Sanamu la Magufuli na ukarabati wa kumbi za kisasa kujengwa kwa Tsh milioni 420 viwanja vya Sabasaba

Sanamu la Magufuli na ukarabati wa kumbi za kisasa kujengwa kwa Tsh milioni 420 viwanja vya Sabasaba

Sawa sana na wenye chuki binafsi shauri zao! Hiyo ni kumbukumbu nzuri kwa nchi yetu na kwa vizazi vijavyo. Kila la heri.
Kuna nchi niliona masanamu yaliyothaminiwa kwa miaka mingi yakipondwapondwa na watu wenye hasira. Wangetengeneza kitu chenye matumizi kwa jamii wangemkumbuka vizuri zaidi.
 
Ni matumizi mabovu ya pesa za wananchi.

Haya ndiyo mambo ambayo Samia anasema tusubiri afanye kabla ya kutupa katiba mpya

mambo ya ajabu sana!
Mkapa kajeng mifumo ya nchi hii na hatujawahi kumjengea Sanamu itakuwa huyo kiongozi dhalimu aliyekuwa muonevu kupitiliza?

Hapo tayari kuna upigaji wa watu wameshanusa fursa

Ndio maana tunasema tunataka katiba MPYA!!

Magufuli katusababishia hasara kubwa ktk nchi hii, kaiba sana, kanyanyasa sana raia wa nchi hii na ujinga mwingine mwingi kafanya,

Kwa heshima gani hasa hadi pesa ya wananchi itumie kumjengea sanamu? Ndio maana waTanzania wengi hawalipi kodi, kodi tunalipa ila inaelekezwa kwa mambo ya kipuuzi na ya kishamba kama haya!?

Huu ujinga upo Tanzania tuu na ni sababu ya hii katiba butu na ya kikoloni tulio nayo.

Ni mtu mjinga tu anaweza kubeza mchakato wa katiba mpya.
Katiba ipya itawakataza NBC kufadhili ujenzi wa sanamu?
 
Sabasaba’ sambamba na ujenzi wa sanamu ya Rais wa Awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli.
Sijui Hayati Edward Moringe Sokoine aliwakosea nini, picha ya pale Dakawa haifanani naye, uwanja hautunzwi na wao wanapita pale kila siku
 
Sio kwamba CCM wanapenda kuchonga sanamu hiyo,ni upigaji yaani ulaji tu.Huyo Magu aliondoa au alifuta sherehe za taifa ili pesa iliotengwa itumike kwa shughuli za maendeleo
Lakni mbna maendeleo hatukuyaona 😃 nafkri kila mmoja alikuwa na style yake ya upigaji
 
Duh,ubongo wetu Kuna mahala umeoza!!!kwann hiyo pesa tusinunue hata madawati kwa baadhi ya shule zenye uhaba?au kwanini tusiongeze na tujenge hata kilomita moja tu ya kalami ndani ya mji wa Mwakaleli?au kwanini pesa hiyo tusiongezee ili tujenge jengo la abiria la maana pale SIA(SONGWE INTERNATIONAL AIRPORT)?
Mnakatisha tamaa Sana!!!!
 
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imesaini hati ya makubaliano ya jumla ya shilingi milioni 420 ya ujenzi wa sanamu la Hayati John Pombe Magafuli, na ukarabati wa kumbi kubwa za kisasa kwenye maonyesho ya sabasaba ya 45.

Mkurugenzi wa TanTrade Rutageruka Sabi amesema kuwa, ujenzi wa sanamu hilo unalenga kuenzi kumbukumbu, jitihada na mchango wa Hayati Dkt Magufuli katika kuinua uchumi.

=====

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeingia makubaliano maalum na Benki ya NBC yanayohusisha ufadhili wa benki hiyo katika ujenzi na ukarabati wa kumbi kubwa za kisasa kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ‘Sabasaba’ sambamba na ujenzi wa sanamu ya Rais wa Awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli.

Wakizungumza wakati wa hafla fupi ya kusaini hati ya makubaliano (MoU) yenye jumla ya thamani ya Tsh mil 420 jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Balozi Mteule Edwin Rutageruka pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi walisema hatua hiyo inalenga kuleta mapinduzi makubwa kwenye Maonesho hayo yanayoendelea jijini humo huku yakivutia maelfu ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi.

Balozi Mteule Rutagaruka alisema mkataba huo unahusisha kipindi cha miaka mitatu huku akitaja maeneo yatayaoguswa na ufadhili wa benki hiyo kuwa ni pamoja na ukarabati mkubwa wa ukumbi unaofahamika kwa jina ‘Sabasaba’ wenye ukubwa wa mita za mraba 1600 ili uweze kuwa na hadhi ya juu zaidi si tu katika maonesho hayo bali pia katika wilaya yote ya Temeke.



