Sasa tunaweza kukubaliana kuwa; aina ya siasa anayoifanya Rais Samia ni ya kiwango cha juu sana ambapo ni nadra sana kuiona Afrika

Sasa tunaweza kukubaliana kuwa; aina ya siasa anayoifanya Rais Samia ni ya kiwango cha juu sana ambapo ni nadra sana kuiona Afrika

Ndio maana hatusemi ccm ni chama bora tukaishia hapo, bali tunasema ccm ni chama bora ukilinganisha na vyama mbadala vilivyopo. Ila usipolingalisha hivyo, ccm nayo inakabiliwa na changamoto nyingi tu.
CCM siyo chama bora ukilinganisha na vilivyopo, bali CCM ni chama kibovu kinachoongoza wajinga wengi. Endapo CCM Kingekuwa chama bora basi kwa wingi wa rasilimali zilizopo, Tanzania ingekuwa moja ya nchi zilizoendelea sana duniani. Chama bora huzaa viongozi bora. Chama bora hakiwezi kuwa na hofu mpaka kijikite kutetea mifumo mibovu ya uchaguzi, wizi wa kura, kubatilisha matokeo kwa mtutu wa bunduki, katiba mbovu, udikteta, kupiga marufuku siasa zinazopingana na waliopo madarakani nk.
 
MkuuTindo huwa tunapima uzuri au ubaya wa mtu/kitu kwa kufanya mlinganisho, hakuna kitu ambacho ni absolute kizuri au kibaya bali ni 'relatively'.

Extreme good ni malaika, extreme bad ni shetani katikati ni mtu.

Halafu sijui kwa nini utatumia vyama vya upinzani kama standard pekee kupima uzuri na ubaya wa rais huku ukijua kuwa hao wapinzani wenyewe ni chenga kichizi.
Wewe haupo reasonable kwa hoja zako. Umejikta kupamba na kutoa sifa tu kwa upande unaoona unakufaa bila kuonyesha results za wazi au hata za kuhisiwa za hizo sifa unazotoa.

Vipimo halali vya demokrasia siyo maneno ya kuokota hapa na pale bali ni matokeo yanayoonekana wazi.

Demokrasia ni universal concept. Kila mtanzania ana uelewa wa kutosha kukuthibitishia kuwa bado mama hajafanya lolote kurekebisha mfumo wa kidemokrasia nchini. AMESEMA MANENO YA HAPA NA PALE TU.

Bado hatujafanya uchaguzi hata mmoja tukaona kama vipimo vya kidemokrasia vimetimia.

Kwa hili hana anachoweza kujisifia.
 
Rais Mama Samia ni mtu anayeamini kwenye siasa za ushawishi badala ya kutumia maguvu ‘Unnecessarily’.

Ni mtu anayeamini kwenye utu na muadilifu kweli kweli. Falsafa yake hii, humfanya asiwe anaangalia tu matokeo ya mwisho ya michakato, bali pia uhalali wa michakato yenyewe na kutumia busara ya hali ya juu ili kupunguza madhara na kuongeza tija (Ikumbukwe kila kitu kina pros na cons zake, kwa hiyo kiongozi tunampima kwa kuangalia ana maximize upande upi).

Rais Uhuru Kenyetta wa Kenya amekuwa mfano bora wa siasa za namna hii kwa miaka ya hivi karibuni na kuwa role model wa EAC kama sio Afrika nzima.

Hata hivyo sasa rekodi yake inavunjwa na mama kwa kuonesha viwango vya juu sana vya siasa za kistaarabu na kisasa.

Inaendelea...
Kwa Hilo binafsi na mpongeza na pia naifananisha aina ya siasa anayofanya ni kama Ile ambayo imekuwa ikihubiriwa na chadema au kama ambavyo mdau mmoja ameifananisha na aina ya siasa anayoiamini Uhuru Kenyatta.
 
Naomba nikuulize mleta hoja. Kwanini mama bado anakuwa na kigugumizi kwenye mambo makubwa kama kufufua mchakato wa kuandika katiba bora itakayowapa wananchi uhuru kamili wa kuchagua viongozi watakaoona wanafaa.?

Kwanini bado anaamini kuwa ni CCM pekee ndiyo inayopaswa kuchaguliwa kuongoza nchi na siyo mtu yeyote ambaye wananchi watamwona anafaa kwa wakati husika?
Hana kigugumizi kwenye katiba mpya bali anataka kuwe na utaratibu mzuri na shirikishi ili mchakato ukianza uende smoothly na tusije kukwama kama tulivyokwama 2014.

