Sanamu la Magufuli na ukarabati wa kumbi za kisasa kujengwa kwa Tsh milioni 420 viwanja vya Sabasaba

Sanamu la Magufuli na ukarabati wa kumbi za kisasa kujengwa kwa Tsh milioni 420 viwanja vya Sabasaba

Hata kina Gaddafi walijenga masanamu yao kwa gharama ila yaliishia kuvunjwa tena kwa fedheha kubwa tu.
Bwashee hiyo milioni 420 ni fedha ya V8 moja tu!

Sasa jiulize selikali ina 420 ngapi zinatembea barabarani?

Hata hivyo hako kahela ni kadogo sana!

Tuacheni wivu. Magufuli kafanya mambo mengi sana zaidi ya hako ka milioni 420.
 
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imesaini hati ya makubaliano ya jumla ya shilingi milioni 420 ya ujenzi wa sanamu la Hayati John Pombe Magafuli, na ukarabati wa kumbi kubwa za kisasa kwenye maonyesho ya sabasaba ya 45.

Mkurugenzi wa TanTrade Rutageruka Sabi amesema kuwa, ujenzi wa sanamu hilo unalenga kuenzi kumbukumbu, jitihada na mchango wa Hayati Dkt Magufuli katika kuinua uchumi.

Duu!!!!🙄🙄
 
Sijaelewa bado,Sanamu ya nani inajengwa?inajengwa wapi na nani kasema hayo?
 
Tunatumia milioni 420 kulijenga,billion 40 kulilinda halafu baada ya miaka 10 anaingia Lowassa madarakani anatumia bilioni 1.5 kulibomoa;hii wachumi wanaita hasara plus
 
Kwa kweli bado una akili ya kitumwa. Hakuna kiongozi mzalendo kwa Libya kama Gaddafi. Uliza hali ya Libya kabla na baada ya Gaddafi kuuawa bila kusahau kabla ya kuchukua nchi View attachment 1842514

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
acha uwaki arifu huyo Gadafi wa propaganda ndio alikua hivyo ila kiuhalisia hajawahi kua hivyo tatizo waarabu weusi mnalishwa Sana propaganda aisee huyu mpuuzi alivuna alichopanda unajua kwanini wa Libya walimsaliti?

Nilikutana na wazee wa Libya wawili nilivyowaambia jamaa alikua shujaa walitamani kunikata makonzi wanasema huyo jamaa alikua mbaguzi Sana hata huko Libya Kuna makabila alikua hawajali
watu wake ndio walienjoy keki
Ikafika kipindi wakaona Bora wakose wote tu

Halafu naona unajisahaulisha pale alipotuma wanajeshi na vifaa vita kumsaidia Idd Amin Dada atutandike vizuri
Hujapata machungu Kama ya ndugu zetu kule Kagera halafu Leo uje unambie alikua shujaa
What the hell!
 
Mimi naishauri Serikali ijenge pia kieneo hapo hapo jirani cha watu wenye wivu na wasiompenda Hayati JPM cha kujinyonga, ili hao machadema wakifika hapo hasira zimewafura, basi wasipate tabu, wanajitundika tu!!
 
si tulikibaliana sisi bado ni watu wa kutawaliwa tena, na soon mabeberu watakuja kututawala..ama nasema uongo ndugu zangu???
 
Lazima watu wapige , bro wangu kapewa tenda ya kusanifu mchoro , amekula mil 30 akanikatia mil 1.5 ..... Nasema hviiii hii sanamu ijengweeeee ma-mae
Mkuu rusha hata vocha, wewe naona umeonja matunda ya uhuru kidogo
 
This is ridiculous 😲😲,kwani Hili limepitishwa wap?tupe source ya habari yako mkuu😬😬
 
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imesaini hati ya makubaliano ya jumla ya shilingi milioni 420 ya ujenzi wa sanamu la Hayati John Pombe Magafuli, na ukarabati wa kumbi kubwa za kisasa kwenye maonyesho ya sabasaba ya 45.

