Salamu za pasaka kutoka katika taasisi za Serikali zinasikitisha

Salamu za pasaka kutoka katika taasisi za Serikali zinasikitisha

Mtoa mada wewe ni mkiristo wa mchongo na dini yako kumbe hujaisoma.mbona miaka yote wanaweka hayo mayai na sungura pia?? Ipo hivi miaka ya nyuma ya upagani kuna mfalme jina nimelisahau alikuwa na desturi ya kumuadhimisha mungu wa uzazi hivyo alitumia mayai kama ishara ya uzazi huo .lakin ukiristu ulipoingia hyo ya mungu wa uzazi ikawa modified na kuwekwa jambo lingine la kuashiria kuzaliwa upya kwa kristu na yai ndo ikawa ishara hiyo..soma baadhi ya comment wadau wamekujibu
 
Dini zilizoletwa na mabeberu hawawezi kukwepa mambo yanayoendana na sherehe kama utamaduni wao!
 
Wangeweka msalaba, maana msalaba ni alalama ya ukombozi kwa wanadamu, Yesu alisulubiwa hapo akashushwa akazikwa kaburini na siku ya tatu akafufuka. Sasa hayo mayai ya nini ikiwa tu si alama ya tukio kama hili?
Mayai hutumika kwenye sherehe ipi?
 
Wangeweka msalaba, maana msalaba ni alalama ya ukombozi kwa wanadamu, Yesu alisulubiwa hapo akashushwa akazikwa kaburini na siku ya tatu akafufuka. Sasa hayo mayai ya nini ikiwa tu si alama ya tukio kama hili?
Kwani msalaba si upo tu siku zote sasa utakuwaje alama ya pasaka?
 
Hata unge disign wewe ungekula mkwanja wa maana!

Ova
Hizi taasisi kuna vitengo vya mahusiano pamoja na IT ndo Huwa wanadesign vitu hivo na haina mahusiano na madai ya watu maana nina uzoefu na hivo vitu
 
Nimeona taasisi nyingi za umma zimetuma salamu za pasaka zikiambatana na picha za mayai yenye rangi mbalimbali.

I mean, what the f*ck is that? Kwa wakristo pasaka ni sherehe ya kufufuka kwa mwokozi wetu Yesu Kristo, mayai yanatoka wapi?

Au ndio dharau kwakua awamu hii ni wa upande ule??

I'm very disappointed with this, hizi habari za Santa na Easter eggs waachieni mabepari walio monetize sherehe za kikristo.

Kama hamuwezi kuweka picha zenye uhusiano na sherehe yenyewe ni bora mngeacha tu.

View attachment 2190638
View attachment 2190639
View attachment 2190640
View attachment 2190641
Serikali inaingia kwenye kuhamasisha udhalilishaji wa kidini.

Kwa mfano watokee wahuni waanze kuihusisha Maulid ya Mtume na alama zisizoendana na dhima ya sherehe itakuwaje?
 
images (23).jpeg
 
Pasaka ni siku ya kufufuka Yesu. Anything in that theme na sio mayai.
Roho wa Bwana akukomboe kutoka vifungo vya shetani.

Pasaka ni siku ya ukombozi maana Yesu alituamrisha tuishike siku ya Pasaka na alifufuka siku ya Tatu ambapo tumeibadilisha sisi kuwa ndo Pasaka.

Pasaka ipo tangu enzi za Musa alipowatoa Waisrael Misri.

Usiku ule waliochinja mwanakondoo na kumla ndiyo kumbukumbu ambayo Yesu alifanya kwenye karamu ya mwisho na akasema tumkumbuke hivyo.
 
Wakristo wa mapema, walitambua nguvu ya yai kama ishara ya maisha mapya, waliunganisha mayai na maisha mapya yaliyopatikana katika Ufufuo wa Yesu Kristo wakati wa Pasaka.

Mayai ni ishara kamili ya Pasaka, na ishara ya maisha mapya katika Kristo. Fikiria mstari ufuatao maarufu wa Mtakatifu Paulo, “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; tazama, kila kitu kimekuwa kipya!" ( 2 Wakorintho 5:17 ).

Zaidi ya hayo, yai ni kielelezo cha Ufufuo wenyewe kifaranga akitoka kwenye ganda lake anawakilisha Yesu akitoka kaburini mwake siku ya Pasaka.

Copy & paste
Naomba mstari wa Neno la Mungu kuthibitisha hili
 
Back
Top Bottom