Hiki kitu hata mimi nimekuwa nikijiuliza mara kadhaa...
Kijijini kwetu kulikuwa na mnada wa kila mwezi, ilikuwa ni nadra sana. Angalau kila mwezi lazima ugomvi utokee. Ninapoongea ugomvu siyo wa kupigana ngumi tu, ugommvi wa kuchomana visu. Kiufupi ni kuwa kila mnada ilikuwa lazima mtu afe au ajeruhiwe vibaya sana...
Kwenye mikesha ya sikukuu na sikukuu zenyewe ndo usiseme, zilikuwa zinapigwa sana ngumi mitaani. Kuna mkesha mmoja pardi alizichapa na waumini kwenye kilabu cha pombe.
Wanawake walikuwa wanapigwa sana na waume zao. Ilikuwa ni kawaida kila wiki kusikia mwanamke anapiga kelele yavilio kisa kupigwa. But now nipo mkoani kwetu mwezi wa tanoo huu sijawahi kusikia mwanamke analia kwa kipigo, kweli zama zimebadilika.
Mimi nilikuwa mpole na muoga sana, lakini nilikuwa nalazimika kupigana sababu ya kuwa usipopigana unaonekana kama mtoto wa kike.
Siku hizi hizo mambo zimepungua kwa sababu
1. Ugumu wa maisha; Zamani watu walikuwa na uhakika wa chakula ndo maana walikua wanapata nguvu na mawazo ya kupigana. Siku hizi maisha magumu, mtu anakula mara moja kwa siku nguvu za kupigana anazitoa wapi?
2. Afya: Watu wa zamani walikuwa na afya sana, mnadundana ngumi kavukavu lakini fresh tu. Siku hizi unamuona mtu mzima kumbe ana magonjwa kibao. Ukimpiga ngumi moja kazima. Unapata kesi ya mauaji
3. Polisi kuongezeka: zamani hasa vijijini ilikuwa ni nadra sana kuona polisi. Kwa hiyo ugomvi mwingi ulikuwa unaisha kienyeji tu. Siku hizi polisi wamekuwa wengi na kama mjuavyo kuingia polisi ni bure ila kutoka ndo kipengele. Hii imesababisha watu wapunguze ukorofi...
4. Elimu na kustaarabika: Zamani ilikuwa kawaida kuona mtu anajisifia ubabe wa kupiga watu, lakini siku hizi baada ya watu kuelimika wanaona hayo ni mambo ya kijinga. Ubabe wa sasa ni kuwa na pesa nyingi...
5. Masculinity: Nadhani pia homoni za kiume zilikuwa juu sana zamani na kama tujuavyo uanaume unaendana na kuwa aggresive. Lakini siku hizi wanaume tumekuwa siyo aggresive kama zamani. Unakuta mwanaume yupo tiktok yupo busy anasema 'tap tap screen guy, please send me gifts' Huyu ukimwambia apigane anaona kama unampa laana...