Sanamu la Magufuli na ukarabati wa kumbi za kisasa kujengwa kwa Tsh milioni 420 viwanja vya Sabasaba

Sawa sana na wenye chuki binafsi shauri zao! Hiyo ni kumbukumbu nzuri kwa nchi yetu na kwa vizazi vijavyo. Kila la heri.
Kuna nchi niliona masanamu yaliyothaminiwa kwa miaka mingi yakipondwapondwa na watu wenye hasira. Wangetengeneza kitu chenye matumizi kwa jamii wangemkumbuka vizuri zaidi.
 

Katiba ipya itawakataza NBC kufadhili ujenzi wa sanamu?
 
Sabasaba’ sambamba na ujenzi wa sanamu ya Rais wa Awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli.
Sijui Hayati Edward Moringe Sokoine aliwakosea nini, picha ya pale Dakawa haifanani naye, uwanja hautunzwi na wao wanapita pale kila siku
 
Sio kwamba CCM wanapenda kuchonga sanamu hiyo,ni upigaji yaani ulaji tu.Huyo Magu aliondoa au alifuta sherehe za taifa ili pesa iliotengwa itumike kwa shughuli za maendeleo
Lakni mbna maendeleo hatukuyaona 😃 nafkri kila mmoja alikuwa na style yake ya upigaji
 
Duh,ubongo wetu Kuna mahala umeoza!!!kwann hiyo pesa tusinunue hata madawati kwa baadhi ya shule zenye uhaba?au kwanini tusiongeze na tujenge hata kilomita moja tu ya kalami ndani ya mji wa Mwakaleli?au kwanini pesa hiyo tusiongezee ili tujenge jengo la abiria la maana pale SIA(SONGWE INTERNATIONAL AIRPORT)?
Mnakatisha tamaa Sana!!!!
 
wanafki hawa, ndo juzi walisema sasa pesa zimeongezeka mambo yanaenda fresh, mbona wasijenge na la mkapa
 
Mkuu iyo ndo CCM , kwao kushughulika na vitu vyepesi ni jadi yao
 
Sasa hizo ni mishahara ya vijana wangapi kama wangepunguza idadi ya wahanga wa ajira?

Kwa uzoefu wa JPM kubadili matumizi ya fedha, angekua hai hizi angezibadilisha matumizi..! Haiwezekani!
Hivi ajira mnayo taka (kupiga kelele) ni ipi? Maana hapa, atakaye chora hiyo sanamu, atakayefinyanga, kuchomelea, kupiga rangi, - kukarabati kumbi nk. Zote hizo ni ajira! Au nyinyi ajira ni ualimu tu?
 
Hizi pesa ni za kodi zetu au znatoka mfukoni kwao?HUYO WANAOMJENGEA NINA UHAKIKA HUKO ALIKO ANALIPINGA HILI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…