Salamu za pasaka kutoka katika taasisi za Serikali zinasikitisha

Wakristo wa mapema, walitambua nguvu ya yai kama ishara ya maisha mapya, waliunganisha mayai na maisha mapya yaliyopatikana katika Ufufuo wa Yesu Kristo wakati wa Pasaka.

Mayai ni ishara kamili ya Pasaka, na ishara ya maisha mapya katika Kristo. Fikiria mstari ufuatao maarufu wa Mtakatifu Paulo, “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; tazama, kila kitu kimekuwa kipya!" ( 2 Wakorintho 5:17 ).

Zaidi ya hayo, yai ni kielelezo cha Ufufuo wenyewe kifaranga akitoka kwenye ganda lake anawakilisha Yesu akitoka kaburini mwake siku ya Pasaka.

Copy & paste
 
Udini umeshika kasi awamu ya sita, mama hapendi kabisa ukristo anatamani usingekuwepo ila haiwezekani.
Sio yeye ni mafundisho ya dini ile kwa watoto wao.


Tuzidi kuwaombe..waipate neema ya Yesu kristo maishani mwao.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hata wangeweka picha ya bangi, haitikisi imani yetu ktk kristo na nguvu ya msalaba. hivyo usiwe na hasira mkuu
 

cc: Carleen, hebu msikie huyu.!
 
Wanauogopa msalaba ingawa wanaweza kuokolewa kwa huo wakitubu.
 
Jamani ee dini za watu hizi sie tufate tu wanavyotupeleka
 
Kuna baadhi ya thread ukisoma unapata picha halisi ya akili za great thinkers. Chama cha kijani kitatawala kwa miaka mingi zaidi kwa mwenendo huu.
 
Tatizo ni kwamba dini nyingi si zetu- sisi tumeiga tuu ukristo au Uisilamu. Wewe kama kweli ni mkristo ungejua haya mayai kwenye sherehe ya pasaka yanatoka wapi. Kwenye Christmas kuna Santa claus na kwenye Pasaka - watu wa majuu wanatumia mayai yaliyopakwa rangi na mara nyingine sungura. Yai linaonyesha "uzazi" viumbe vingi vinaanzia kwenye yai. Pasaka ni sikukuu ya kuzaliwa upya Yesu Kristo baada ya kushinda mauti. Dini ya Kikristo inaanza upya baada ya Yesu kufufuka baada ya kukaa kaburini siku tatu. Kwahiyo hakuna Udini wala Dharau ambayo inafanywa na taasisi za Umma. Tuache "Ku Overthink" na kukuza mambo ambayo hayapo. Jifunze zaidi historia ya dini yako kabla ya kufadhaika na kulaumu watu wengine.
 
Jamani ee dini za watu hizi sie tufate tu wanavyotupeleka
Natamani na sisi tuanzishe siku ya kumbukizi ya babu zetu akina Mwanamarundi,mabandiko yarembwe kwa michoro ya nyoka,bundi,fisi,mikuki,vibuyu vyenye shanga,nk....
Ya wazungu tuwaachie wenyewe.
 
Tutatengwa,corona tu na malimao yetu na barakoa za vitenge tulisimangwa
Natamani na sisi tuanzishe siku ya kumbukizi ya babu zetu akina Mwanamarundi,mabandiko yarembwe kwa michoro ya nyoka,bundi,fisi,mikuki,vibuyu vyenye shanga,nk....
Ya wazungu tuwaachie wenyewe.
 
Picha gani sasa ingewekwa? Mbona miaka yote huwa zinawekwa hizo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…