Tanzania ni nchi huru, sovereign state, Amiri jeshi kaongea kaonesha mwelekeo, sasa ni wakati wa sisi wenye kulitakia mema taifa letu kutembea kifua mbele.
Jana Kitima kajitutumua kupambana na Amiri jeshi wa Tanzania. KItima wewe ni Katibu tu wa TEC baada ya miaka mitatu hutakuwepo kwenye nafasi hiyo. Jaribio lako la kuandaa na kuratibu mapinduzi ya nchi hii yalikwamba, sasa ni wakati wa kukinywea kikombe. Umesema upo na watu kila kona, na serikali ipo na watu kila kona.
Brother huwezi ukashindana na serikali ukashinda. Serikali ipo na vyombo vya ulinzi na usalama wewe unatembea tu na biblia na msalaba mkubwa shingoni. Waliokushauri walikudanganya. Na jana uliingizwe kwenye mkenge ili uyaongee yako ya moyoni watu wayajuea.
Watu wote waliokuwa karibu na wewe sasa watakugeuka.
Kwa hotuba hii ya leo, kila kitu kimeisha. Ukitoka uanze tena kupambana na Serikali, kaka utakuwa unashida kichwani. Kaka yangu pambana na kazi yako ya kuwapeleka mbinguni wakatoliki. Wewe kazi yako ni ya katoliki siyo waumini wa dini na madhehebu mengine.
Huu ni ushauri tu nakupatia kaka, unatakiwa uchutame uende hata kwa kificho ukamuombe msamaha Amiri Jeshi mkuu.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Mimi binafsi namjua Padri Kitima, tumekaa naye mara nyingi sana kwenye vikao vya hapa na pale; pale makao makuu a TEC. Kuna mgahawa na viti hapo, tumekaa mara nyingi sana na Padri Kitima tukijadili na kupanga mambo mengi. Nakushauri ndugu yangu chutama utazeeka vizuri. Tunajua asilimia kubwa ya ndugu zako wote walishakufa, amebaki mmoja unayempenda sana.
Kaka Kitima badilika rudi uwe katika ubora wako. Baadae utaanzisha kikundi cha uasi. Sijui hata kama unajua kutumia silaha, sijui hata kama unaweza kupiga push up hata mbili.
Jitafakari Kaka