Pia haamini kuwa ccm tu ndio wanaopaswa kuchaguliwa. Utakuwa umeelewa vibaya tu. Anaamini kuwa kiongozi na chama bora miongoni mwa waliopo/vilivyopo ndio kinapaswa kuchaguliwa ambapo kwa Tanzania CCM imewaacha wenzake kwa mbali sana kwa sababu mbalimbali.
 
CCM siyo chama bora ukilinganisha na vilivyopo, bali CCM ni chama kibovu kinachoongoza wajinga wengi. Endapo CCM Kingekuwa chama bora basi kwa wingi wa rasilimali zilizopo, Tanzania ingekuwa moja ya nchi zilizoendelea sana duniani. Chama bora huzaa viongozi bora. Chama bora hakiwezi kuwa na hofu mpaka kijikite kutetea mifumo mibovu ya uchaguzi, wizi wa kura, kubatilisha matokeo kwa mtutu wa bunduki, katiba mbovu, udikteta, kupiga marufuku siasa zinazopingana na waliopo madarakani nk.
Hapana mkuu, viongozi bora ni matokeo ya jamii bora na kinyume chake. Kwa bahati mbaya tuna jamii yenye watu wengi wa ovyo ambapo watu hao ndio hujiunga kwenye vyama randomly.

Kwa bahati mbaya zaidi kwenye vyama vya siasa vyote tanzania, hakuna mfumo intensive wa kuwatengeneza viongozi kwa kuwapa chakula cha ubongo bali vyama hu assume kuwa watu tayari ni competent automatically. Tatizo hili tumelijadili sana na bado ni serious.

Angalau kinachowasaidia CCM dhidi ya vyama vingine ni kwamba historia imeiweka CCM upande wa winners toka enzi za nyerere na hivyo kuweza kujijenga mifumo imara ukilinganisha na vyama mbadala.
 
Wewe haupo reasonable kwa hoja zako. Umejikta kupamba na kutoa sifa tu kwa upande unaoona unakufaa bila kuonyesha results za wazi au hata za kuhisiwa za hizo sifa unazotoa.

Vipimo halali vya demokrasia siyo maneno ya kuokota hapa na pale bali ni matokeo yanayoonekana wazi.

Demokrasia ni universal concept. Kila mtanzania ana uelewa wa kutosha kukuthibitishia kuwa bado mama hajafanya lolote kurekebisha mfumo wa kidemokrasia nchini. AMESEMA MANENO YA HAPA NA PALE TU.

Bado hatujafanya uchaguzi hata mmoja tukaona kama vipimo vya kidemokrasia vimetimia.

Kwa hili hana anachoweza kujisifia.
Unapofanya demokrasia kwenye jamii yenye watu wengi wanaopenda ujinga, umbea, uzembe, ushabiki na uchawi ( kupenda zaidi kuona watu wengine wanapata shida) unafiki n.k ni lazima uwe na tahadhari kubwa. Vinginevyo unaweza kusababisha janga la ajabu.

Jamii yetu ina watu wengi wenye uelewa na mitizamo yeye utata mkubwa. Ukiwaendekeza bila ya kuwa na utaratibu mzuri ni tatizo kubwa.

Kuna uzi mmoja niliandika kuwa demokrasia ni malaika na ni shetani. Sio dhahabu ambayo iko pale, kwa hiyo inabidi kwenda nayo kwa tahadhari.
 
Hebu nitajie kiongozi mmoja ambaye ni excellent Africa halafu uniambie kwa nini ni excellent! Ok tufanye duniani, usije ukasema Afrika ninekupa wigo mdogo sana wa kuchagua!

Nijuavyo mimi, tusemapo vitu ni vizuri au vibaya ni kwa kulinganisha na vingine. Lakini hakuna kitu kizuri au kibaya kwa ujumla wake chenyewe chenyewe tu.

Hata mwanga ni mzuri kwa kulinganisha na 'relative' giza kwenye eneo husika.

Ndio maana hatusemi ccm ni chama bora tukaishia hapo, bali tunasema ccm ni chama bora ukilinganisha na vyama mbadala vilivyopo. Ila usipolingalisha hivyo, ccm nayo inakabiliwa na changamoto nyingi tu.

Hakuna kiongozi excellent labda Mungu kama yupo. Nimekupa levels tu, lakini kuna viongozi wengi bora bila hata kuwafananisha na wengine kwani wanafikia viwango vya ubora. Hao viongozi bora utakapoamua kuwafananisha na hawa utopolo, unaweza ukahisi wako excellent.
 