“Kwa jitihada hizi za Benki ya NBC, kwasasa ukumbi huu ambao pia unatumika kama banda la maonesho ndio linalovutia zaidi washiriki wa kimataifa na limebeba hadhi hiyo ya kimataifa na ndipo yanapofanyika maonesho ya madini. Zaidi pia linatumika kamba kumbi ya mikutano ya kisiasa na shughuli za kijamii zikiwemo harusi,’’ Balozi Mteule Rutagaruka

Alitaja kumbi nyingine zitakazohusishwa na ufadhili huo kuwa ni pamoja na ukumbi wa Mikutano wa Rashid Mfaume Kawawa unaofanyiwa ukarabati mkubwa sambamba na ukarabati wa banda la bidhaa za viwanda vya Tanzania ambao utakarabatiwa katika hatua ya pili ya utekelezaji wa makubaliano hayo.
View attachment 1842533
“Haya yote yanadhihirisha namna benki ya NBC inavyoshiriki katika kuchochea mazingira bora ya ufanyaji biashara,’’ alisema Balozi Mteule Rutagaruka huku akitolea mfano wa uwepo wa Kliniki ya biashara inayofadhiliwa na benki katika maonesho hayo ikihusisha uwepo wa taasisi na mamlaka mbalimbali za kibiashara ikiwemo Tantrade, Shirika la Viwango nchini(TBS), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Kwa upande wake Sabi alisema ni heshima kubwa kwa benki hiyo kuingia katika ushirikiano huo kwa kuwa utatoa fursa kwao kufanikisha adhima ya msingi ya kuendelea kuwahudumia wadau wake muhimu wakiwemo wafanyabiashara wanaoshiriki maonesho hayo.
View attachment 1842534
“NBC tumekuwa na utamaduni wa kuhakikisha kwamba ushirikiano wetu na wadau wetu haushii kwenye viunga vya majengo yetu au huduma tunazotoa kwao bali pia tumekuwa tukihakikisha kwamba tunakuwa nao bega kwa bega katika kurahisisha shughuli zao ikiwemo kuona kwamba wanafanya shughuli zao katika mazingira bora na ndio sababu tunakarabati hadi maeneo ya wao kufanya maonesho ya biashara zao huku pia tukiwasogezea huduma zetu za kifedha,’’ Sabi

Kuhusu ujenzi wa Sanamu ya Rais wa Awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli Sabi alisema unalenga kukumbuka jitihada na mchango wake katika kuinua uchumi wa viwanda nchini ambao ni kichocheo kikubwa cha biashara na ndio msingi wa maonesho hayo.
wanafki hawa, ndo juzi walisema sasa pesa zimeongezeka mambo yanaenda fresh, mbona wasijenge na la mkapa
 
Tunalo tatizo la elimu nchini, hatuna madawati ya kutosha, hatuna waalimu wa kutosha, hatuna vitendea kazi ikiwemo vitabu then yupo mtu amekaa wizarani huko amesoma sanaa na utamaduni anawaza kuidhinisha M420 kwa ajili ya sanamu kweli.

Hii imegeuka kuwa nchi ya sanamu Kama vipaumbele vyetu kweli? Kwamba tumeingia kwenye imani za sanamu kwa mabilioni ya Kodi za wananchi? We can't be serious. Kwamba tunakatwa pesa kwenye vocha na miamala mingine ili hizo fedha zikajenga sanamu?

Kwamba Mkapa 420 milion, sijui Nani mwingine akitutoka 420Milion, Mawaziri wakuu 220 milion, makawa wa Rais tuwajengee sanamu za milioni 300, Mawaziri milioni 150, wakuu wa Mikoa milioni 100, wakuu wa Wilaya 50milion? Ni hivi ndivyo tumejipanga kuiendesha nchi?

Lakini pia hizo fedha mbona hazipo kwenye bajeti ya serikali? Unaweza ukatamani kumpiga mtu rungu la kichwa atambae kwa mambo haya yakijinga unayoyasikia kutoka kwa watu wanaolipwa fedha za umma.

Hakuna anayewaza kuhusu maskini wote wanawaza matumbo yao na Sasa wameanza kuweka na utaratibu wakuhudumiwa hata wanapotwaliwa. Shame shame shame nchi masikini kutumia fedha za umma kwa mambo ya kijinga
Mkuu iyo ndo CCM , kwao kushughulika na vitu vyepesi ni jadi yao
 
AI-L00.jpg
 
Sasa hizo ni mishahara ya vijana wangapi kama wangepunguza idadi ya wahanga wa ajira?

Kwa uzoefu wa JPM kubadili matumizi ya fedha, angekua hai hizi angezibadilisha matumizi..! Haiwezekani!
Hivi ajira mnayo taka (kupiga kelele) ni ipi? Maana hapa, atakaye chora hiyo sanamu, atakayefinyanga, kuchomelea, kupiga rangi, - kukarabati kumbi nk. Zote hizo ni ajira! Au nyinyi ajira ni ualimu tu?
 
Hizi pesa ni za kodi zetu au znatoka mfukoni kwao?HUYO WANAOMJENGEA NINA UHAKIKA HUKO ALIKO ANALIPINGA HILI
 
Back
Top Bottom