GE2025 Samia aahidi kununua matrekta milioni 10 akiingia madarakani kwa awamu ya pili

GE2025 Samia aahidi kununua matrekta milioni 10 akiingia madarakani kwa awamu ya pili

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Si ananunue sasa hivi? Kwani katoka madarakani? Pesa hiyo haitoshi kujenga viwanda vya matrekta kadhaa?

Shida itakua parking ujue...
trekta haendi kituo cha mafuta ndugu tuna mapori mengi sana nchi hii

mama anakwenda kuyatifua yote na kuya jaza mazao ya biashara na nafaka nafikiri ni wakati sasa watanzania kukaa makao wa kula
 
trekta haendi kituo cha mafuta ndugu tuna mapori mengi sana nchi hii

mama anakwenda kuyatifua yote na kuya jaza mazao ya biashara na nafaka nafikiri ni wakati sasa watanzania kukaa makao wa kula
Wakati dunia nzima huwa haizalishi matrekta milion 10,yanayozalishwa milion 4
 
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo kwa kuhakikisha serikali inanunua matrekta milioni 10 pamoja na zana nyingine za kisasa ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo.

Akizungumza leo, Agosti 31, 2025, mbele ya maelfu ya wananchi wilayani Chemba, mkoa wa Dodoma, Dkt. Samia amesema mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi, wenye lengo la kumrahisishia mkulima upatikanaji wa huduma bora za kilimo na kuongeza tija katika uzalishaji.

Kwa mujibu wake, serikali itahakikisha wakulima wanalimiwa kwa gharama nafuu zaidi kuliko sekta binafsi. “Kwa ekari moja, baadhi ya watu binafsi wanatoza hadi shilingi 80,000, na baada ya serikali kuanzisha vituo vya zana gharama zimeanza kushuka hadi shilingi 40,000. Lakini kwa bei yoyote sekta binafsi itakayowatoza wakulima, serikali itatoza nusu ya bei hiyo,” amesisitiza.View attachment 3460410
Kwani mtu akisema "tractor" ni lazima imaanishe matractor makubwa?
 
1756790261475.jpg
 
Back
Top Bottom