Sasa hivi kupita mkesha/sikukuu bila ngumi imekuwa kawaida sana kitu ambacho miaka hiyo ilikuwa ni Nadra mno

Sasa hivi kupita mkesha/sikukuu bila ngumi imekuwa kawaida sana kitu ambacho miaka hiyo ilikuwa ni Nadra mno

Ugomvi umemalizwa na kuku wa kfc 😂 sahizi vijana wote laini laini na wanaogopa kuumia sana wanakwepa shari kwa namna yeyote ile.
Ukweli kijana wa miaka19 anapigwa halafu anaenda kusema Kwa mama yake na mama yake analibeba kama kapigwa yeye.

Enzi zetu ukiwa huko ukija kusema unaulizwa mbona wewe ulikuwa umewaangalia huna mikono? Unapigwa Tena😂😂
 
Mtoa mada umeongea ukweli sikuhizi watu wameacha kugombana physically nadhani pia kuelimika kumechangia pia kuzingatia sheria za nchi... zamani ilikuwa shida unakuta mnacheza mpira ukipigwa rafu tu unaacha kucheza unamfuata unamwambia tutoke nje ya uwanja tukazichape kidogo tusiwaharibie wanaotaka kuendelea kucheza..mkienda huko mzichapa ee ukishindwa unanyoosha mikono juu halafu mnaludi kucheza mpira kesho mnakuwa marafiki wa kweli..wakati mwingine ugomvi unawapatanisha.
 
Level ya hormones za kiume ni ndogo Sana leo !

Zamani hasa miaka ya tisini kurudi nyuma pombe nyingi zilikua na hormones za kiume kibao (testosterone)ugomvi ukawa mwingi sana kwa walevi!

Kanisa likalaani,viwanda vikaweka hormones za like kibao na wanaume tukaanza kuwa humble kama wanawake na sio kuwa agressive kama zamani!!

Nakumbuka mitaa ya Bunda pale nikiwa mdogo niliona vurugu sana kukutwa mtu kafia mtaroni ilikua kawaida sana!!
Sikupingi mkuu sio Bure. Wee ngumu zinapigwa padre akiwa anabatizwa Watoto na ugomvi hataturuki yaani
 
daah we jamaa umenikumbusha mbabe wetu legendary kaka mkubwa ahmad huyu kwanza mkwara wake anafunga kitambaa chekundu mkono wa kushoto kama kapteni wa mpira na kingine anazungusha kichwani (usongo). hapo nyie hata mje shule nzima lazma mchezee kichapo wkt huo sisi tupo nyuma yake tunamtia hasira kwa hype kibao mwamba anashusha kipondo.
Haya mambo yalitufanya tuwe imara sana yaani huwezi nipiga mkwara Kwa namna yoyote Ile. Sidhani kama Kuna mtu alikuwa hajawahi kupigwa dingi yetu alikuwa mpole lakini Kuna siku uvumilivu ulimshinda akatembeza mkono buchani kisa kapimiwa nyama yenye mifupa sana.

Daah maisha hayo kwetu sisi tuliona mwanaume lazima uwe mbabe mbabe
 
Hiki kitu hata mimi nimekuwa nikijiuliza mara kadhaa...

Kijijini kwetu kulikuwa na mnada wa kila mwezi, ilikuwa ni nadra sana. Angalau kila mwezi lazima ugomvi utokee. Ninapoongea ugomvu siyo wa kupigana ngumi tu, ugommvi wa kuchomana visu. Kiufupi ni kuwa kila mnada ilikuwa lazima mtu afe au ajeruhiwe vibaya sana...

Kwenye mikesha ya sikukuu na sikukuu zenyewe ndo usiseme, zilikuwa zinapigwa sana ngumi mitaani. Kuna mkesha mmoja pardi alizichapa na waumini kwenye kilabu cha pombe.

Wanawake walikuwa wanapigwa sana na waume zao. Ilikuwa ni kawaida kila wiki kusikia mwanamke anapiga kelele yavilio kisa kupigwa. But now nipo mkoani kwetu mwezi wa tanoo huu sijawahi kusikia mwanamke analia kwa kipigo, kweli zama zimebadilika.

Mimi nilikuwa mpole na muoga sana, lakini nilikuwa nalazimika kupigana sababu ya kuwa usipopigana unaonekana kama mtoto wa kike.

