Sasa hivi kupita mkesha/sikukuu bila ngumi imekuwa kawaida sana kitu ambacho miaka hiyo ilikuwa ni Nadra mno

Ugomvi umemalizwa na kuku wa kfc πŸ˜‚ sahizi vijana wote laini laini na wanaogopa kuumia sana wanakwepa shari kwa namna yeyote ile.
Ukweli kijana wa miaka19 anapigwa halafu anaenda kusema Kwa mama yake na mama yake analibeba kama kapigwa yeye.

Enzi zetu ukiwa huko ukija kusema unaulizwa mbona wewe ulikuwa umewaangalia huna mikono? Unapigwa TenaπŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mtoa mada umeongea ukweli sikuhizi watu wameacha kugombana physically nadhani pia kuelimika kumechangia pia kuzingatia sheria za nchi... zamani ilikuwa shida unakuta mnacheza mpira ukipigwa rafu tu unaacha kucheza unamfuata unamwambia tutoke nje ya uwanja tukazichape kidogo tusiwaharibie wanaotaka kuendelea kucheza..mkienda huko mzichapa ee ukishindwa unanyoosha mikono juu halafu mnaludi kucheza mpira kesho mnakuwa marafiki wa kweli..wakati mwingine ugomvi unawapatanisha.
 
Sikupingi mkuu sio Bure. Wee ngumu zinapigwa padre akiwa anabatizwa Watoto na ugomvi hataturuki yaani
 
Haya mambo yalitufanya tuwe imara sana yaani huwezi nipiga mkwara Kwa namna yoyote Ile. Sidhani kama Kuna mtu alikuwa hajawahi kupigwa dingi yetu alikuwa mpole lakini Kuna siku uvumilivu ulimshinda akatembeza mkono buchani kisa kapimiwa nyama yenye mifupa sana.

Daah maisha hayo kwetu sisi tuliona mwanaume lazima uwe mbabe mbabe
 
Yote ni kweli mkuu lakini No5 umemaliza Kila kitu. Ujue mwanaume akiwa aggressive hawazi habar za police au jera kwanza utapigika halafu hayo mengine yatakuja badae
 
Hatari sana
 
Hatari sana
VIJANA WA KILEO HOVYO KABISA UNAKUTA KIJANA KAJAZIAJAZIA MWENYEWE MTANASHATI ANA BONGE LA KIFUA NA MUSTACHI WA NGUVU LAKINI AKITOKEA NYOKA TU HAPO AU PAKA ALIYEPAGAWA ANAKULA KONA.

HUWA NASHANGAA SANA HATA MAJESHI YETU SIJUI WANAPATA WAPI NGUVUKAZI KWA SASA MAANA VIJANA HAWANA UJASIRI KABISA. NDIO MAANA SI AJABU KUSIKIA KIJANA SHABABI WA KIUME AMELAMBWA MAKOFI YA USO NA BINTI KIGORI MKUNANAZI ALIYEMTOLEA MAHALI.
 
umesema vizuri sana kiongozi ongezea saizi kuna utawala wa sheria. zamani ilikuwa ngumu kupata haki kwenye hivi vyombo vya sheria sio ajabu unamuweka mtu ndani asbh ikifika jioni mnagongana na muhalifu wako baa ya jirani anagonga gambe ndio maana watu walijilinda wenyewe kwa kujichukulia sheria mkononi.
 
Hata Waalimu walikuwa wanazipiga shuleni tunaona Kwa macho yetu na muda mwingine kama mwalimu mnamkubali na mwingine hakubaliki atakibizwa mnoo asipojifungia ofisini basi atakimbia mnoo kwenda kwakwe.
nimewahi shuhudia mwanafunzi akimshushia kipondo ticha siku ya assembly. kisa kilitokea baada ya mwanafunzi wa f.6 kukataa kuadhibiwa sasa yule ticha akawa amekomaa anataka amwadhibu jamaa. weee moto uliwaka sio wa hapaπŸ”₯πŸ”₯. ticha alikula mbata za kutosha za yule f.6. sasa madogo wa low classes kuona mwalimu anakula mambata wakaingia nao kumshushia kipondo cha maana yule ticha maana walikuwa hawampendi.
 
Mkuu kwa niliyoyaona si haba acha niyasimulie asee.Waalimu wa sasahivi wanaraha sana asee kuna siku tulikuwa tunaenda kwenye michezo tumepanda kwenye fuso humohumo zikaanza mwalimu na mwanafunzi dereva nae wala hasikii wanafunzi wanashangilia hata huwezi elewa ...dereva anajua ni vibe tu kumbe ngumi zinapigwa sio powa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…