Sauti ya Kiongozi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara akiponda ubunifu wa Gari ya Masoud Kipanya yavuja


Kipanya kafanya jambo kubwa ila kisanii , uzuri wa JF haina kubembeleza unachanwa ukweli na ukweli unakuweka huru , no kusifia sifia ujinga, alipozindua gar wadau wengi walijitokeza, lakni gari ikaonekana ni powerless , poor design na almost imeunganishwa unganishwa tuu vtu, sana sana alichofanya ni kuchora mchoro ambao nao alifeli tu ( aliuchora kikatuni katuni)

watu walimsifia na wakampa ushauri ,wahisani wakajitoa na akatengeneza pesa mingi tuu, wote haya tunayajua, jamaa akapotea kwenye karakana yake , no progress yyte ya maana , perhaps anataka aombe mpunga wa ruzuku serikalini kama mtanzania mwenye kiwanda cha kutengeneza magari , achukue mpunga alaf apite hv , wahuni wenzake wamemsanukia
 

Huyu waziri naye akisema ajagundua kitu anakuwa mjinga, hivi kwenye gari sasa hivi unagundua nini ambacho hakijagunduliwa?
 
Ukiona ndugu yako anaunganisha unganisha madude na kusema kagundua yafuatayo.

[emoji736] Katapila.

[emoji736] Helicopter.

[emoji736] Kituo Cha kurushwa matangazo ya redio.

[emoji736] Gari.

Kaa naye mbali zimeshalipuka tayari.
Ukisikia mawazo mgando ndio hayo
 
Nchi ngumu hii! Yaani hawaoni kama kuna ujuzi watu wanaupata, hata kama wanachofanya ni kuunga vipande vinavyotoka nje ya nchi? Wanafikiri tutaanzia wapi?
 
Masoud amejiajili Waziri ameajiliwa na kuajiliwa ni kumpa mtu maisha yako akuendeshe maana akili yako haitoshi kujiendesha
 
Kiuhalisia hayo mazungumzo hayana kasoro yoyote na huo ni ukweli halisi. Kwanini?

1. Kipanya alisema amevumbua gari lake. Kitu ambacho hakikuwa ukweli. Kipanya alifanya vehicle body design kwa kuboresha muonekano wa muundo wa magari ambayo yapo tayari duniani. Hakuna uvumbuzi wowote pale.

2. Hiyo clip ni mazungumzo ya ndani, binafsi au siri baina ya maafisa wa wizara, hivyo wahusika walikuwa huru kuzungumza ukweli bila chenga baina yao. Hiyo sio chuki wala kitu kibaya. Ni mambo binadamu huwa tunafanya kila siku kwenye maisha yetu ya kawaida.
 
Ile ilikuwa gari au takataka tu, Ule ulikuwa uhuni na hata sisi tunajua
 
Mbona kaongea ukweli?
 
Hebu tuwe realistic. Ilo gari alilotengeneza Masoud lipo katika category gani?
1. Invention
2. Innovation
3. Imitation?
Kwenye Invention najua halipo sababu tukimuuliza hata patent right hana. Innovation na kwenyewe hayupo sababu kigari kama icho ni kweli kinauzwa China.
Atapata support ya wasiokuwa na uelewa wa haya mambo ila nyuma ya pazia kwa vyovyote product yake haiwezi kwenda sokoni
 
Kiongozi kaeleza ukweli ila atachukiwa, kwamba lile ni gari?
Halafu unapoomba kibali toka kwenye mamlaka ni kwamba lazima u-comply kwenye TOR au Guidelines zao na siyo mamlaka ifuate unachotaka wewe muombaji. Serikali inatulinda sisi ambao baadaye tungekuwa wateja wa hayo magari dhidi ya ajali na majanga tarajiwa

Masoud anaweza akawa ni galacha kwenye Sanaa ya kuchora vikaragosi lakini siyo huku. Huku siyo kwake, atoke kabisa awaachie wenyewe.

Naona hata wanaomtetea ni mashabiki wa cartoon zake. Huku kwenye magari nawahakikishia ATAWAUA hata nyie mnaomshabikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…