Siku hizi hizo mambo zimepungua kwa sababu

1. Ugumu wa maisha; Zamani watu walikuwa na uhakika wa chakula ndo maana walikua wanapata nguvu na mawazo ya kupigana. Siku hizi maisha magumu, mtu anakula mara moja kwa siku nguvu za kupigana anazitoa wapi?

2. Afya: Watu wa zamani walikuwa na afya sana, mnadundana ngumi kavukavu lakini fresh tu. Siku hizi unamuona mtu mzima kumbe ana magonjwa kibao. Ukimpiga ngumi moja kazima. Unapata kesi ya mauaji

3. Polisi kuongezeka: zamani hasa vijijini ilikuwa ni nadra sana kuona polisi. Kwa hiyo ugomvi mwingi ulikuwa unaisha kienyeji tu. Siku hizi polisi wamekuwa wengi na kama mjuavyo kuingia polisi ni bure ila kutoka ndo kipengele. Hii imesababisha watu wapunguze ukorofi...

4. Elimu na kustaarabika: Zamani ilikuwa kawaida kuona mtu anajisifia ubabe wa kupiga watu, lakini siku hizi baada ya watu kuelimika wanaona hayo ni mambo ya kijinga. Ubabe wa sasa ni kuwa na pesa nyingi...

5. Masculinity: Nadhani pia homoni za kiume zilikuwa juu sana zamani na kama tujuavyo uanaume unaendana na kuwa aggresive. Lakini siku hizi wanaume tumekuwa siyo aggresive kama zamani. Unakuta mwanaume yupo tiktok yupo busy anasema 'tap tap screen guy, please send me gifts' Huyu ukimwambia apigane anaona kama unampa laana...​
Yote ni kweli mkuu lakini No5 umemaliza Kila kitu. Ujue mwanaume akiwa aggressive hawazi habar za police au jera kwanza utapigika halafu hayo mengine yatakuja badae
 
Enzi hizo magomeni mitaa ya day break uwanja wa zamaleki kukiwa na mechi ngumi kupigwa ni kawaida hadi ndondo zilikuwa ni ngumi tu..pia ya kurushiana mawe watoto wa mwananyamala vs watoto wa magomeni ilikuwa ni hatari..nimemkumbuka mwenzetu mmoja(Abubakari kwa sasa marehemu) alikuwa na ngumu hatari ila kwa bahati alikuwa anasumbuliwa na kifafa..
Hatari sana
 
Hatari sana
VIJANA WA KILEO HOVYO KABISA UNAKUTA KIJANA KAJAZIAJAZIA MWENYEWE MTANASHATI ANA BONGE LA KIFUA NA MUSTACHI WA NGUVU LAKINI AKITOKEA NYOKA TU HAPO AU PAKA ALIYEPAGAWA ANAKULA KONA.

HUWA NASHANGAA SANA HATA MAJESHI YETU SIJUI WANAPATA WAPI NGUVUKAZI KWA SASA MAANA VIJANA HAWANA UJASIRI KABISA. NDIO MAANA SI AJABU KUSIKIA KIJANA SHABABI WA KIUME AMELAMBWA MAKOFI YA USO NA BINTI KIGORI MKUNANAZI ALIYEMTOLEA MAHALI.
 
Hiki kitu hata mimi nimekuwa nikijiuliza mara kadhaa...

Kijijini kwetu kulikuwa na mnada wa kila mwezi, ilikuwa ni nadra sana. Angalau kila mwezi lazima ugomvi utokee. Ninapoongea ugomvu siyo wa kupigana ngumi tu, ugommvi wa kuchomana visu. Kiufupi ni kuwa kila mnada ilikuwa lazima mtu afe au ajeruhiwe vibaya sana...

Kwenye mikesha ya sikukuu na sikukuu zenyewe ndo usiseme, zilikuwa zinapigwa sana ngumi mitaani. Kuna mkesha mmoja pardi alizichapa na waumini kwenye kilabu cha pombe.

Wanawake walikuwa wanapigwa sana na waume zao. Ilikuwa ni kawaida kila wiki kusikia mwanamke anapiga kelele yavilio kisa kupigwa. But now nipo mkoani kwetu mwezi wa tanoo huu sijawahi kusikia mwanamke analia kwa kipigo, kweli zama zimebadilika.

