SATIVA adhibitiwe kwa matusi ya nguoni anayotoa mitandaoni

SATIVA adhibitiwe kwa matusi ya nguoni anayotoa mitandaoni

Anakwambia yeye alishakufa Katavi, hakuna anachokiogopa tena.

Kila mtu ana uhuru wa kufanya anachojiskia hasa pale nafsi inapofika kikomo cha uvumilivu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kiwango alichofikia huyu kijana ni kibaya sana,ni kiwango ambacho hakihitaji kuvumiliwa wala kuachwa hivi hivi pasipo kudhibitiwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Kwa sasa anatukana matusi ya nguoni mpaka mtu mwenye hekima na akili timamu unabaki unaona aibu na fedheha kubwa.Ni matusi na lugha ambazo yeyote mwenye akili Timamu,mwenye hofu ya Mungu na mcha Mungu na aliyepata malezi mazuri ya wazazi wake hawezi kutukana wala kutoa iwe hadharani au mafichoni.

Sielewi huyu kijana kama wazazi wake wapo hai au walishatangulia mbele za haki.sielewi ikiwa huyu kijana ana ndugu wa karibu au viongozi wa Dini . sielewi huyu kijana kama amewahi hata kujua kama Mungu yupo na kwamba kuna siku sisi wanadamu tutakufa na kwenda kutoa hesabu mbele za Mwenyezi Mungu.sielewi kama huyu Kijana amewahi kuishi na wazazi wake na kulelewa katika ukuaji wake.

Anatoa lugha na matusi makubwa na yenye kuibua hasira,chuki na ghadhabu kubwa sana . Ni matusi na lugha ambazo hazikubaliki mbele ya jamii iliyostaarabika. Ni matusi na lugha ambazo haziwezi na hazipaswi kufumbiwa macho na kuachwa zipite hivihivi.

Huyu kijana anapaswa kudhibitiwa haraka sana.hawezi kuachwa aendelee kutukana matusi ya Nguoni.ni lazima akamatwe na kuwajibishwa kisheria.ni lazima afundishwe adabu ,ni lazima aambiwe huo siyo utamaduni wetu na siyo maadili yetu ya kitanzania. Ni lazima aambiwe wazi kwa vitendo kuwa popote pale Duniani hakuna uhuru wa kutukana matusi kama kichaa au mwendawazimu mbele ya watu waliostaarabika na ukaachwa hivi hivi.

Kama kuna mtu anaweza kuunga mkono matusi ya huyu kijana basi atakuwa ni mtu wa ajabu sana,mwenye matatizo ya akili,mwenye kukosa hofu ya Mungu na aliyekosa malezi ya wazazi wake na mwenye matatizo kichwani na asiyejitambua.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Tukiweza kuwathibiti watekaji haya yote hatutayasikia!!


Unaacha mlango wazi ili akiingia mwizi umdhibiti!!? Pumbavu
 
Matusi aliyotumia jana kumtukana IGP hayakubaliki wala kuvumilika hata kidogo.ni ukiukwaji na uvunjifu mkubwa sana wa sheria na maadili yetu na kwa jamii yoyote ile iliyostaarabika haiwezi kukubali matusi ambayo anatukana huyu jamaa.ambaye mimi nahisi anamatatizo kichwani mwake yanayohitaji matibabu ya dharura.
Wanaharibiwa na kina Mbowe.
 
..km mtu hapendi kusemwa au kutukanwa juu ya yale anatendea watu akiwa kwenye nafasi ya umma, jibu analo yeye mwenyewe..ondoka kwenye hiyo nafasi! hutasikia mtu anakuongelea tena!aliyetekwa si mtoto wa mbowe, alitekwa sativa..na km wewe una uhakika viongozi wa chadema wanahamasisha watu kupambana na dola, why don't you deal with them direct?
Kutukana ni kosa la jinai. Kukosolewa sio kutukanwa. Hata katiba haijawahi toa uhuru wa kutukana. Hao mnaowapa vichwa ndo kila mara wanajikuta matatizoni huku nyie mkiwa mmetulia na familia zenu.
 
Maneno unayotamka ni km umelewa au una ufahamu mdogo wa mambo kias hujui tafsiri ya unachoandika..elewa hivi, ukipenda kukaa kwenye ofisi ya umma, uwe tayari kutukanwa, hutaki kutukanwa au kukosolewa toka kwenye ofisi ya umma, watakaa wale wanafahamu maana ya kutumikia watu! Ukitoka hakuna mtu atakutaja..!
muerevu umejaa mihemko na ghadhabu tu 🤣

tukana kwa maneno, ukijibiwa matusi yako kwa vitendo, huna haya ya kutia huruma na kusumbua wadau.

hayo ni matokeo ya utovu wa nidhamu 🐒
 
Kutukana ni kosa la jinai. Kukosolewa sio kutukanwa. Hata katiba haijawahi toa uhuru wa kutukana. Hao mnaowapa vichwa ndo kila mara wanajikuta matatizoni huku nyie mkiwa mmetulia na familia zenu.
Kutukana kunatokea baada ya jinai inayotokana na kukosolewa..tena jinai ya kuteka na kuua sabab amekosoa serikali, serikali gn haikosolewi..? waliomo ndani ya serikali ni malaika? Watekaji na wauaji wametajwa kwa majina lkn hata kuhojiwa tu hakuna, kwa hiyo kuna watu wako juu ya sheria? Yupo Mch. Mbeya analalamika mwanae kuuawa na Said masoro former DG wa tiss lkn serikali inajifanya haisikii..kwa hali ya namna hiya unataka mtu afanye nini, wewe unaona jinai anavyotukana lkn huona jinai zilizosababisha atoe matusi..!
 
muerevu umejaa mihemko na ghadhabu tu 🤣

tukana kwa maneno, ukijibiwa matusi yako kwa vitendo, huna haya ya kutia huruma na kusumbua wadau.

hayo ni matokeo ya utovu wa nidhamu 🐒
Punda wewe..ambia wanao hayo maneno sababu unawalisha! achana na mambo ya watu..when the day comes God takes care not you! endelea kula hayo makombo unayotupiwa na hao unawatetea, no one will remain in this world!
 
Back
Top Bottom