SATIVA adhibitiwe kwa matusi ya nguoni anayotoa mitandaoni

Ndugu zangu Watanzania,

Kiwango alichofikia huyu kijana ni kibaya sana,ni kiwango ambacho hakihitaji kuvumiliwa wala kuachwa hivi hivi pasipo kudhibitiwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Kwa sasa anatukana matusi ya nguoni mpaka mtu mwenye hekima na akili timamu unabaki unaona aibu na fedheha kubwa.Ni matusi na lugha ambazo yeyote mwenye akili Timamu,mwenye hofu ya Mungu na mcha Mungu na aliyepata malezi mazuri ya wazazi wake hawezi kutukana wala kutoa iwe hadharani au mafichoni.

Sielewi huyu kijana kama wazazi wake wapo hai au walishatangulia mbele za haki.sielewi ikiwa huyu kijana ana ndugu wa karibu au viongozi wa Dini . sielewi huyu kijana kama amewahi hata kujua kama Mungu yupo na kwamba kuna siku sisi wanadamu tutakufa na kwenda kutoa hesabu mbele za Mwenyezi Mungu.sielewi kama huyu Kijana amewahi kuishi na wazazi wake na kulelewa katika ukuaji wake.

Anatoa lugha na matusi makubwa na yenye kuibua hasira,chuki na ghadhabu kubwa sana . Ni matusi na lugha ambazo hazikubaliki mbele ya jamii iliyostaarabika. Ni matusi na lugha ambazo haziwezi na hazipaswi kufumbiwa macho na kuachwa zipite hivihivi.

Huyu kijana anapaswa kudhibitiwa haraka sana.hawezi kuachwa aendelee kutukana matusi ya Nguoni.ni lazima akamatwe na kuwajibishwa kisheria.ni lazima afundishwe adabu ,ni lazima aambiwe huo siyo utamaduni wetu na siyo maadili yetu ya kitanzania. Ni lazima aambiwe wazi kwa vitendo kuwa popote pale Duniani hakuna uhuru wa kutukana matusi kama kichaa au mwendawazimu mbele ya watu waliostaarabika na ukaachwa hivi hivi.

Kama kuna mtu anaweza kuunga mkono matusi ya huyu kijana basi atakuwa ni mtu wa ajabu sana,mwenye matatizo ya akili,mwenye kukosa hofu ya Mungu na aliyekosa malezi ya wazazi wake na mwenye matatizo kichwani na asiyejitambua.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Ng'ombe mwenyewe akikoswa koswa kuchinjwa anachizika
 
..sativa hatukani mtu au watu ovyo, kama hupendi au una allegy ya kusemwa au kutukanwa, t s simple ondoka kwenye nafasi inayokuletea kutukanwa!
mchochee na kumpandisha mori na mihemko huyo muungwana, na umwambie aongeze bidii zaidi ya kuyaporomosha yale mazito mazito zaid, tena kwa mpangilio maalumu kama makombora ya Al-qas, ikiwa yanamsaidia kuongeza kipato chake..

akumbuke tu kuporomosha matusi sio ujasiri, ni ujinga 🐒
 
aisee na huku upo! basi naomba kuthibitisha kuwa Lukas mshamba ni chawa mkuu aliyefikiwa level ya utekaji! Mtafuteni huyu mshamba ale kichapo haraka!
 
mchochee na kumpandisha mori na mihemko huyo muungwana, na umwambie aongeze bidii zaidi ya kuyaporomosha yale mazito mazito zaid, tena kwa mpangilio maalumu kama makombora ya Al-qas, ikiwa yanamsaidia kuongeza kipato chake..

akumbuke tu kuporomosha matusi sio ujasiri, ni ujinga 🐒
..hatuishi kwa sababu ya kipato, ndio maana umekubali kuwa mpumbavu sababu ya kipato? hakuna anayemchochea, amefanya hayo mara kwa mara, tunashangaa wewe kuumizwa na matusi badala ya kuumizwa kwanza na waliomfanyia hicho kinachomfanya atukane!
 
Alichokifanya dogo Sativa sio kizuri kimaadili yetu sema wewe hauko fair.
Watu wanatekwa na kuuliwa hujawai kuandika andiko refu kukemea kama hili. Punguzeni uchawa vijana fanyeni kazi kwa maendeleo yenu ili musiwe wanafiki.
Kama unaona kuna jambo sijaandika.basi na wewe waweza kuandika ili nasi tusome na kutoa maoni yetu.
 
Ninyi ndio mnampoteza huyo kijana badala ya kumsaidia hata kwa ushauri wa kisaikolojia. Hivi hamuoni kuwa anaendelea kupotea kabisa.
Ameshawataja waliosababisha aathirike kisaikolojia lkn bado mnajitoa ufahamu. Ataendelea kutema nyongo hadi pale mtakapowakamata na kuwafikisha mbele ya sheria wabaya/watesi wake.
 
Halafu wajinga jinga wanaunga mkono matusi haya.namshangaa Robert mtibeli anaunga mkono ujinga huu
Hakuna anaeunga mkono matusi , ila siku kijana alipo tekwa na kuumizwa ambalo ni jambo baya zaidi ya matusi, haukuonyesha ishara yoyote ya kukemea , ndio maana waungwana wanaona kama kuna chembechembe za unafki 😅
 
Sijasoma uzi wako ila nimesoma heading tu nikaelewa.
Nikuulize tu mleta mada hivi siku ukitekwa wewe au mwanao akapitia aliyoyapitia huyo bwana mdogo Sativa utakuja hapa kuandika hiki ulichoandika?!
Matukio haya yana matokeo mabaya sana huko mbeleni maana hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kufurahia mwanaye apotezwe au kuachwa na kilema cha maisha halafu unataka asifu na kuabudu!
Dogo alieleza kila kitu lakini ameishia kupuuzwa kama mwendawazimu!
Haya angalia tukio la mzee Kibao Unaambiwa muuaji hajulikani na hili tukio la juzi mpaka clipp na picha na sura za wahusika zimeonekana kabisa lakini mpaka leo ishu imepita kimya kimya
Watu wana maumivu wanaogopa kusema ukweli kwa kuhofia yatawakuta lakini ipo siku roho ya kinyama itawavaa wananchi wengi na kitakachotokea ni balaa
Unalizaje swali wakati unakiri kuwa hujasoma? Ndio akili yako inakutuma kufanya hivyo? Ndio mijadala inavyofanyika hivyo?
 
Back
Top Bottom