Mimi nilikuwa mpole na muoga sana, lakini nilikuwa nalazimika kupigana sababu ya kuwa usipopigana unaonekana kama mtoto wa kike.

Siku hizi hizo mambo zimepungua kwa sababu

1. Ugumu wa maisha; Zamani watu walikuwa na uhakika wa chakula ndo maana walikua wanapata nguvu na mawazo ya kupigana. Siku hizi maisha magumu, mtu anakula mara moja kwa siku nguvu za kupigana anazitoa wapi?

2. Afya: Watu wa zamani walikuwa na afya sana, mnadundana ngumi kavukavu lakini fresh tu. Siku hizi unamuona mtu mzima kumbe ana magonjwa kibao. Ukimpiga ngumi moja kazima. Unapata kesi ya mauaji

3. Polisi kuongezeka: zamani hasa vijijini ilikuwa ni nadra sana kuona polisi. Kwa hiyo ugomvi mwingi ulikuwa unaisha kienyeji tu. Siku hizi polisi wamekuwa wengi na kama mjuavyo kuingia polisi ni bure ila kutoka ndo kipengele. Hii imesababisha watu wapunguze ukorofi...

4. Elimu na kustaarabika: Zamani ilikuwa kawaida kuona mtu anajisifia ubabe wa kupiga watu, lakini siku hizi baada ya watu kuelimika wanaona hayo ni mambo ya kijinga. Ubabe wa sasa ni kuwa na pesa nyingi...

5. Masculinity: Nadhani pia homoni za kiume zilikuwa juu sana zamani na kama tujuavyo uanaume unaendana na kuwa aggresive. Lakini siku hizi wanaume tumekuwa siyo aggresive kama zamani. Unakuta mwanaume yupo tiktok yupo busy anasema 'tap tap screen guy, please send me gifts' Huyu ukimwambia apigane anaona kama unampa laana...​
umesema vizuri sana kiongozi ongezea saizi kuna utawala wa sheria. zamani ilikuwa ngumu kupata haki kwenye hivi vyombo vya sheria sio ajabu unamuweka mtu ndani asbh ikifika jioni mnagongana na muhalifu wako baa ya jirani anagonga gambe ndio maana watu walijilinda wenyewe kwa kujichukulia sheria mkononi.
 
Hata Waalimu walikuwa wanazipiga shuleni tunaona Kwa macho yetu na muda mwingine kama mwalimu mnamkubali na mwingine hakubaliki atakibizwa mnoo asipojifungia ofisini basi atakimbia mnoo kwenda kwakwe.
nimewahi shuhudia mwanafunzi akimshushia kipondo ticha siku ya assembly. kisa kilitokea baada ya mwanafunzi wa f.6 kukataa kuadhibiwa sasa yule ticha akawa amekomaa anataka amwadhibu jamaa. weee moto uliwaka sio wa hapa🔥🔥. ticha alikula mbata za kutosha za yule f.6. sasa madogo wa low classes kuona mwalimu anakula mambata wakaingia nao kumshushia kipondo cha maana yule ticha maana walikuwa hawampendi.
 
Unaongelea mavarangati ya juzijuzi tu, we kumbe bado dogo uliza wakongwe wakuambie vagi za enzi zao kwenye madisko na mikesha nyie mkasome. Unaambiwa hapohapo kwenye madisko ya shuleni wahuni wa mitaani walikuwa wanakuja na kucheza na mademu zenu wa hapohapo shuleni mnanyang'anywa. Mkono ulikuwa unapigwa haswa kati ya ya raia na wanafunzi au wanafunzi kwa wanafunzi kugombea mademu wa kucheza nao disko la welcome form one/form five na lile disco la kuhitimu form four/six
Mkuu kwa niliyoyaona si haba acha niyasimulie asee.Waalimu wa sasahivi wanaraha sana asee kuna siku tulikuwa tunaenda kwenye michezo tumepanda kwenye fuso humohumo zikaanza mwalimu na mwanafunzi dereva nae wala hasikii wanafunzi wanashangilia hata huwezi elewa ...dereva anajua ni vibe tu kumbe ngumi zinapigwa sio powa.
 
unategemea huyu akitoka hapa ndo arushe ngumi huyu?
Screenshot_20250112-173537_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom