Sasa tunaweza kukubaliana kuwa; aina ya siasa anayoifanya Rais Samia ni ya kiwango cha juu sana ambapo ni nadra sana kuiona Afrika

Sasa tunaweza kukubaliana kuwa; aina ya siasa anayoifanya Rais Samia ni ya kiwango cha juu sana ambapo ni nadra sana kuiona Afrika

Bila kusahau aliyemuweka Mbowe ndani
Sio kila kitu anafanya rais. Unapoongoza watu wengi kuna mambo mengi yanaweza kufanywa na 'other actors' bila wewe kuwatuma wanafanya wao kama wa kwa sababu tofauti tofauti.Ndio maana tunasema ni muhimu kila mtu awajibike ili tufanikiwe.
 
Mkuu JokaKuu , Mama hakufukuza mtu kwa kutofautiana mitizamo. Na yeye alieleza mtizamo wake kuhusu mikopo na hayo ndio mapambano ya hoja. Aliyekuwa spika akajikuta anajichanganya na kushindwa kusimamia hoja yake. Mwisho baada ya kuyumba yumba akaona ajiuzulu. Ukisema alifukuzwa sio kweli.

Kuhusu watu kukamatwa, jamani sio kila kitendo kinachofanyika wafanyaji wanakuwa wametumwa na Rais, au Rais anakuwa anakifurahia. mambo mengine ni mitizamo, uelewa na tabia binafsi za mfanyaji. Kumlaumu rais ni kumuonea bure. Kama angeagiza au kutoka hadharani na kuunga mkono vitu vizivyo vya kawaida, hilo lingekuwa jambo jingine.

..Raisi alitoa kauli ngumu dhidi ya Spika ndio maana akalazimika kujiuzulu.

..Ni mapema mno kumpa SSH sifa ya uvumilivu kwasababu kuna kauli amezitoa hapo katikati inaonekana ni mtu mwenye hofu na challenge za kihoja na kisiasa.

..Jambo lingine matamanio yake ya kuwa "MAMA" wa wanasiasa wenzake na Watanzania kwa ujumla.

..SSH amekula kiapo cha Uraisi, lakini anataka tumchukulie kama Mama aliyetupa nyonyo na kutusafisha tulipokuwa wachanga.

..Mwisho, Raisi wa Tanzania anasifiwa kwa kila kitu hata mambo yaliyofanywa na wasaidizi wake bila kuwa wamepewa maagizo direct kutoka kwake.

..Kwasababu Raisi hukubali sifa zote, basi ni lazima pia akubali na abebe lawama za wasaidizi wake wanapoboronga.

..Masuala ya wapinzani kukamatwa na kunyanyaswa na Polisi lawama na kilio lazima ziende mpaka kwa Raisi na Amiri Jeshi Mkuu.
 
Sio kila kitu anafanya rais. Unapoongoza watu wengi kuna mambo mengi yanaweza kufanywa na 'other actors' bila wewe kuwatuma wanafanya wao kama wa kwa sababu tofauti tofauti.Ndio maana tunasema ni muhimu kila mtu awajibike ili tufanikiwe.

..kwenye interview na Salim Kikeke, Hangaya alidai Mbowe anahusika na wako wenzake ambalo walishahukumiwa.

..kwa msingi huo inaonyesha kuwa suala la Mbowe lilikuwa na baraka zake, amekuja kuachana nalo baada mashahidi wa Jamhuri kuonekana wanasema uongo waziwazi.

..Binafsi nilitegemea Rais atawachukulia hatua za kinidhamu wote waliohusika kutunga kesi dhidi ya Mbowe. Lile ni jaribio baya sana ambalo lingeweza hata kupelekea kifungo cha maisha.
 
Mtu, kwa sasa upinzani hawana hoja yoyote ya maana zaidi ya katiba mpya ambayo iko wazi sana na tayari inafanyiwa kazi. Tunachotofautiana ni kuhusu utaratibu tu.

Kuhusu kwamba ni mstaarabu kwa sababu hajakabiliana na uchaguzi, hili au kweli. Ustaarabu ni tabia ya mtu. Vinginevyo kwa kupata madaraka tu, ingetosha kubadilika na kufanya vitu vya ajabu lakini uungwana au uhuni ni tabia ya mtu tu.

Kuhusu siasa za upinzani, unatakiwa ujue kuwa huko nako kuna wahuni wakutosha tu, kwa hiyo bila kuweka utaratibu mzuri ni tatizo lingine tena.

Imebidi nicheke sana, kwa sasa unapompamba huyu mama kuwa ni mstaarabu, ila kimsingi sio mstaarabu hivyo bali kwakuwa kipimo cha ustaarabu wake ni Magufuli, basi lazima ni aonekane malaika. Nimeona huyu mama anapokutana na jambo lililo nje ya matamanio yake anaishia kupanick.

Hapo wapinzani kuwa hawana hoja, hapa inaonyesha ww ni bendera fuata upepo, ukisikia neno linarudiwa kila mara, na ww unalibeba, hoja za wapinzani wakitaka kuzionyesha ndio hapo polisi wanatumwa kuwadhalilisha. Kwenye suala la katiba sio suala la kuweka utaratibu vizuri, bali rasimu halali ya Warioba ipo, na ilikuwa na maoni halali ya wananchi. Tuingie huko na sio kutumia kikundi cha walaji kukusanya maoni huko vichochoroni.
 
Mtu JokaKuu wakati fulani kiongozi huweza kujikuta kwenye dilemma of undesirable ends kwa sababu fulani fulani. Moja ya sababu yaweza kuwa kupewa taarifa zisizo sahihi, au makosa ambayo yalishafanyika awali.

Kwa hiyo makosa yanaweza kuwepo hapa na pale. Hatutakiwi ku concetrate kwenye makosa ambayo amma yalirekebishwa au tunaona jitihada za wazi za kuyarekebisha.
 
MkuuTindo huwa tunapima uzuri au ubaya wa mtu/kitu kwa kufanya mlinganisho, hakuna kitu ambacho ni absolute kizuri au kibaya bali ni 'relatively'.

Extreme good ni malaika, extreme bad ni shetani katikati ni mtu.

Halafu sijui kwa nini utatumia vyama vya upinzani kama standard pekee kupima uzuri na ubaya wa rais huku ukijua kuwa hao wapinzani wenyewe ni chenga kichizi.
 
Siasa safi ni kuwafanya wananchi wapate mkate wao na maisha yanayotabirika

Siasa ya kuwafanya wananchi wawe na njaa, haijawahi kupendwa na mtu hata mmoja

Labda huko juu keki inakoanzia!
Njaa ipi Mzee? Unalala na njaa? 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220526-100025.png
    Screenshot_20220526-100025.png
    137.2 KB · Views: 4
Mtu JokaKuu wakati fulani kiongozi huweza kujikuta kwenye dilemma of undesirable ends kwa sababu fulani fulani. Moja ya sababu yaweza kuwa kupewa taarifa zisizo sahihi, au makosa ambayo yalishafanyika awali.

Kwa hiyo makosa yanaweza kuwepo hapa na pale. Hatutakiwi ku concetrate kwenye makosa ambayo amma yalirekebishwa au tunaona jitihada za wazi za kuyarekebisha.

..unaweza kurekebisha makosa bila kukubali kuwa umekosea?

..kama Ssh hatakubali kuwa yeye na serikali yake walikosea ktk suala la Fam basi hatakuwa na nia ya dhati ya kurekebisha makosa yaliyofanyika.

..Na kama hakutaarifiwa na kutoa baraka zake basi alitakiwa kuwachukulia hatua za kinidhamu waliompotosha au kumshauri vibaya.
 
MkuuTindo huwa tunapima uzuri au ubaya wa mtu/kitu kwa kufanya mlinganisho, hakuna kitu ambacho ni absolute kizuri au kibaya bali ni 'relatively'.

Extreme good ni malaika, extreme bad ni shetani katikati ni mtu.

Halafu sijui kwa nini utatumia vyama vya upinzani kama standard pekee kupima uzuri na ubaya wa rais huku ukijua kuwa hao wapinzani wenyewe ni chenga kichizi.

Azizi bana unachekesha kweli, ubora una viwango/vigezo vyake bila kujali kuwa kuna ulinganifu. Mfano mrahisi mwanafunzi aliyefaulu vizuri atakuwa na marks kuanzia 80-100 bila kujali matokeo ya wengine. Ila wewe unataka kusema mwanafunzi atakuwa ana akili kwa sababu yuko juu ya wenzake, bila kujali ana marks kiasi gani. Yaani mwanafunzi akiwa juu ya wenzake hata kama ana Marks chini ya 20, wewe unasema ana akili simply kwakuwa yuko juu ya hao wengine! Unachokisema hapa ni kama iwapo kitu kitakosa ulinganifu, basi huwezi kupima ubora wake!
 
Mkuu, kumbuka wabongo tunajijua tulivyo, so tunaangalia the best miongoni mwetu maana sample zetu ndio hizi hizi.

Masudi alitegeneza gari ya umeme, tulimkubali sana kwa sababu kibongo bongo alifanya kitu kisicho cha kawaida, ila tungemlinganisha na wachina, tungemuonea bure.

Halafu pia u smart wa mtu wakati mwingine hutegemea aina ya wateja wako. Fikra mfano unahudumia watu wanaopenda umbea kuliko kula.
 
Kuna nini huko mkuu? ungetupa hint halafu utupe connection na mada.
Ingia king'amuzi cha Azam kisha fungua chaneli za Malawi ziko saba, kwenye taarifa zao za habari kwa kiingereza(huenda kikawa kikwazo) utajionea ambavyo watu na vyama vyote vinauhuru wa kujieleza bila kuzuiwa na polisi na mahakama, wako huru kumsema rais au IGP kama amekosea.
 
Rais Mama Samia ni mtu anayeamini kwenye siasa za ushawishi badala ya kutumia maguvu ‘Unnecessarily’.

