Salamu ya Rais Samia Suluhu 'Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano' ni salamu bomba sana

Idumu Jamhuri ya Muungano....nimekopi ile ya kidumu chama cha Mapinduzi [emoji23][emoji23]
Kiitikio hakifai kabisa.

SAALAM.
Nawasalimu kwa jina na Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

KIITIKIO NAPENDEKEZA
1, Tuilinde na kuijenga nchi yetu
2. Tuwaenzi waasisi wake
 
Team Magufuli mmesha anza maneno yenu ya hovyo hovyo, Tanzania ni nchi isiyo na dini ingawa watu wake wana dini kikatiba ipo hivyo, sasa usitake kulazimisha Rais aishi kwa kile unacho amini wewe huo ni ujinga

Kama huyo mungu wenu magufuli aliwaaminisha kwamba kutaja taja mungu ndio utakatifu basi aliwaposha sana, na ndio maana mmekuwa wajinga wajinga, ucha mungu unatakiwa uuishi sio kujiongelesha ongelesha kwa watu kwenye majukwaa halafu kumbe unaficha ukatili, uuaji, utekaji, uongo, uzinzi,lugha chafu zisizo na utu, na mengine mengi ya hovyo hovyo.
 
Mi naona atusalimie tu hivi, 'Hi guys!'
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano.

Hii ni salamu bora kutokea toka tumepata uhuru.

Mama endelea kutumia hii salamu kila mara.

Salamu hii haina ubaguzi, ni salamu yenye kuunganisha Taifa.
Yaani Madam President ameongeza quality of my life. Tuzidi kumuombea afya na ulinzi wa Mungu. Naona mwanga
 
Hi salamu itumike ktk shguli za kitaifa mnk hao watajao jina la bwana si wa kuwaamini
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano.

Hii ni salamu bora kutokea toka tumepata uhuru.

Mama endelea kutumia hii salamu kila mara.

Salamu hii haina ubaguzi, ni salamu yenye kuunganisha Taifa.
Hii nzuri, siyo zile za imani ya dini
 
Kaikwepa ile ya Bwana asifiwe......
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano.

Hii ni salamu bora kutokea toka tumepata uhuru.

Mama endelea kutumia hii salamu kila mara.

Salamu hii haina ubaguzi, ni salamu yenye kuunganisha Taifa.
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano ni salamu ya kitaifa kwelikweli😀😀

1.Asalam aleykumu
2.Tumsifu Yesu kristu
3.Bwana Yesu asifiwe
4.Bwana yesu atukuzwe

Tutakutana nazo ibadani😅😅

Watanzania ndo mlipiga kura CCM ikapata ushindi wa kishindo uchaguzi wa 2020.
Hongereni sana watanzania,endeleeni tu kutu zoom.
Hongera sana, tena sana.
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano ni salamu ya kitaifa kwelikweli😀😀

1.Asalam aleykumu
2.Tumsifu Yesu kristu
3.Bwana Yesu asifiwe
4.Bwana yesu atukuzwe

Tutakutana nazo ibadani😅😅😅
Siyapendi mimi hayo masalamu ya sijui asalam nini nini...
 
Wanabodi siku ya uapisho wa Katibu Mkuu Kiongozi ndugu katanga kuna jambo lilitokea, Bwana katanga alisalimu Raia kwa lugha moja tu ya dini ya kiislamu yaani Salaam Allahkum na akaendelea na hotuba yake,

Tutumie maneno ya Kiswahili fasaha wakati wa Salamu tuachane na Haya maneno ya makanisani au Misikitini

Ikumbukwe pale kuna makundi mengi

Mama Samia aligundua kundi kubwa halijaridhika na ile Salamu Yeye akasalimia kwa Salamu mpya yaani"Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ni maoni yangu tu bora kama mtu anaona kusalimia kwa lugha za dini ni kero basi atumie" Habari zenu wananchi"

Wanasiasa wanasalimia kwa lugha zote ili kuleta umoja, Sasa ukisalimia kwa imani yako tu hii itagusa watu fulani tu

Nakupongeza sana Mama Samia kwa kuliona hilo na kulirekebisha pale pale kuna ujumbe umetuma kwa huyo msaidizi wako
 
Mama Mbunifu mno!

Atatufaa
 
Acha UDINI

Sent from my Moto E (4) using JamiiForums mobile app
 
Acha UDINI

Sent from my Moto E (4) using JamiiForums mobile app
Unafahamu maana ya udini au unaongea mambo usiyoyafahamu

Je Adam na Hawa wapo mbinguni au motoni?

Adam na Hawa ndio watu wa kwanza na walifanya makosa

Unajua wapo wapi Mbinguni au Motoni?

Usiongee mambo usiyoyajua kuhusu udini

Rudi shule kasome sana maana ya hizi Dini

Zilikuwepo dini kabla ya uislamu na ukristo

uislam na ukristo ni Dini za karibu tu
 
Acheni ujinga bila kusalimiwa kwa salamu ya kidini inamaanisha huna Mungu???

Mama kafanya vizuri! Imani ibaki suala la mtu binafsi kwenye salamu tunasalimiana kwa Jina la Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Kwanza Kwa taarifa yako hata iyo Salam Alyekum sio salamu ya kiislamu, icho ni kiarabu tu ambacho maana yake ni amani iwe nawe. Sawasawa na myahudi akisema shalom zote zinamaanisha amani iwe nawe.

Huyo Marehemu ambaye kila mda alikuwa anamtaja Mungu Mbona yeye ndo alikuwa muuaji, mshenzi na mbambikaji kesi mkubwa????

Mataga muacheni Mama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…