Upo sahihi sana. Sidhani kama watu wanaoamini kuwa huyu Lucas ana akili timamu, idadi yao inaweza kufika hata 10. Hata wanaCCM wenye akili timamu, wanajua kuwa huyu bwana kichwani na moyoni kumeyumba kabisa. Maana hakuna mwenye akili timamu ambaye ataona kuuawa na kutekwa kwa watu ni sawa alimradi kufanywe na CCM na agents wao ila hata kukemea tu juu ya matendo hayo machafu kukifanywa na wanaosadikika ni wa mlengo wa upinzani ni sawa.
Juzi nilikuwa safarini kuelekea Nyanda za juu, njiani, nikakutana na wakili wa mashtaka wa Serikali, katika kuongea, akasema, "huyu mama, hapana, anakoipeleka nchi siyo kwenyewe kabisa. Kitendo chake cha kuwakumbatia watekaji na wauaji mradi tu watu hao wanamkosoa yeye au serikali yake, ni maangamizi kwa nchi. Kama watu wangekuwa wanajitambua, ilitakiwa kumwondoa mara moja"
Tena jana nikakutana na mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM, wengine aliokuwa nao japo sikujua nafasi zao, lakini wote wanaCCM, yule mjumbe wa mkutano mkuu ni kama alikuwa anarefer mkutano walioufanya, akawa anawaambia wenzake, "watu huku CCM bado wanaipenda, tatizo ni huyu mama. Tena napenda ingekuwa inawezekana wapinzani wangechukua vijiji vingi ili wajye kuwa huyu atatupatia wakati mgumu mwakani. Sasa jana wamemkamata Mbowe na watu wengi wa upinzani, unafikiri pale tena CCM irapendwa!!".