Ni mtu anayeamini kwenye utu na muadilifu kweli kweli. Falsafa yake hii, humfanya asiwe anaangalia tu matokeo ya mwisho ya michakato, bali pia uhalali wa michakato yenyewe na kutumia busara ya hali ya juu ili kupunguza madhara na kuongeza tija (Ikumbukwe kila kitu kina pros na cons zake, kwa hiyo kiongozi tunampima kwa kuangalia ana maximize upande upi).

Rais Uhuru Kenyetta wa Kenya amekuwa mfano bora wa siasa za namna hii kwa miaka ya hivi karibuni na kuwa role model wa EAC kama sio Afrika nzima.

Hata hivyo sasa rekodi yake inavunjwa na mama kwa kuonesha viwango vya juu sana vya siasa za kistaarabu na kisasa.

Inaendelea...
Chawa kaziniiii
 
Mkuu, kumbuka wabongo tunajijua tulivyo, so tunaangalia the best miongoni mwetu maana sample zetu ndio hizi hizi.

Masudi alitegeneza gari ya umeme, tulimkubali sana kwa sababu kibongo bongo alifanya kitu kisicho cha kawaida, ila tungemlinganisha na wachina, tungemuonea bure.

Halafu pia u smart wa mtu wakati mwingine hutegemea aina ya wateja wako. Fikra mfano unahudumia watu wanaopenda umbea kuliko kula.

Hao sio best miongoni mwetu, mfumo wetu hautoi nafasi ya kupata watu bora, bali hupata yoyote mwenye uvumilivu na mazingira ya chuki, fitina, Majungu na ushirikina.

Ni kweli Masud tulimkubali kwa alichofanya na sio ubora wa alichofanya. Inaonyesha ww huzungumzii ubora, bali unawakilisha hisia zako tu zisizo na uhusiano na ubora.
 
Ingia king'amuzi cha Azam kisha fungua chaneli za Malawi ziko saba, kwenye taarifa zao za habari kwa kiingereza(huenda kikawa kikwazo) utajionea ambavyo watu na vyama vyote vinauhuru wa kujieleza bila kuzuiwa na polisi na mahakama, wako huru kumsema rais au IGP kama amekosea.

Ameathiriwa na mfumo CCM, na ameshiba zile propaganda za kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani, kumbe kiuhalisia sio kisiwa cha amani bali ni kisiwa cha majoga na wasiojua haki zao.
 
Hao sio best miongoni mwetu, mfumo wetu hautoi nafasi ya kupata watu bora, bali hupata yoyote mwenye uvumilivu na mazingira ya chuki, fitina, Majungu na ushirikina.

Ni kweli Masud tulimkubali kwa alichofanya na sio ubora wa alichofanya. Inaonyesha ww huzungumzii ubora, bali unawakilisha hisia zako tu zisizo na uhusiano na ubora.
Mkuu, nazungunzia ubora lakini katika mazingira yetu na sample tulizo nazo.

Waasiasa wa Tanzania ni lazima wawe watanzania na watanzania tunajijua. Mfano wengi wetu wana roho mbaya na za kichawi. Hivyo akitokea ambaye hana roho mbaya katika mazingira hayo tu, hilo tayari ni jambo kubwa. Lakini katika jamii ambazo hazina wachawi kwa mfano, 99℅ ya watu ni watu wa ungwana ambao hawadhulumiani wala kurudishana nyuma, hapo huwezi kuona upekee wa mtu muungwana kwa sababu ni kawaida kwenye jamii hiyo.
 
Kwa muktadha huu, hapa ni dhahiri huzungumzii ubora, bali unaoongelea uafadhali, ndio maana nikakuambia toka mwanzo kuwa Mama Samia sio kiongozi bora, bali ana afadhali kuliko Magufuli. Na hapo ni iwapo SI unit ni Magufuli. She is somehow fair only campared to Magufuli, but very far from good, very good or excellent.
 
Hebu nitajie kiongozi mmoja ambaye ni excellent Africa halafu uniambie kwa nini ni excellent! Ok tufanye duniani, usije ukasema Afrika ninekupa wigo mdogo sana wa kuchagua!

Nijuavyo mimi, tusemapo vitu ni vizuri au vibaya ni kwa kulinganisha na vingine. Lakini hakuna kitu kizuri au kibaya kwa ujumla wake chenyewe chenyewe tu.

Hata mwanga ni mzuri kwa kulinganisha na 'relative' giza kwenye eneo husika.

Ndio maana hatusemi ccm ni chama bora tukaishia hapo, bali tunasema ccm ni chama bora ukilinganisha na vyama mbadala vilivyopo. Ila usipolingalisha hivyo, ccm nayo inakabiliwa na changamoto nyingi tu.
 
Naomba nikuulize mleta hoja. Kwanini mama bado anakuwa na kigugumizi kwenye mambo makubwa kama kufufua mchakato wa kuandika katiba bora itakayowapa wananchi uhuru kamili wa kuchagua viongozi watakaoona wanafaa.?

Kwanini bado anaamini kuwa ni CCM pekee ndiyo inayopaswa kuchaguliwa kuongoza nchi na siyo mtu yeyote ambaye wananchi watamwona anafaa kwa wakati husika?
 
Back
Top Bottom