Hapana mkuu, viongozi bora ni matokeo ya jamii bora na kinyume chake. Kwa bahati mbaya tuna jamii yenye watu wengi wa ovyo ambapo watu hao ndio hujiunga kwenye vyama randomly.

Kwa bahati mbaya zaidi kwenye vyama vya siasa vyote tanzania, hakuna mfumo intensive wa kuwatengeneza viongozi kwa kuwapa chakula cha ubongo bali vyama hu assume kuwa watu tayari ni competent automatically. Tatizo hili tumelijadili sana na bado ni serious.

Angalau kinachowasaidia CCM dhidi ya vyama vingine ni kwamba historia imeiweka CCM upande wa winners toka enzi za nyerere na hivyo kuweza kujijenga mifumo imara ukilinganisha na vyama mbadala.

Nimecheka kwa nguvu, eti CCM kwakuwa iko madarakani kwa sababu za kihistoria imejenga mifumo imara! Hivi unajua mifumo imara au umeandika hilo neno kwa bahati mbaya? Unajua hizi smartphone zina word suggestions, hivyo hilo neno la mifumo imara limejitokeza auto, ili kuokoa muda ikabidi uliache hivyo hivyo. Umeamua kutetea chama ambacho kinakufanya uonekane punguani.
 
Hivi mfano kilichotokea kwa wabunge 19 chadema, kama kinaweza kutokea chama kikiwa hakiko madarakani, unadhani kikiwa madarakani siku moja kitatokea nini? Kama yaliyotokea CUF ya lipumba yaliweza kutokea vile chama kikiwa hakiko madarakani, siku kikiwa madarakani tutegemee kuona nini? Kama nccr kimetokea kilicho tokea kwa namna kilivyotokea na nccr haiko madarakani, ikiwa madarakani tutegemee nini?

Kama tuna wenyeviti na.k wako madarakani kwa zaidi ya miaka 20, na vyama vyao havijawahi kushika dola, vikishika tutegemee nini? Kama kuna vyama vina karibu miaka 30 lakini kujenga ofisi za makao makuu tu vimeshindwa tusemeje sasa? Au sababu ni CCM?

Ni katika mazingira hayo, tunajenga hoja kwamba CCM ina uafadhali mkubwa. Sasa sababu za CCM kuwa na uafadhali ni zipi? Ndio hizo tumezieleza. Kwa sababu hatuwezi kusema kuwa eti CCM imekuwa bora tu kwa bahati nasibu kama ambavyo chadema imekuwa ikituaminisha kuwa eti mtu akijiunga tu na chama hicho tayari ni kiongozi bora akihama tayari ni fisadi. Huo ni uongo na ulaghai wa wazi sana.
 
Nimecheka kwa nguvu, eti CCM kwakuwa iko madarakani kwa sababu za kihistoria imejenga mifumo imara! Hivi unajua mifumo imara au umeandika hilo neno kwa bahati mbaya? Unajua hizi smartphone zina word suggestions, hivyo hilo neno la mifumo imara limejitokeza auto, ili kuokoa muda ikabidi uliache hivyo hivyo. Umeamua kutetea chama ambacho kinakufanya uonekane punguani.

Mifumo imara kwa kiingereza ni " STRONG Systems"; na kutokana na strong systems unapata strong Institutions! Unaweza kusema kwa mfano kuwa Tanzania ina bunge na Mahakama imara ? Bunge imara halipati maelekezo ya utendaji wake toka kwa Muhimili mwingine, na kwa Mahakama ni hivyo hivyo!! Bunge na Mahakama Tanzania zinapata maelekezo ya utendaji wake kutoka kwa Rais wa nchi; ilikuwa hivyo wakati wa Magufuli na iko hivyo sasa wakati wa Hangaya!!
Zinahitajika TAASISI ambazo hazitapata maelekezo juu ya utendaji tofauti na ilivyoainishwa kwenye katiba ya nchi!!
 
Kutokomeza njaa sio maana yake chakula kiwepo pekee, bali chakula kiwepo na watu waweze kumudu kukinunua!!! Maneneo matupu na ahadi za Bashe sio chakula!!!
Kwa sasa wasioweza kununua unaweza kuwaainisha? ni interventions gani ambazo ungependa zifanyike ili wasioweza kununua waweze?
 
Kwa sasa wasioweza kununua unaweza kuwaainisha? ni interventions gani ambazo ungependa zifanyike ili wasioweza kununua waweze?

