mwanamke anatoa hutuba!?? 😃 Hii nadhani ni Tanzania pekee duniani ndo tumepata kuiona
 
Duh aiseee hatimae mwanamke anahesabika ugeni rasmi msikitini
Hili nimelisema mimi, kwasababu nimemuona Rais Samia yupo!.
Kwenye Uislamu na kwenye Swala za Kiislamu Msikitini, hakunaga mgeni rasmi isipokuwa Allah!, na mwanamke haruhusiwagi hata kuzungumza!. Rais Samia ni atakuwa mgeni rasmi kwenye Baraza la Iddi mchana huu pale JNICC.
P
 
Back
Top Bottom