SATIVA adhibitiwe kwa matusi ya nguoni anayotoa mitandaoni

SATIVA adhibitiwe kwa matusi ya nguoni anayotoa mitandaoni

Hajitambui kabisa yule jamaa.ndio maana anajiropokea tu chochote kile kinachomjia Mdomoni mwake
Na nyie ma CCM ndo wapumbavu. Huyo sativa kulikuwa hakuna haja ya kuhangaika nàe hadi kàtavi, mngemfukia pale mto ruvu, leo añgeshasahaulika. Sasa mmemwaçhia anatukana wazazi wake.
 
Pia mshawahi ata kujiuliza iyo SATIVA ina maana gani?
Mimi binafsi sishangai angejiita INDICA apo ninge doubt kwa anayoyafanya,
Niseme tu watekaji mliingia kwenye 18 za mtoto wa kona mbaya acha awanyooshe na msijaribu kufanya ujinga tena maana mtazidi kupoteza trust yenu kwa wananchi.
Kijana hana power yoyote ya kuwadhibiti watesi wake acha basi awavuruge matumbo akili ziwakae sawa.
Wewe nae mtoa mada punguza mihemuko hayo matusi ya SATIVA hatukani kwenye DM yako kama hupendezwi nayo acha kufuatilia nyendo zake na wanaomsapoti hutoyaona tena hayo matusi ..

Nawasilisha✍🏾
 
Sio kwa nia mbaya ila huyu dogo sativa hana adabu, hata kama alifanyiwa vibaya ila sio kwa matusi yale, na mbaya zaidi kuna watu wanampa sapoti + chadema na anashindwa kujua likimtokea jambo atapambana nalo yeye mwenyewe afu hao wanaompa kichwa wataongea tuu huko mtandaoni na itaishia hapo.
Mbaga jr.,haya yanayotokea huenda ni kuelekea ama kwenye hatua ya kukata tamaa ama tayari hatua ya shida ya akili,tukubali au hata kama tukikataa yapo mambo mengi ya kuvunja moyo,yakuhuzunisha ,yajukasirisha na yakuchosha yanafanywa kwa makusudi na kimfumo haya yasiwe tu sababu ya kupoteza udhibiti wa amani yetu siku moja.Hali hii ikiachwa kuendelea tusishange mnaosema wanakosa adabu wakaenea kama moto wa nyikani.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kiwango alichofikia huyu kijana ni kibaya sana,ni kiwango ambacho hakihitaji kuvumiliwa wala kuachwa hivi hivi pasipo kudhibitiwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Kwa sasa anatukana matusi ya nguoni mpaka mtu mwenye hekima na akili timamu unabaki unaona aibu na fedheha kubwa.Ni matusi na lugha ambazo yeyote mwenye akili Timamu,mwenye hofu ya Mungu na mcha Mungu na aliyepata malezi mazuri ya wazazi wake hawezi kutukana wala kutoa iwe hadharani au mafichoni.

Sielewi huyu kijana kama wazazi wake wapo hai au walishatangulia mbele za haki.sielewi ikiwa huyu kijana ana ndugu wa karibu au viongozi wa Dini . sielewi huyu kijana kama amewahi hata kujua kama Mungu yupo na kwamba kuna siku sisi wanadamu tutakufa na kwenda kutoa hesabu mbele za Mwenyezi Mungu.sielewi kama huyu Kijana amewahi kuishi na wazazi wake na kulelewa katika ukuaji wake.

Anatoa lugha na matusi makubwa na yenye kuibua hasira,chuki na ghadhabu kubwa sana . Ni matusi na lugha ambazo hazikubaliki mbele ya jamii iliyostaarabika. Ni matusi na lugha ambazo haziwezi na hazipaswi kufumbiwa macho na kuachwa zipite hivihivi.

Huyu kijana anapaswa kudhibitiwa haraka sana.hawezi kuachwa aendelee kutukana matusi ya Nguoni.ni lazima akamatwe na kuwajibishwa kisheria.ni lazima afundishwe adabu ,ni lazima aambiwe huo siyo utamaduni wetu na siyo maadili yetu ya kitanzania. Ni lazima aambiwe wazi kwa vitendo kuwa popote pale Duniani hakuna uhuru wa kutukana matusi kama kichaa au mwendawazimu mbele ya watu waliostaarabika na ukaachwa hivi hivi.

Kama kuna mtu anaweza kuunga mkono matusi ya huyu kijana basi atakuwa ni mtu wa ajabu sana,mwenye matatizo ya akili,mwenye kukosa hofu ya Mungu na aliyekosa malezi ya wazazi wake na mwenye matatizo kichwani na asiyejitambua.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Huyo kijana ni mtu mzima.Usihusishe wazazi wake wala malezi.Mtu mkamilifu akichukizwa au kuumizwa aachwe alie au atoe sumu mwilini mwake.Wewe kachome mbalagha ule Luca!
 
Back
Top Bottom