Maisha ya binadamu pamoja na chakula, pia kuna mahitaji mengine muhimu yanayomfanya awe na maisha bora na si bora maisha!! Hivyo Serikali kutokuwa na kodi kandamizi zinawawezesha hasa wananchi wengi wa vijijini kuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji yao, hivyo basi interventions muhimu ni kuondoa kodi ambazo zinampunguzia mwananchi uwezo wa kupata mahitaji yake ya kila siku!!
Kwa siku hizi kwa vile watu wengi nchini hutumia Simu za mikononi kwa biashara na mawasiliano kwa ujumla, kufuta hizo TOZO za simu ni intervention muhimu sana. You can recoup the revenue you forfeit by abolishing TOZO by taxing the the super profits from the oil companies as well as scaling back the renumeration given to members of parliament.
Kaya za kipato cha nchini mijini na vijijini ndio waathirika wakubwa wa food deficit!!
 
Rais Mama Samia ni mtu anayeamini kwenye siasa za ushawishi badala ya kutumia maguvu ‘Unnecessarily’.

Ni mtu anayeamini kwenye utu na muadilifu kweli kweli. Falsafa yake hii, humfanya asiwe anaangalia tu matokeo ya mwisho ya michakato, bali pia uhalali wa michakato yenyewe na kutumia busara ya hali ya juu ili kupunguza madhara na kuongeza tija (Ikumbukwe kila kitu kina pros na cons zake, kwa hiyo kiongozi tunampima kwa kuangalia ana maximize upande upi).

Rais Uhuru Kenyetta wa Kenya amekuwa mfano bora wa siasa za namna hii kwa miaka ya hivi karibuni na kuwa role model wa EAC kama sio Afrika nzima.

Hata hivyo sasa rekodi yake inavunjwa na mama kwa kuonesha viwango vya juu sana vya siasa za kistaarabu na kisasa.

Inaendelea...
Kamshawishi nani?
 
Siasa safi ni kuwafanya wananchi wapate mkate wao na maisha yanayotabirika

Siasa ya kuwafanya wananchi wawe na njaa, haijawahi kupendwa na mtu hata mmoja

Labda huko juu keki inakoanzia!
Unataka serikali ikuletee mkate? Utasubiri sana...aiyefanya kazi na asile
 
Wote nyie ni Lumumba!
Siasa safi ni kuwafanya wananchi wapate mkate wao na maisha yanayotabirika

Siasa ya kuwafanya wananchi wawe na njaa, haijawahi kupendwa na mtu hata mmoja

Labda huko juu keki inakoanzia!
 
Eh.
Kugunaguna.
Tanzania ni moja za Nchi za Afrika ambayo uongozi na ushawishi wake ni wa hali ya juu, sasa tunalegalega.

Uongozi na ushawishi wake unafifiya(hili linauma) kwa sababu ya kutoa sera za mihemuko...sera zinazokinzana na sera za Uafrika za Ukombozi, halafu tunadiriki kusema ati 'tuna viwango vya juu vya
"Ustaa-arab" na siasa za kisasa!' Whaat?

Bado, ni mwaka mmoja tu hapimiki Fungueni macho na masikio katika siasa za kanda zinazonyemelea hivi sasa halafu tuone kama viwango vinvyotumika hapa yaani...siasa za kistaarabu na za kisasa zitaonyesha nguvu na ushawishi wa Nchi yetu Tanzania.
Sikubaliani
 
Watu wana maisha magumu mtaani wewe unasema ni mfano wa kuigwa? Rais gani asie yahisi machungu na magumu waliyonayo wananchi wake? Kwa suala la kuwatumikia wananchi wake, Rais Samia hawezi na hatamfikia Hayati Magufuli. Ila kwa kujikomba kwa MABEBERU, hapo sawa. Rais Samia ni mfano wa kuigwa!
 
Uk
Rais Mama Samia ni mtu anayeamini kwenye siasa za ushawishi badala ya kutumia maguvu ‘Unnecessarily’.

Ni mtu anayeamini kwenye utu na muadilifu kweli kweli. Falsafa yake hii, humfanya asiwe anaangalia tu matokeo ya mwisho ya michakato, bali pia uhalali wa michakato yenyewe na kutumia busara ya hali ya juu ili kupunguza madhara na kuongeza tija (Ikumbukwe kila kitu kina pros na cons zake, kwa hiyo kiongozi tunampima kwa kuangalia ana maximize upande upi).

Rais Uhuru Kenyetta wa Kenya amekuwa mfano bora wa siasa za namna hii kwa miaka ya hivi karibuni na kuwa role model wa EAC kama
 
Back
Top Bottom