Mkurugenzi wa TanTrade Rutageruka Sabi amesema kuwa, ujenzi wa sanamu hilo unalenga kuenzi kumbukumbu, jitihada na mchango wa Hayati Dkt Magufuli katika kuinua uchumi.

=====

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeingia makubaliano maalum na Benki ya NBC yanayohusisha ufadhili wa benki hiyo katika ujenzi na ukarabati wa kumbi kubwa za kisasa kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ‘Sabasaba’ sambamba na ujenzi wa sanamu ya Rais wa Awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli.

Wakizungumza wakati wa hafla fupi ya kusaini hati ya makubaliano (MoU) yenye jumla ya thamani ya Tsh mil 420 jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Balozi Mteule Edwin Rutageruka pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi walisema hatua hiyo inalenga kuleta mapinduzi makubwa kwenye Maonesho hayo yanayoendelea jijini humo huku yakivutia maelfu ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi.

Balozi Mteule Rutagaruka alisema mkataba huo unahusisha kipindi cha miaka mitatu huku akitaja maeneo yatayaoguswa na ufadhili wa benki hiyo kuwa ni pamoja na ukarabati mkubwa wa ukumbi unaofahamika kwa jina ‘Sabasaba’ wenye ukubwa wa mita za mraba 1600 ili uweze kuwa na hadhi ya juu zaidi si tu katika maonesho hayo bali pia katika wilaya yote ya Temeke.



“Kwa jitihada hizi za Benki ya NBC, kwasasa ukumbi huu ambao pia unatumika kama banda la maonesho ndio linalovutia zaidi washiriki wa kimataifa na limebeba hadhi hiyo ya kimataifa na ndipo yanapofanyika maonesho ya madini. Zaidi pia linatumika kamba kumbi ya mikutano ya kisiasa na shughuli za kijamii zikiwemo harusi,’’ Balozi Mteule Rutagaruka

Alitaja kumbi nyingine zitakazohusishwa na ufadhili huo kuwa ni pamoja na ukumbi wa Mikutano wa Rashid Mfaume Kawawa unaofanyiwa ukarabati mkubwa sambamba na ukarabati wa banda la bidhaa za viwanda vya Tanzania ambao utakarabatiwa katika hatua ya pili ya utekelezaji wa makubaliano hayo.
View attachment 1842533
“Haya yote yanadhihirisha namna benki ya NBC inavyoshiriki katika kuchochea mazingira bora ya ufanyaji biashara,’’ alisema Balozi Mteule Rutagaruka huku akitolea mfano wa uwepo wa Kliniki ya biashara inayofadhiliwa na benki katika maonesho hayo ikihusisha uwepo wa taasisi na mamlaka mbalimbali za kibiashara ikiwemo Tantrade, Shirika la Viwango nchini(TBS), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Kwa upande wake Sabi alisema ni heshima kubwa kwa benki hiyo kuingia katika ushirikiano huo kwa kuwa utatoa fursa kwao kufanikisha adhima ya msingi ya kuendelea kuwahudumia wadau wake muhimu wakiwemo wafanyabiashara wanaoshiriki maonesho hayo.
View attachment 1842534
“NBC tumekuwa na utamaduni wa kuhakikisha kwamba ushirikiano wetu na wadau wetu haushii kwenye viunga vya majengo yetu au huduma tunazotoa kwao bali pia tumekuwa tukihakikisha kwamba tunakuwa nao bega kwa bega katika kurahisisha shughuli zao ikiwemo kuona kwamba wanafanya shughuli zao katika mazingira bora na ndio sababu tunakarabati hadi maeneo ya wao kufanya maonesho ya biashara zao huku pia tukiwasogezea huduma zetu za kifedha,’’ Sabi

Kuhusu ujenzi wa Sanamu ya Rais wa Awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli Sabi alisema unalenga kukumbuka jitihada na mchango wake katika kuinua uchumi wa viwanda nchini ambao ni kichocheo kikubwa cha biashara na ndio msingi wa maonesho hayo.
Totally hopeless
 
Matumizi mabaya ya fedha ya uma, Hiyo pesa ingelipa vijana wangapi walio kwenye ajira, Tan trade cjuh mmewaza nn?
 
Back
Top Bottom