Mkuu
JokaKuu , Mama hakufukuza mtu kwa kutofautiana mitizamo. Na yeye alieleza mtizamo wake kuhusu mikopo na hayo ndio mapambano ya hoja. Aliyekuwa spika akajikuta anajichanganya na kushindwa kusimamia hoja yake. Mwisho baada ya kuyumba yumba akaona ajiuzulu. Ukisema alifukuzwa sio kweli.
Kuhusu watu kukamatwa, jamani sio kila kitendo kinachofanyika wafanyaji wanakuwa wametumwa na Rais, au Rais anakuwa anakifurahia. mambo mengine ni mitizamo, uelewa na tabia binafsi za mfanyaji. Kumlaumu rais ni kumuonea bure. Kama angeagiza au kutoka hadharani na kuunga mkono vitu vizivyo vya kawaida, hilo lingekuwa jambo jingine.