Sanamu la Magufuli na ukarabati wa kumbi za kisasa kujengwa kwa Tsh milioni 420 viwanja vya Sabasaba

Mwigulu amesisitiza makampuni ya simu yaanze kututoza pesa zaidi ili wapate kodi kumbe matumizi ya kodi zetu ndiyo haya kujenga sanamu ya kuchonga.
Ndio...na kwenye noti mojawapo wanamchi watafanya petition awepo....
 
Nashauri sanamu hilo likijengwa usiende sabasaba maana utaogopa
 
Lazima watu wapige , bro wangu kapewa tenda ya kusanifu mchoro , amekula mil 30 akanikatia mil 1.5 ..... Nasema hviiii hii sanamu ijengweeeee ma-mae
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Tunalo tatizo la elimu nchini, hatuna madawati ya kutosha, hatuna waalimu wa kutosha, hatuna vitendea kazi ikiwemo vitabu then yupo mtu amekaa wizarani huko amesoma sanaa na utamaduni anawaza kuidhinisha M420 kwa ajili ya sanamu kweli...
Vikaragosi kwa hela zote hizo? Halafu unakuta sanamu lenyewe linakuwa na sura ya Steveni Wasira halafu unaambiwa eti ni la hayati baba wa Taifa.
 
Tuongeze tax base tulipe kodi.....ndio solution sio katiba kwa sasa....Mama upige mwingi sana katiba after 2025....
Tulipebkodi ili wachache wazitumie kwa manufaa yao binafsi kama hao wanaojijengea masanamu. Wameona mahekalu hayatoshi sasa wameamua kujifanyizia masanamu
 
Hivi ajira mnayo taka (kupiga kelele) ni ipi? Maana hapa, atakaye chora hiyo sanamu, atakayefinyanga, kuchomelea, kupiga rangi, - kukarabati kumbi nk. Zote hizo ni ajira! Au nyinyi ajira ni ualimu tu?
Sasa ualimu wa watu unaingiaje kwenye sanamu la magufuli??
 
Mwambie huyo fundi alijengee na uzio kabisaa maana linaweza pigwa mawe hadi likadondoka,mwendazake akapata majeraha buree...
 
Matumizi mabaya ya pesa

Kuna wanafunzi wanaksa chini Hadi Leo

Kuna hospital hazina vitanda

Acheni kujikomba kwa wafu hawasikii Wala kuwaona mnajikomba Sana.

Kuna watu hawajui watakula Nini usiku huu mayatima na wasiojiweza

Hizo milioni 420 mngewasaidia Sana .

Kweli nchi maskini upuuzi hauisshi

Halafu kesho mnaenda kukopa IMF,WB kwa akina adesina mjenge barabara wakati mnapoteza hela kwa Mambo ya kifala sana .

Yes ufala
 
Kuna mtu kakuwahi tayari anapiga hela. Uko sloo usipoteze pesa...kamalisie mahari..
Haha washtue mataga wenzako mchangamkie deal hiyo nimewapa.

Tengenezeni na rozari za mwendazake muuze, mataga wapo wengi mtapiga pesa.
 
Believe this, you'll believe anything.
Na wakishalijenga siendi sabasaba tena
 
Hilo sanamu wangechangisha kwa watu nafikiri ingepatika
Mbona Will na Harry walichangisha na sasa limekamilika na kulisimika
Pamoja na kumuenzi mama yao hata thamani hawajasema imegharimu kiasi gani yaani kama siri vile, ila watu wabishi wanataka kujua

Imagine zingekuwa fedha za Umma
Halafu sisi tunajisifia kabisa na kutangaza gharama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…